Vimbwanga ndani ya vyumba vya mtihani.

Vimbwanga ndani ya vyumba vya mtihani.

Upo kwenye mtihan unakuta mwana anatumia vifaa vyote vya mkebe hafu wewe kapuku hahahaha ... Another booklet please akat wewe ndo kwanza page tatu unahangaika wapi ukondens hata kanyimbo ili umeonekana umeandika sana nyie jaman shule ... Shule achen iitwe shule .. Nawasalimu ndugu zangu pcb popote mlipo ... Phosphoenol pyruvate halet tena pyruvate now days wala atp .. Naye vyuma vimekaza .......
Huwa wanatisha sana
 
Nakumbuka nipo kwenye U.E Mi hata niwe nimesoma vip lazima niingie na mgombea mwenza kibomu. sa siku hiyo nawaangalia crew yangu wanajifanya wanaelewa et dk za mwisho ndo wanajifanya wanasolve na vitu vinasogea mi huwa sipendi mambo ya kujaribu maisha. Tumeingia wamekuta mambo kama miujiza tu vitu havieleweki, halaf maswali kama matatu hivi nnayo kwenye kibomu , nikawaambia nnayo mazee, wakataka niwaonyeshe nikawarushia vibomu shughuli ikaingia mchanga kibomu hakijafika kimeishia katikati Aiseee pale ndo niligundua rafiki wa kweli ni baba na mama yani kila mtu aligeuka upande wake kwamba hataki kujihusisha kisa kimeanguka vibaya eti...
Pole sana Mkuu sipati picha hiyo siku ulitamani ardhi ipasuke uzame
 
Wakuu Baba Swalehe na mkuu Theriogenology salaam kwenu.

Nimepitia maongezi yenu hapo juu, nimeshangazwa jinsi mlivoichambua Chemistry from atomic to molecular level kama vichaa vile... Yaani nimewapenda bure...

Kumbe nyie mazee ni vipanga wenzangu kabisa yani (hatutazami matokeo ya cheti, bali masomo ulosoma).

Sasa nimebaki najiuliza hapa iweje mkawa mnashangilia kuwa team MAPUGI huku mtabe mwenzenu nikiwa nabwekewa na mbwa majike-dume (MAPUGI).

By keeping other variables constant, rasmi leo hii nawatoa na kuwafuta kabisa kwenye banda ya MAPUGI. Nyie ni watabe... Wababe. Mmepita shule.
Ila engineer mkuu hahaha daah ila we jamaa mi sina neno ngoja nikae kimya .....
 
Kipindi hiko niko form three nilikuwa na swahiba wangu Laban, hapo tupo pared tukatangaziwa badala ya Biology tutafanya Geography hapo watu tumejiandaa full nondo na Bios tukitoka tukafanye Geog kesho yake. Tukapiga hesabuuuu, Laban akanambia hapa tulia tu, pepa tutafanya na itavyokuwa na iwe.

Tukakaa mbele kabisa, ticha akaja akagawa pepa watu mzigoni, kucheki swali la kwanza buluu, la pili buluu, la tatu patupu, kuna moja akaliona akanambia hili linaenda. Kulichek kweli linasogea tukaanza kufanta. Tukiangalia nyuma watu wanaofanya ni wachache wengi wanazuga tu. Ile ticha wakat anakuja kugawa pepa akawa amekuja na Burnet, nikamstua oya kitabu hiko, akanambia poa. Akakichukua tukaanza kula chabo swali kwa swali, ticha akarud tukafunika mchezo, tukatoka nje.
 
S
Inabidi uandike muandiko mkubwa ili uende nae sawa katika uchukuaji wa makaratasi
Sasa hapo unakuta mwandiko wako ni mwembamba kama wangu. Hata uandikeje, ukijitahidi sana unajaza pepa moja tu. Ila mwingine akija kuyakopi anaeza andika hata karatasi mbili na nusu
 
Nakumbuka enz hizo pandahill kuna ticha mmoja mlevi alisahisha marking scheme yake akapata 47 .. Aljsahau ... Alkua anasahisha huku amelewa ... Siku anakuja kugawa pepa ... Wa kwanza nan huyu hajaandika jina ... ***** hahaa kumbe ni yeye
Haaahaaaa
 
Aisee !! Mi nilikuwa napiga bao kabisaaa, pia kuna siku nililetewa taarifa kwamba nyumbani nimeibiwa, ile hali ya kua na haraka kuwahi home nikajikuta napiga bao
Hali ya kawaida.
 
