Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Watoto ni karaha, furaha, Amani na faraja kubwa kwetu sie Wazazi wao! Mambo ya Watoto ni mengi mengine hayana haja hata kuandika hapa!
 
Malezi duni mkuu, unajua watu wanadhani kumlea mtoto ni kumlisha, kumsomesha na kumvalisha wanasahau kuwasimamia na kuwaongoza watoto kwenye njia sahihi, wanawaacha watoto watazame chochote kwenye TV na kwenda kucheza kwenye mazingira ambayo si rafiki kwa akili ya mtoto na matokeo yake ndio hayo. Kwa mfano mtoto wa huyo mzee aliridhika kwa sababu aliona babake ana maisha mazuri na kitendo cha kukaa naye ofisini kilimjengea mtoto mtazamo wa uhakika wa kula bila jasho ndio maana mzee wake amemuona hayuko kama alivyotegemea.
 
Babyboy wangu wa miezi 6 yani nikimchemki DNA zangu kabisa naziona anavyolala anavyosmile akikasirika
 
Ugomvi wa mwanangu mgeni aje amsalimie mamake au mimi kwa kunikumbatia atalia mpaka basi , my dude is turning 2yrs next week.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Wangu mm ana 4 years yani yeye akiamka asubuhi Tu ni kuwasha laptop na kuanza kuangalia katuni hata Kula anasahau ,simu ya mamake ndo anaimiliki muda wote yy ni kuangalia katuni tu
 
Mdogo wake anaekaribia miaka 3 ni mtundu na mbabe. Yeye anapenda magari na ufundi. Yaani umuoneshe video ya magari kwenye simu imekula kwako huna jinsi ya kujitoa atakavyotupa tantrums.
Usije ukaanza kumlazimisha asome awe daktari au mwanasheria hicho ni kipaji tayari anacho kitamtoa aongezewe tu elimu kiasi sio madegree ili mzazi ujisifie.

Hongera sana Mkuu
 
Wangu 1.5 yrs anapenda kuandika andika kuna sehem yake ukutan ndo hapo hapo kila siku.kinachonishangaza zaid hatakag na hapend tushikiane simu mm na mama yake, nikishika ya mama yake anaichukua na kuitupa ila mama yake akiishika yangu anamnyan'ganya na kuniletea
 
Mtoto wako anatazama movie kama za bongo movie ndio maana amejua kuna kitu kinaitwa mimba na kuolewa au amejifunza kutoka kwa watu. Katika umri huo ni mapema mno kufikiria mambo hayo.


Itakuwa ni hizi Movie za Kibongo.... ila nashukuru sasa kanashinda shule akirudi amechoka sana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…