Crimea
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 25,874
- 36,030
Dada ukiandamania chumbani?I'm also on my way to leave this land of thugs, whose "boss" is barbaric and embracing thuggery.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dada ukiandamania chumbani?I'm also on my way to leave this land of thugs, whose "boss" is barbaric and embracing thuggery.
Lissu alipigwa risasi 16+ , ikiwa ni baada ya kutishiwa kama sasahivi wanavyodai kutishwa. Mbaya zaidi wapiga risasi,watekaji, wapotezaji, .......... hawajulikani!Kama wanataka kumuua angefika hata huko Namanga? Acheni uongo wenu.
Fungua akili yako kidogo tu, na usiwe shabiki maandazi.Hii ni dalili kuwa hamlitakii mema taifa letu na ipo siku mtaliletea janga kubwa. Ndio maana aliyekuwa mbunge wa Temeke kupitia CCM aliwahi kutoa ombi kuwa Chadema ni chama cha wapenda vurugu hivyo kinastahili kufutwa.
Baada ya kushindwa uchaguzi kwenye box la kura na wananchi kuichagua Ccm sasa mnataka kuiaminisha jumuia ya kimataifa kuwa hapa Tanzania kuna ukiukwaji wa haki za binadamu. Je mbona mlipokuwa wabunge hizi propaganda zenu hatukuzisikia?
Sasa hivi mmezua mchezo mchafu eti mnatafuta hifadhi kama wakimbizi wa kisiasa kuwa kuna tishio la kuuliwa na vyombo vya dola. Mnachotaka tu ni kuchafua taswira ya nchi yetu kuwa hakuna amani na kuna ukiukwaji wa haki za binadamu. Je kama kuna ukiukwaji wa haki za binadamu mbona UN wapo kimya na wana ofisi hapa Tanzania.
Kama vyombo vya dola vilitaka kumuua G Lema wangemuacha yupo salama wiki zote hizi mbili tangu uchaguzi uishe? L Nyalandu anatafuta kick kuwa anakimbia kuuliwa hivi mwanasiasa ambae unataka kuuliwa watu watakuacha hizi siku zote upo salama?
Godbless Lema alipokuwa mbunge alikumbana na kesi nyingi sana,na mpaka alikaa mahabusu miezi minne mbona alipotoka mahabusu hakukimbilia Kenya kwenda kuomba hifadhi kama mkimbizi wa kisiasa?
Kwa ujumla ni kutokubali matokeo ndio sababu ya kutaka kuchafua taswira ya nchi yetu. Na kukosa ubunge ambao kwenu mlidhania nia ajira za kudumu ndio sababu mnataka kwenda kujifanya wakimbizi.
Na hii propaganda mlioamua kuitumia itabuma na mtaaibika zaidi na huu ndio unaenda kuwa mwisho wenu mbaya kisiasa. Maana watanzania wana akili na hawadanganywi kitoto.
Nota bene : Kila propaganda mlizoanzisha zote zilibuma,kumbukeni wakati wa Covid-19 mlipata aibu kubwa,amabayo imewanyima kura.
Mbona aliweza kurudi na kufanya kampeni pasi na kuhakikishiwa usalama?Kama mmeshindwa kumuhakikishia Lissu ulinzi wake mpaka leo, unataka wafanyeje? unaweza kukaa sehemu usiyo na amani?
Upinzani sio uadui, fungueni akili zenu.
Umeandika nini?Fungua akili yako kidogo tu, na usiwe shabiki maandazi.
Kwanini uwe na chuki kwa bindamu wenzio.
Kwani siasa ni ugomvi
Unataka watu wakitendewa ndivyo sivyo ,wapongeze tu. Ulisikia wapi
Hata kunapokuwa na mechi ya simba na yanga, kunakuwa na malalamiko juu ya goli au magoli yaliyofungwa na upande mwingine. wewe unataka refa akikosea asiambiwe
Unadhani kama watu wanataka kukuua ukiwa Kenya hawawezi kukufuata? Huyu anaeneza sumu mbaya kuchafua nchi yetu. Kama walitaka kumuua wangemuua mapema tu.Kwa hiyo ulitaka g. Lema na nyalandu wauawe kwanza halafu wafufuke ndo wake kusema kuwa wanafatiliwa?
