Noti mpya tz
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 974
- 247
Kwa mtu ambae amekuwa anafatilia matukio ya unyanyasaji na mauaji ya wafuasi wa CDM binafsi sioni sababu ya CDM kuendelea kukaa kujadili chochote na jeshi hili. CDM wanajua kabisa mpango uliopo uliosukwa na ccm kwa ajili ya kuwamaliza kabla ya mwaka 2014, wanajua kila kitu, wanakumbukumbu ya kesi walizofunguliwa za uonevu na jeshi la polisi na bado wanendela kuhudhuria mahakamani pamoja na kuwa baadhi ya kesi zimeishia jalalani, wanakumbuka jinsi walivyozushia na jeshi la polisi kule Igunga na sehemu zingine nchini, wanakumbukumbu ya mauaji ya wafuasi wao pale Arusha Janury 2011, wanakumbuka pia jinsi mwenyekiti wao wa USA RIVER alivyochinjwa na polisi haikuchukua hatua sitahiki, wanajua jinsi wabunge narudia hapa WABUNGE wao kule Mwanza walivyotaka kuuawa na mbele ya jeshi la polisi na wanajua mambo mengi yanayofanywa kwa maelekezo ya jeshi hilo ngazi ya juu na serikali lengo likiwa ni kuwamaliza kabla ya 2014.
Sasa mimi najiuliza, hawa cdm nao hawasikii? hawajui? au wameamua kuacha wapotezwe? Mara ngapi wamekaa na jeshi la polisi na kukubaliana na baada ya wiki mbili wakitaka kufanya mikutano na maandamano hali hujirudia vile vile? Kuna haja gani basi ya kukutana na IGP kwamara nyingine baada ya mauaji? Ina maana CDM hawawajui maadui zao ambao wanawavizia kwenye mikutano yao na kufanya mauaji kisha wanaelekeza kwao? Ivi mpaka atakapokufa nani ndio CDM waseme sasa imetosha? Mimi si mtabiri lakini mbele yetu nauona msiba mkubwa wa viongozi wa chama hiki kilichojifanya bubu na kufanywa kama TOI linalogeuzwa geuzwa bila lenyewe kujitambua.
CDM wajue kuwa mipango yote hii ni kwa ajili ya kuwamaliza wao na chama chao kabla ya 2014 na ccm wanatafuta cha kuwaeleza wananchi.
Lakini upumbavu mkubwa wa chadema ni kudhani kila yanapofanyika mauaji na jeshi la polisi wanenda kukaa na uongozi wa jeshi ngazi ya juu na kupewa maneno na ahadi tamu na kujisahau mpaka tukio lingine tena litakapotokea wanadhani adui yao mkuu ni ccm tu.
CDM sasa wanalazimika kuitisha maandamano ya nchi nzima ambayo hayatarudi nyuma mpaka uongozi wa jeshi utakapojiuzulu bila kujali vitisho na mauaji yatakayotokea vinginevyo namuona kiongozi wa CHADEMA akiuawa kwenye maandamo na nitakuwa mtu wa mwisho kutoa pole.
Tanzania kuna TUME YA HAKI ZA BINADAMU... sijui kama inafanya kazi na sijui wanafanya kazi gani wao wanasubiri migomo ya madaktari ndo watoke waonekane. Nchi yetu hii imekuwa ya matukio tu likija hili linapita na tunasubiri lingine, ndugu zangu Syria haikuanza na mauaji ya watu 100 ilianza na mauaji ya mtu mmoja mmoja mpaka wakafikia hapo walipo na hata sisi huu ni mwendo tu kama hatutachukua hatua leo kesho watakuwa 20 tutaona ni kawaida na tutasonga mbele watakufa 50, 70, 90 na hata 100 tutakuwa tumeshazoea tutasonga mbele mpaka hapo mataifa mengine yatakapoinuka kukemea nasi tutafuata mkumbo tukiongea kwa sauti kali na kutokwa na mishipa ya shingoni kama waimbaji.
R.I.P Daud Mwangosi wewe umeifia taaluma yako.