Viongozi wa CHADEMA kikaoni na IGP kwa R.P.C Iringa

Viongozi wa CHADEMA kikaoni na IGP kwa R.P.C Iringa


Kwanza kabisa ameanza kwa kusema AMESHUHUDIA KWA MACHO YAKE TUKIO HILI MWANZO HADI KIFO CHA MAREHEMU. Wakati kikao cha ndani kinaendelea ghafla zikafika defender nne za FFU akiwapo OCD. OCD baada ya kuzungumza na viongozi wa CHADEMA na kumweleza kuwa hakuna mkutano wa hadhara akakubali waendelee, FFU wakawa nje. Mara akatokea RPC na gari lake. Yeye alipofika akasema NI AMRI TAWANYIKENI. Wananchi waliokuwapo nje ya ofisi WAKAJISALIMISHA KWA KUKAA CHINI NA KUNYOOSHA MIKONO JUU. Lakini hiyo isitoshe mabomu ya machozi yakaanza kumiminika kama mvua hovyo hovyo. Waandishi wakarudi kwenye gari lao. Ndipo polisi wakamdaka mwandishi mmoja na kuanza kumpa kipigo kikali. Kuona hivyo, marehumu akashuka kwenye gari akakimbilia kwa RPC aliyekuwa garini akaanza kugonga kioo cha gari kumsihi RPC afungue kioo. RPC akafungua kidogo tu na marehemu akaanza kumsihi kuwa yule waliyemkamata si mfuasi wa CHADEMA bali ni mwandishi wa habari. RPC akamtazama marehemu kwa dharau halafu askari wengine wakamdaka.Ndipo RPC akamgeukia askari mmoja "na kumwambia BOMU". Mara moja ukasikika mlipuko wa kutisha na marehemu akadondoka hapo hapo. Maaskari wengine wakalifuata gari la huyu mr. Joseph na kuanza kuligonga gonga, akalazimika kuondoka kwa kasi sana eneo la tukio kujinusuru.
[/I]
Habari hii mliosikiliza wapo mtakuwa mmeisikia laivu kuto kwa dereva mwenyewe. Yaani bila kuumauma maneno kasema alimsikia RPC akitamka BOMU kabla ya huo mlipuko kutokea. Hebu sasa fanyeni MAGAZIJUTO!

Asante sana mkuu,to make a long story short ni kua RPC ndie alieamua Mwangosi auawawe bila hatia,ila sasa narudi kwenu Watanzania wenzangu tutalalamikia haya mambo kwenye keyboard mpaka lini wakati wao wanaendelea kutuua?
 
Mkuu Nyerere, yaani kwa kuangalia hadi RPC anakuwepo ni ishara tosha kwamba alikuja kutoa baraka kwa ufedhuli uliofanyika.
 
Nani atatoa taarifa rasmi ya kikao hicho? Itasomwa au ni mdomoni mwa askari mmoja asiye na aibu?

Nauliza kwa sababu Polisi hawawezi hata kutunga uongo kwa watu wazima.

Huyo aliyetoa taarifa tangu jana kwamba Marehemu aliwakimbilia na kitu kikatua toka huko kusikojulikana kumuuma mwandishi na kujeruhi askari, ana akili timamu? Yaani ndo mwenye akili kuliko wengine kiasi cha kuaminika kutoa taarifa kama hiyo?

Na baada ya kutoa taarifa hiyo kwa ufahamu wake, akaongeza sasa inaundwa tume ya kuchunguza jinsi alivyouawawa! hiyo ikiwa ni baada ya yeye mwenyewe kuelezea alivyouwawa!!

Kama Mwema hakujifunza mauwaji ya Morogoro, atajifunza wapi? Eti huyu Mwema ndo tuliambiwa alitkuwa afisa Interpol, Jamani!

Tunahitaji watu wafike the Hague.
 
mwema hana jipya kwani amefanya jeshi la polisi kwa mara ya kwanza kuanza kuwasaidia c.c.m hata kwa kumwaga damu
 
Panapotokea tatizo linalohusu mtu kuuawa na dola na mtu mwenyewe hakuwa na silaha; we need to speak about that matter as watu wenye utu. Not just talking blah blah! Tuondoe uCCM na uCHADEMA jamani. Tatizo hapa ni polisi kuua na kujichunguza wenyewe..
 
Asante sana mkuu,to make a long story short ni kua RPC ndie alieamua Mwangosi auawawe bila hatia,ila sasa narudi kwenu Watanzania wenzangu tutalalamikia haya mambo kwenye keyboard mpaka lini wakati wao wanaendelea kutuua?