Sijui kwa sehemu nyingine. Ila kwa TUNDUMA walikomba sio kuiba kule. Hata mbele ya Mungu akiniuliza kuhusu TUNDUMA ntajibu.Kura ziliibiwa wapi? Mnatengeza clip za uongo kuaminisha watu upuuzi! Kama waliiba si mfungue kesi na sio kwenda nje kuwa wakimbizi.
akina nani hao wauaji. inaonekana unawajua.Unadhani kama watu wanataka kukuua ukiwa Kenya hawawezi kukufuata? Huyu anaeneza sumu mbaya kuchafua nchi yetu. Kama walitaka kumuua wangemuua mapema tu.
Mimi siwajui ,ila hata kama una jirani ana uhasama na wewe akitaka kukuua hawezi kusema anakuua kimya kimya. Hii ya kutishiwa wiki mbili ni uongo tu.akina nani hao wauaji. inaonekana unawajua.
ipo siku nawe yatakukuta, we endelea kushabikia ujinga
Non sense na nje ya mada.Hivi wewe ulikuwa wapi wakati viongozi wa CHADEMA walipokamatwa na kuambiwa watafunguliwa mashitaka ya ugaidi hivi kweli hao wabunge wastaafu ni magaidi. Wewe unaona sawa wananchi wa tanzania kunyimwa haki yao ya huduma ya internet. Wewe unaona sawa watu walivouwawa huko pemba ili kupitisha wabunge wa chama tawala. Huo uchaguzi unaousema wewe ni huu huu ulikuwa na mabegi ya kurazilizopigwa mtaani tena wakionesgwa polisi wameyashikilia. Hivi umeshamsikia enani kafikishwa mahakamani kwa hivyo vitendo vya jinai
Watu wa aina ya mleta mada ndio wanao haribu hata nyumba za Dada zao kwa kutembea na shemeji wakati Dada hayupoHii hadithi unaweza kuwasimulia watoto wa Dada yako hapo sebleni kwa shemeji yako wakakuelewa.
ila jumuia za kimataifa zinafahamu kuwa lisu alipigwa risasi kibao,na hakuna aliyekamtwa,twasira yetu imeharibiwa na ccm academia,ccm asili isingetufikisha hapaHii ni dalili kuwa hamlitakii mema taifa letu na ipo siku mtaliletea janga kubwa. Ndio maana aliyekuwa mbunge wa Temeke kupitia CCM aliwahi kutoa ombi kuwa Chadema ni chama cha wapenda vurugu hivyo kinastahili kufutwa.
Baada ya kushindwa uchaguzi kwenye box la kura na wananchi kuichagua Ccm sasa mnataka kuiaminisha jumuia ya kimataifa kuwa hapa Tanzania kuna ukiukwaji wa haki za binadamu. Je mbona mlipokuwa wabunge hizi propaganda zenu hatukuzisikia?
Sasa hivi mmezua mchezo mchafu eti mnatafuta hifadhi kama wakimbizi wa kisiasa kuwa kuna tishio la kuuliwa na vyombo vya dola. Mnachotaka tu ni kuchafua taswira ya nchi yetu kuwa hakuna amani na kuna ukiukwaji wa haki za binadamu. Je kama kuna ukiukwaji wa haki za binadamu mbona UN wapo kimya na wana ofisi hapa Tanzania.
Kama vyombo vya dola vilitaka kumuua G Lema wangemuacha yupo salama wiki zote hizi mbili tangu uchaguzi uishe? L Nyalandu anatafuta kick kuwa anakimbia kuuliwa hivi mwanasiasa ambae unataka kuuliwa watu watakuacha hizi siku zote upo salama?
Godbless Lema alipokuwa mbunge alikumbana na kesi nyingi sana,na mpaka alikaa mahabusu miezi minne mbona alipotoka mahabusu hakukimbilia Kenya kwenda kuomba hifadhi kama mkimbizi wa kisiasa?
Kwa ujumla ni kutokubali matokeo ndio sababu ya kutaka kuchafua taswira ya nchi yetu. Na kukosa ubunge ambao kwenu mlidhania nia ajira za kudumu ndio sababu mnataka kwenda kujifanya wakimbizi.
Na hii propaganda mlioamua kuitumia itabuma na mtaaibika zaidi na huu ndio unaenda kuwa mwisho wenu mbaya kisiasa. Maana watanzania wana akili na hawadanganywi kitoto.
Nota bene : Kila propaganda mlizoanzisha zote zilibuma,kumbukeni wakati wa Covid-19 mlipata aibu kubwa,amabayo imewanyima kura.
mtadanganya nani nyinyi mnasemaga kuna amani ,,baadae mnapiga watu risasiAmefanya kampeni miezi miwili kuna mtu alimgusa? Nchi hii inafuata misingi ya sheria. Anaogopa nini?