Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Kuna mtoto wa mpangaji mwenzangu hapa kitaa

Ni katoto ka kike kana miaka minne hivi....

Kuna siku nilikakuta kameandaliwa kuogeshwa,kalivyoniona tu hivi kakafichwa ikulu yake kwa kutumia mikono.

Duh!!nikajiuliza kumbe hata haka katoto kanajua pale kati haparuhusiwi kuonwa.

Na kwa nini hakakuficha/kuziba sehemu nyingine.
 
Wanangu 7yrs na 5yrs walikuwa wanabishana na binti Msaidizi wa kazi nyumbani juu ya udocta wa Rais wetu, maana walisikia kwenye habari wakisema dkt Magufuli, wakashangaa wakasema huyu kakosea maana huyu si dkt ni Rais yeye hatibu wagonjwa, dada alivyozidi kung'ang'ania wakamuuliza ni dkt wa hospitali gani?
Pia walishangaa kumwona alipoenda muhimbili na mke wake mama Janet, wakauliza huyu kwani ana wake wawili? Nikawaambia hapana wakasema mbona huyu nae wamesema ni mke wa rais? Ilibidi niwaulize nyie mnamjua yupi? Wakasema si mama Samia Suluhu? Ikabidi niwaeleweshe yule si mke wake ni makamu wa Rais lakini walikubali tu yaishe, maana picha nyingi wanamwona yupo pembeni yake.

My boy 3yrs alinifwata jikoni na kuniambia sili chapati za dada nataka unazopika wewe, nikamjibu hizi za baba, akadai hata yeye atakuwa baba. Nikamwambia baba ndie ameleta haya mayai namtengenezea mwenyewe, akajibu na mimi nikiwa baba nitakuletea hayo mayai.
Nikashindwa mie.

Siku dada yake akasema leo mama mimi nalala na wewe chumbani kwako, dogo wakiume akasema weeee hamna chumbani kwa mama wanalala boys tu, baba boy na mimi boy.

Kwa kweli watoto ni baraka na Furaha ndani ya nyumba, unaweza toka huko umeudhiwa ukifika home unasahau yote.
 
Wazazi wapya.
 
hii kitu mwanangu wa mwaka na nusu naye anayo anasema pot kukojoa ukigeuka hayupoo, anapigana sana na dada yake ukimuudhi anakuvizia na kitu anarusha huyoo anakimbia...ana vituko viingi nikieleza hapa sitamaliza.
 
Nilipomaliza chuo nilifanya kazi kampuni moja ya binafsi, ilikuwa ya ukandarasi huyo bosi alikuwa na watoto 6, kati ya hao mmoja tu ndio alikuwa wa kiume na wa mwisho mwisho kuzaliwa, akawa anasema natamani ingekuwa na uwezo wa kumvuta mtoto akue haraka ili huyu jembe anisaidie majukumu wakati huo alikuwa class seven, sasa hivi yule kijana kamaliza chuo ana degree baada ya kumaliza form four pale ST.. Costantene Arusha akampeleka chuo Nairobi, ila jamaa amekuwa MZIGO, ZOBA yaani hana afanyalo pale zaidi ya kuendesha magari ya baba, siku moja nikaenda kusalimia maana nilishaondoka kitambo hapo, nikamuuliza vipi sasa amekua kuna msaada unaopta kama ulivotamani kumkuza fasta, aliniangalia kwa huruma sana yaani kama anajuta mtoto kukua, alijua acha tu nibebe msalaba wangu nikifa vikiisha basi sitakuwa na la kulaumiwa, nilimuhurumia.. Alipokuwa mdogo alikuwa anapenda sana kuja ofisini na hukaa na mzee wake kwa umakini kama kuna jambo ana hakikisha haliharibiki.
 


Mama aliwahi kuniambia kwamba mwanamke akienda kwao na mtoto mdogo 0-6years akirudi walikua wakimlipisha fain. Maana aliondoa furaha ya familia
 
Ana miezi 5 yeye hata akiwa analia jifanye unaongea na simu ananyamaza kusikiliza maongezi ukiacha tuu anashusha kilio....anapenda sana kusikiliza maongezi ya simu hata kama anasinzia ataamka
Duh dogo ana nyota ya Umbea.[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 


Tatizo shule alizompeleka
 
Ulikuwa unaitolea [emoji102] ndo maana
 
Ni jukumu letu kama wazazi kuwalea watoto katika njia ipasayo, akimpendeza Mungu maana mwisho wa siku tutaulizwa kwanini huyu mtoto yuko hivi?

Tusifurahie matendo wafanyao watoto, huku hayo matendo tukijua kabisa yatakuja kuwa na athari kwenye maisha yake ya baadae, mtoto mdogo kupiga wenzake, kudanganya unajitafutia matatizo ya huko mbeleni.
 
mimi wa kwangu ana 3yrs anamuita mdogo wake wa mwaka na nusu "mwanangu' Na
huyo wa mwaka na nusu karibu kila siku lazima aamke saa 11 au 12 kasoro siku akipitiliza lazima nichelewe kazini..
Na akiamka nyumba nzima tunaamshwa sababu lazima atoke,,alie kufunguliwa mlango akaite kinadada..Na
Siwezi kununua zawadi ya mmoja lazima ninunue mbili lasivo kunatokea vita ya majimaji hapo ndani..
Na ole waone hata mkono umeshikwa tu na baba yao ni atamwambia mwache na kuanza kulia,,,amewahi kuongea yupo kama kasuku,,,
ukuta wa home ni balaa lingine..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…