Hahahhh...huyo mshikaji noma saana...Duuh.
Mi nakumbuka mshikaji mmoja alikuaga baunsa, aliingia na kibomu knye test ya programming akaweka chini ya question paper. Sasa katika kupitapita, lecturer akakiona kinachungulia chini akapeleka mkono kwenda kukichukua... Weeeee.. Huyo mshikaji alimkata jicho halafu akabana ile question paper na kiwiko. Daaah sikuamini macho yangu, yule lecturer aliogopa, ikabidi aendelee kusimama hapo hadi muda wa paper ukaisha. Baunsa akakunja question paper pamoja na kibomu ndani akatoka.
Matukio mengine yanahitaj ujasiri wa kuzaliwa au kuvuta bange, maana....hatare sana
Haha..jamaa alicheza kama pele[emoji16] [emoji16] [emoji16]

Nakumbuka enzi zangu navaa saa kubwa naandika nondo za programming kikaratasi kinakunjwa kinakua kidogo napitisha chini ya saa kimya
 
Muda wa kulala kwenye mtihani unautoa wapi..
hizi ni chai tu
 
tukiwa chumba cha mtihani CBE enzi hizo ukiona math ngumu unamtengenezea jamaa wa DIT kitambulisho chenye jina lako anenda kupiga paper fresh

sasa masnitch hawakosekani kumbe wakawatonya viongozi siku ya paper tunashangaa wasimamizi wanaingia na polisi venue after venue walipofika venue letu lilikuwa ni T4 bonge la hall wanakuja na mashine kama ya supermarket ile wanamulika kwenye kitambulisho kama kimetengenezwa CBE inapiga beep kama umetengeza nje hailii unapigwa pingu

nakumbuka kuna jamaa wa DIT alitoka mbio akampiga push HOD mmama alivyodondoka akamanyang'anya ile karatasi tuliyosign IN akakikimbia nayo alikimbizwa na polisi akaruka ukuta akadondokea makaburi ya upanga akatokomea 😀😀😀😀
Huyo jamaa unayemuongelea anaitwa mndewa alikua mzee wa kupiga ndondo cbe hiyo siku alichubuka ile mbaya, utakua umesoma juzi juzi baada ya tent kujengwa!
 
Mkuu mimi tangu nimeanza kusoma mitihani iliyonikamata kabisa ni michache mno, mara nyingi huwa namaliza kabla ya muda kwa kuwa naelewa nijibu nini japo ufaulu wangu ni wa wastani.
Mimi mtihani ukinijia vizuri ndio utapata sana, kwani kama ninatakiwa kufanya maswali matano nitafanya saba mwisho nakata mawili kulingana na uzito wake
 
umekata solution...alaf ile unaanza kurudia kufanya kwa usahihi unasikia''ZIMEBAKI DKK2'' ukicompare na solution utakayofanya mda hautoshi basi MKONO UNATETEMEKA NA MKOJO UNATAKA UACHIE TARATIBUUUU....haaaaah
 
Mimi mtihani ukinijia vizuri ndio utapata sana, kwani kama ninatakiwa kufanya maswali matano nitafanya saba mwisho nakata mawili kulingana na uzito wake
Hahahaha aiseeee.....kuna jamaa yangu alikuwa na tabia hiyo...anafanya maswali meengi then anachagua eti ni yapi amejibu vizuri zaidi. Kuna watu mko tofauti sana aseeee
 
tukiwa chumba cha mtihani CBE enzi hizo ukiona math ngumu unamtengenezea jamaa wa DIT kitambulisho chenye jina lako anenda kupiga paper fresh

sasa masnitch hawakosekani kumbe wakawatonya viongozi siku ya paper tunashangaa wasimamizi wanaingia na polisi venue after venue walipofika venue letu lilikuwa ni T4 bonge la hall wanakuja na mashine kama ya supermarket ile wanamulika kwenye kitambulisho kama kimetengenezwa CBE inapiga beep kama umetengeza nje hailii unapigwa pingu

nakumbuka kuna jamaa wa DIT alitoka mbio akampiga push HOD mmama alivyodondoka akamanyang'anya ile karatasi tuliyosign IN akakikimbia nayo alikimbizwa na polisi akaruka ukuta akadondokea makaburi ya upanga akatokomea 😀😀😀😀
haaaah haaaah wew jamaaa daah
 
Back
Top Bottom