Quotes-A-Day-copy-Break-The-Silence.jpg
 
CHADEMA wanaongozwa na Dkt. Slaa upande wa Jeshi la Polisi wanaongozwa na IGP Said Mwema, almost 4 agendas on table, polisi wameomba kufanyike roundtable meeting for now...tume yao haijaanza kufanya kazi yet.

Makene, Onyo kwa Chadema na Dr Slaa: Polisi hawaaminiki hata kidogo kwa maazimio mtakayofikia, chukueni tahadhari kubwa. Mfano mzuri ni kukubaliana kusitisha mikutano ya Iringa kwa siku tano lakini baada ya hapo Polisi wamewageuka na kusitisha kwa siku saba zaidi. Be Careful CDM, don't trust Police at all!
 
Ndio maana Lowassa anawaambia Elimu kwanza, mmekomalia kilimo kwanza. Mkuu, Shule kwanza,kujua kubofya kibodi na shule ni vitu viwili tufauti....

POMPO

this is a fact on the ground

thank you for this useful post
 
Una jeshi la polisi lililojaa wasema uongo! Ndio maana hawawezi kushinda kesi mahakamani.
 
Anaokoa maisha yake kutoka kwa nani? Mwandishi wa habari ambae anakwenda kwenye sehemu iliyovunjika amani ni lazima ajuwe mbinu za kujisalimisha, tuseme ukweli. Hakuna duniani anaejisalimisha yanakotokea mashambulizi na akaenda kumkumbatia kiongozi wa mashambulizi. Inabidi mjifunze namna ya kujisalimisha kwa askari yanapotokea machafuko. Njia rahisi ni kunyanyua kitambaa cheupe huku umejilaza chini, kama hauna kitambaa hata shati lako kama huwezi unalala kifudifudi. Hata siku moja usijaribu kukimbilia wanakotokea askari wanaoshambulia, wanajuwa umesha panic na uko tayari kwa lolote na umejioa Mhanga.

Huo ndio ukweli. Fikiri! tusipelekee jazba kupelekea kuwacha kufikiri ukweli na kilichomfikisha marehemu kwenye umauti wake. Tuwe makini.

kila kitu kinaonyesha kuwa mwandishi alikua amekwenda kuwa confront askari.
Hapo ndo nashangaa,alikua pale kuripoti matukio au alikua pale kama mwanaharakati wa chadema.
Wakati hadi viongozi wa chadema waliokuwepo hapo wakijiweka mbali,yeye akawafuata askari.
Kwa hali iliyokuwepo hapo kitendo chake kingeweza kutafsiriwa na askari kama hostile move na inawezekana askari walihisi threatened,katika nyakati hizi za watu kujivika mabomu ya kiunoni anything can happen.
 
mi sijaelewa kwanini mwandishi wa habari ateswe vile? kama mwandishi kapigwa vile hivi mtu wa kawaida itakuaje?
 
Asante sana mkuu,to make a long story short ni kua RPC ndie alieamua Mwangosi auawawe bila hatia,ila sasa narudi kwenu Watanzania wenzangu tutalalamikia haya mambo kwenye keyboard mpaka lini wakati wao wanaendelea kutuua?
mkii imesemwa kuwa GURUDUMU LINALOTEREMKA KWA KASI TOKA JUU HUKU LIKIVUNJAVUNJA MIGUU YA WATU,DAWA SI KUGANGA MAJERAHA BALI NI KUWEKA KIGINGI KWANZAILI LISIMAME.ndugu zangu bila kuweka kigingi bado tutaendelea kuumizwa na dudu hili
 
CHADEMA wanaongozwa na Dkt. Slaa upande wa Jeshi la Polisi wanaongozwa na IGP Said Mwema, almost 4 agendas on table, polisi wameomba kufanyike roundtable meeting for now...tume yao haijaanza kufanya kazi yet.

I do seriously have a problem with this. Is it about easing CHADEMA's tour of rallies or resolving the ghastly murder of a journalist in the recent event or both? Whatever the case, I do not subscribe to the idea of the Police dons just assuming some form of dignity as to hold a roundtable with their opponents short of, first and foremost, cleansing themselves of the evil (cold blooded murder) they just committed so callously and carelessly. If CHADEMA has decided to become party to this charade for the sake of political expediency, then some of us have, certainly, lost them. Whatever the case, man's dignity takes precedence above all else. You just do not murder a human being like a rat!
 
