Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Watoto bwana raha sana,mwanangu anajua kila kitu kilichomo ndani ni cha nani na ana miaka 2 na 6months, akiaja mgeni mama akimwazimisha kitu inabidi afichww kwanza hataruhusu kitoke home,wife akivaa tishert yangu itabidi aivue tu huo msala balaa,kuna siku kaniaibisha[emoji23] [emoji23] [emoji23] nilichukua cm ya wife nikaondoka nayo tukiwa nae dah!
 
kuna haka kamoja ndo balaa kabisa,
mama: itabdidi uhame chumba umeshakuwa mkubwa, kitanda hakitutoshi watatu!!
mtoto: kwani mi na baba nani mkubwa?
mama: baba......
mtoto: basi baba ndo ahame yeye ndo mkubwa kuliko mimi!!!!!!
mama alikosa jibu. watoto burudani sana aisee, mnaweza mkawa mnacheza naye anacheka lakini ndani ya dakika moja akaaza kulia unashindwa kuelewa imekuwaje.
 
Nmeipenda #3
 
Naombeni kujua kuna mtoto wa jirani yangu ana 3yrs lkn hawezi kuongea hiii itakuwa ni nn na afanyaje ili mtoto wake aweze kuongea?

Naombeni msaada wenu tafadhali
 
Vioja vinafanana,mwanangu anapenda kuvaa viatu vyawakubwa, anapenda sfr namsosi ukiwekwa mezani yeye ndio wakwanza kuketi,akisikia
Geti linafunguliwa wakwanza kufika getini ili amuwaoo anaeingia nakupokea alichobeba hasa Asa pochi akiamini kuna zawadi Zake. Jamani watoto wanajua kutupa raha
 
Ana miezi 5 yeye hata akiwa analia jifanye unaongea na simu ananyamaza kusikiliza maongezi ukiacha tuu anashusha kilio....anapenda sana kusikiliza maongezi ya simu hata kama anasinzia ataamka
Dalili za Shilawadu
 
Yuko na mama yake huko anakopiga job (as no uhamisho) ana 2.6 yrs siku mbili mfululizo kagoma kila kitu anataka amwone baba...nikipiga simu analia tu na kusema njoo huku haraka, niletee mkoba na peni!!!!
Jamaniiiiii( with a smile)
 
Wangu ana miez 4 kidume

Halali mpaka alie sana

Nikimgusa mama yake lazima aamke hata kama ana usingiz fofo

Anapenda kuona mwanga wa simu hata kama analia VP ukimwashia simu tu ananyamaza

Anapenda kuangalia TV sijui hata kama anaelewa

Akianza kuimba hapo mavoko akasome....
 
Nkimpata na mimi wakati muafaka utakapo fika ntakuja kuelezea vituko vyake ukuuu
Ila watoto nliobahatika kukaa nao ni wa Dada na kaka zangu yaani ukikaa nao hawa boi ata kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…