Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

[emoji16][emoji16][emoji16] watoto kweli ni rahaa
 
Watoto katika umri mdogo pale wanapokua wana shauku ya kujifunza kila kitu ni wanaleta burudani kweli kweli.
Mtoto anauliza baba hii redio ya nani? Unamwambia yetu wote
Anauliza yetu hata mimi?(akimaanisha yeye).
Kesho anauliza hiki kitanda cha nani[emoji23] [emoji23]
 
Wa kwangu ana miaka 3, kuna siku nimetoka safari nimekaa sebuleni akanifata na kuniuliza "baba leo unalala na mkeo?"
Siku ingine naongea nae kwenye Simu nikamtia mkwara ili ale chakula nae akanambia " baba ntakufumua" Daaaahh nkaona sasa hapa ipo haja ya kununua bunduki mapema.
Ikitokea akaona nimemshika mkono tu mama ake anakasirika sana na kwakua anajua mi haniwezi inabidi aanze kumpiga mama ake ili atoke hapo nilipo (Huyu jamaa anajionaga kama ye ndo ana hati miliki kwa mama ake)
Watoto ni raha sana, wana mambo yao ambayo ni ya kushangaza na kufurahisha kwa pamoja.
 
cuisine=aina/namna ya upishi wa chakula
Natumaini ulikusudia cousin.
 
Hilo la kuchorwa liache mumy halikwepeki mana kama kwangu ukija utacheka chumba kilichopona ni cha kwangu tu kwa sababu hawaingii hovyo hovyo ila nyumba nzima imechorwa chorwa na chumbani kwao ndio usiseme.
 
Da
Dah me hilo swala la kuchora ukuta nimepiga kelele hadi nimeamua niachane nalo achore hadi atakapopata akili ndo nipake rangi upya
 
Huyo ana dalili za wivu kama mwanangu , hata akiwa anacheza bize kiasi gani ukimkumbatia mama yake dogo anakuja mbio mbio anataka mama yake ambebe[emoji23] [emoji23]
 
Kuna watoto wengine wanachagua watu..akiwa analia ukitokea wewe ananyamaza na anakukimbilia umbebe!!
 
Mi mwanangu kuna siku nimetoka kazini nimechoka, mama yake yupo mbali kikazi...akaniambia baba kwanini usiwe na mke mwingine, yani alikua very serious!!!nikamwambia mama yako akijua atalia sana, akanijibu mama akiwa anakuja unamwambie mwingine aondoke mpaka mama atakapoondoka......aisee ni mengi sana, ila kwa kifupi he is real my friend.
 
Miaka mingap mkuu
Mitano mkuu huwa yuko mbali namm siku tukionana huwa haach gape anahakikisha ananiganda kila sehem napo enda juzi usiku wa UEFA nika mwambia naenda kuangalia mpira akanambia dady unampenda Ronaldo namm naenda kumwona nika mkatalia niusiku akachukua funguo anajidai ananifungilia mlango kutoka nje kavaa ndala moja yake moja ya maza ake namm kumkomoa nikaenda nae hvy[emoji23] [emoji23]
 
Hahaa. Kumbe ni karibia watoto wote tabia hiyo ya kuchora chora wanayo. Daah
Yaan ni balaa me mbaya zaid huwa wanapewa rangi za kufanyia hmwrk nyumban sasa naona zote zinaishia ukutan,ukiwa na mtoto mdogo kuna baadhi ya vitu kufanya ni ishu kama sitting room ukipanga akirud unakuta kumevurugwa balaa hapawez kuwa smart kama unavyotaka
 
Jembe langu lina miaka3,akimuona mtu flani akiongea kwenye tv,anakimbilia remote na kubadili chanel.Simply ana aleji naye.
Mtu gani Mkuu.?[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…