Tangu utawala wa Mahita kulikuwa na uharamia ila huu wa sasa ni too much! Ipo siku hata wakiwa wazee watapelekwa the hague
 
Swali langu kwa Makene na Dk. Slaa ni sababu zipi zimewafanya wakubali kukaa meza moja na muuwaji Rpc Kamuhanda? Tuelewe nini sisi wananchi? Mambo ya marehemu yanatusumbua sana lakini kauli ya CDM inavyochelewa kutoka huku polisi wakizidi kukamata watu wasio na hatia ni hatari zaidi kwa CDM. Chadema tokeni hadharani mlaani ubambikizaji huu wa wasafiri waendao Mbeya, la sivyo itaaminika ninyi ndo wenye vurugu.
 
Kaka njoo tuition ya Kiingereza Buguruni Rozana. Hapa chini nimeweka tafsiri isiyo rasmi kwa wasio-waswahili ili angalau wajue ulichokusudia kuandika.

So what? If somebody is dead, will their meeting help to bring him back?
How much are they paid per head (for a meeting of their own creation anyway)?


Uache kuvamia lugha za watu na hicho Kiingereza chako cha Sekondari na Vyuo vya Kata.

nshomile unanuchekesha...teh teh teh! umeona jamaa zako wanavyovunja mayai...ila wanavunja mayai bila kufuata taratibu....mpaka yanaumiza masikio
 
matatizo ya ushemeji hayo! Akitoka nje anampigia shemeji yake, 'shem wamekubali, tulia tu tutawapangia zengwe jingine'
 
Mkuu nina feeling kwamba wengi humu jamii farums hamkusikiliza WAPO radio 98.0 FM. Kila siku saa moja na dakika 20 wana kipindi cha matukio asubuhi na jioni muda huo huo. I am not trying to sell them, ila wanajitahidi sana kutafuta wahusika halisi wa matukio. Hapa natoa kile nilichokisikia kutoka kwa DEREVA ALIYEKODIWA NA WAANDISHI WA HABARI kuwapeleka kwenye eneo la tukio (ndimo alimokuwamo marehemu). Dereva huyo amejitambulisha kama John Joseph.

Kwanza kabisa ameanza kwa kusema AMESHUHUDIA KWA MACHO YAKE TUKIO HILI MWANZO HADI KIFO CHA MAREHEMU. Wakati kikao cha ndani kinaendelea ghafla zikafika defender nne za FFU akiwapo OCD. OCD baada ya kuzungumza na viongozi wa CHADEMA na kumweleza kuwa hakuna mkutano wa hadhara akakubali waendelee, FFU wakawa nje. Mara akatokea RPC na gari lake. Yeye alipofika akasema NI AMRI TAWANYIKENI. Wananchi waliokuwapo nje ya ofisi WAKAJISALIMISHA KWA KUKAA CHINI NA KUNYOOSHA MIKONO JUU. Lakini hiyo isitoshe mabomu ya machozi yakaanza kumiminika kama mvua hovyo hovyo. Waandishi wakarudi kwenye gari lao. Ndipo polisi wakamdaka mwandishi mmoja na kuanza kumpa kipigo kikali. Kuona hivyo, marehumu akashuka kwenye gari akakimbilia kwa RPC aliyekuwa garini akaanza kugonga kioo cha gari kumsihi RPC afungue kioo. RPC akafungua kidogo tu na marehemu akaanza kumsihi kuwa yule waliyemkamata si mfuasi wa CHADEMA bali ni mwandishi wa habari. RPC akamtazama marehemu kwa dharau halafu askari wengine wakamdaka.Ndipo RPC akamgeukia askari mmoja "na kumwambia BOMU". Mara moja ukasikika mlipuko wa kutisha na marehemu akadondoka hapo hapo. Maaskari wengine wakalifuata gari la huyu mr. Joseph na kuanza kuligonga gonga, akalazimika kuondoka kwa kasi sana eneo la tukio kujinusuru.


Habari hii mliosikiliza wapo mtakuwa mmeisikia laivu kuto kwa dereva mwenyewe. Yaani bila kuumauma maneno kasema alimsikia RPC akitamka BOMU kabla ya huo mlipuko kutokea. Hebu sasa fanyeni MAGAZIJUTO!

Asante mkuu...Inatisha kuona hata maaskari wa juu mpaka ukamanda ni vilaza wa kupindukia. Unategemea nini ukimtwanga mtu kwa mlipuko karibu kabisa na alipo? tatizo la uaskari huu wa kufuata amri za kipuuzi puuzi hata wenye akili nao wanakuwa wajinga kupindukia. kwani nchi huwa inaaribikaje? Hizo kelele za CDM au kuua watu wasio na hatia?
 
Back
Top Bottom