Hahaaa. I could talk about my kids the whole day.
Yule mkubwa wa almost 5 years ni mpole na ana hurumaaa. Pia anapenda sana ufugaji na ameshajua kuchanganya vyakula vya kuku. Anawajua kuku wake wakiumwa, anajua kuandika numbers kwenye kila yai linalotagwa na kuliondoa bandani. Pia anajua kufatilia aina ya kinyesi cha kuku kama ni cha kawaida ama ni cha kuumwa.
Mdogo wake anaekaribia miaka 3 ni mtundu na mbabe. Yeye anapenda magari na ufundi. Yaani umuoneshe video ya magari kwenye simu imekula kwako huna jinsi ya kujitoa atakavyotupa tantrums.
Wengi hupenda kusema nampendelea yule mkubwa lakini sio kweli. Ni rahisi kumuonea kutokana na sura yake ya kipole na huruma aliyonayo so nikisikiaga nywiiii amelia basi nageukaga chui. Because the lil man can surely take care of himself.