Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Thanks ....i will make the best of it!wasalim airtel
 
Watoto wanafundishika. Ukimkanya kitu kwa karipio, hatathubutu kukirudia. Tabia ya kulea watoto kama mayai ndiyo inayo waharibu.

Hata kukaripia kunaharibu watoto. Watoto wote wenye akili timamu wanaokulia kwenye mazingira ya "literacy" wakifikia umri fulani huanza kushika kalamu na kupenda kuchorachora huku wameshika kalamu kaa vile mkuki. Wakianza shule ile hali ya kuandika andika huzidi na kutokana na ufahamu mdogo na shauku kubwa huandika popote. Kazi ya mzazi si kukaripia bali kutoa mwongozo kuwa achore chore na kuandikia wapi na si kumkaripia.
 
Miye wangu anapenda kufuatilia naongea na nani, utamsikia 'nani" namjibu rafiki yangu, atauliza tena anasemaje??? Nilichogundua yupo katika umri wa kuhoji, she is 2.4. Yaani kuna wakati nawaza sijui katumwa na mama yake anifuatilie nazungumza na nani!!!
Na tangazo la airtel kuna vikatuni vinaobesha vidole viwili analipenda hatari.
 
Karibu na tunapoishi kuna lodge ya kitalii, mtoto wangu wa miaka sita na wenzake walinyimwa kuingia akamwambia mlinzi "mbona tukija na mummy hautunyimi kwanza mama yangu amesema ananunua hii hotel". Yule mlinzi mbona aliwaruhusu. Baadaye mlinzi alikuja kuniuliza kama ni kweli hotel ilikuwa inauzwa. Nikiwa nashangaa kwa nini ananiuliza mimi, akaniambia 'mtoto wako kasema unainunua'. Mlinzi was so worried. Niliposikia story yote kutoka kwa dada nilimuelwa yule mlinzi.
 
Wangu ana miezi 9.5 anaita Baba,Mama , muda mwingi ana nisemesha mambo ambayo mimi siyaelewi yani eeeeb dadasa dodoo me huwa nina mwambia sawa kabisa anafurahi au wakati mwingine ninamwambia adi kesho anongea wee me nina mwambia swa kabisa!!! nifanye nini sasa wakati lugha gongana hapo!!
Au wakati mwingine nina mwambia mwambie mama yako
 
Halafu wangu haniiti baba, yeye ni mwendo wa kuniita baba Grace, vile anavyoniita mama yake.
Wakati wa kulala, nikimuambia sali, anagonga ile sala ya kuombea chakula, nadhani RCs wenzangu wanaipata hiyo.
 
Kuna watoto wengine wanachagua watu..akiwa analia ukitokea wewe ananyamaza na anakukimbilia umbebe!!
inategemea, ni lazima utakuwa umevaa fresh pia una mawe mfukoni ama kwa pochi na mkononi una smartphone iphone 7 plus la nguvu!!. This is natural bila maelezo ya ziada.
 
Huyo mtoto ni mdadisi sana. Hilo hayo maswali ya "nani" na "anasemaje" yanafurahisha sana.
 
Dah inauma sana, hawajui jinsi gani mtoto alivyokuwa na juhudi. Hakustahili kuadhibiwa yeye.
 
inategemea, ni lazima utakuwa umevaa fresh pia una mawe mfukoni ama kwa pochi na mkononi una smartphone la nguvu!!. This is natural bila maelezo ya ziada.
mmmmh wewe sidhani kama tupo pamoja
 
Mtoto wako anatazama movie kama za bongo movie ndio maana amejua kuna kitu kinaitwa mimba na kuolewa au amejifunza kutoka kwa watu. Katika umri huo ni mapema mno kufikiria mambo hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…