Viongozi hawa wamesema Hayati Magufuli aliongoza nchi vibaya sana, wewe je?

Alafu sisi wananchi millioni 60 tunasema Magufuli aliongoza vizuri.

Ikiwekwa picha ya Magufuli vs hao viongozi tumchague nani bado picha ya Magufuli itawaacha mbali sana.
Sema wewe
 
Kiukweli wote wameongea kweli tupu, na kwa uchache wao wanawakilisha kundi kubwa sana! Ukitaka kujua ukweli wa hilo fuatilia matukio ya namna watu katika sehemu mbalimbali walivyopokea kwa shangwe taarifa za kifo cha mwendazake, lait kama yale matukio yote yangerushwa kwenye vyombo vya habari ndipo watu wangejua ni jinsi gani mwendazake alikuwa na maadui wengi aliojitengeezea mwenyewe kwa maneno na matendo!
 
Hayo yote uliyoyaandika hvi unahisi tanzania ingelikuwa HV.siku mkitawaliwa na dicteta si mtasema magufuli alikuwa mwema sana.IPO siku mtamkumbuka ,ni mda tuu ndio utatupa jibu
 
Hii nchi mpaka kumchagua mbarubaru majnuni yule mara mbili inaonekana tuna tatizo kubwa sana.

Nyie si ndomlisema mnataka nchi ichukueliwe na jeshi. Au mmesahau jinsi mlivyokuwa mkimtukana mzee mtanashati Kikwete. Kweli nimeamini kwa binadamu hamna jema. Ndiyo maana aliyewaumba kaamua awaangalie tu mnavyojivuluga.
 
Unaposema "nyie" unamaanisha kundi gani? Na mimi unanihusishaje na kundi hilo?

Mimi niliwahi kusema hivyo lini?

Mbona kama unaniunganisha na kundi nisilolijua kwa kauli ambayo sijaisema?

Unaweza kunipa nukuu ya maneno yangu mwenyewe niliposema hivyo ili tujue kwamba nilisema maneno hayo kweli na hujanisingizia tu kwa uongo?
 
Usiwe muoga hivyo Kiranga. Kuna kundi kubwa la waTanzania (kama wewe haukuwa miongoni mwao naomba nisamehe bure) waliokuwa wakitamani sana nchi pendwa Tanzania ichukuliwe na jeshi. Hilo nina imani kuwa unalikumbuka.
 
Hakuna mantiki yeyote .....
 
Usiwe muoga hivyo Kiranga. Kuna kundi kubwa la waTanzania (kama wewe haukuwa miongoni mwao naomba nisamehe bure) waliokuwa wakitamani sana nchi pendwa Tanzania ichukuliwe na jeshi. Hilo nina imani kuwa unalikumbuka.
Usiunganishe watu kijumlajumla.
 
Ongeza list Samia, kigwangala, kikwete, Nape, Ndugai.

Sasa kama hawa waliokuwa wanalipwa na kula pesa kutoka kwake wanasema hivi mimi mchuuza dagaa hapa soko la Kibaigwa nitasemaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…