Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 3,651
- 11,548
Leo ni siku ya tatu na ya mwisho ya mkutano wa mataifa yanayounda G7; ambao umewakilishwa na maraisi wa USA, U.K, France, Germany, Italy, Japan na Canada na mawaziri wa fedha kutoka nchi hizo.
Ajenda kuu ilikuwa China.
Maeneo ambayo yamejadiliwa kuhusu China:

1. CHINA INAHATARISHA VIWANDA NA MAKAMPUNI YA NCHI ZAO
Mataifa hayo yameilalamikia China kuwa imekuwa ikifanya industrial overcapacity, hivyo soko la dunia limefurika bidhaa za China hasa kwenye sekta ya green technology kama magari ya umeme, green tech kama solar panels na wind turbines na uzalishaji wa chuma.
Bidhaa hizo zimekuwa zikiuzwa kwa bei nafuu sana kuliko bidhaa za aina hiyohiyo za nchi za Magharibi hivyo inahatarisha viwanda vyao kwani vinashindwa kushindana na bidhaa za China kwenye soko la mataifa yao na la dunia.
Nchi hizo zimesema kuwa hawataacha kushirikiana kibiashara na China wakitambua kuwa ni nchi muhimu duniani kwenye global supply chain.
Ila wataendelea kuchukua hatua ili kulinda biashara, wafanyakazi na viwanda vyao dhidi ya bidhaa za China zenye ubora ambazo zinauzwa kwa bei rahisi.

2. KITENDO CHA CHINA KUDHIBITI MADINI MUHIMU
China imekuwa ikidhibiti uuzaji nje (exportation) madini ya gallium, germnium na graphite ambayo ni muhimu sana kwenye viwanda vinavyotengeneza vifaa vya umeme na mawasiliano kama smartphone (LED), chips, electronic circuits, transistors, solar cells na kwenye magari ya umeme.
Nchi hizo zimeishutumu China kwa kufanya hivyo kwani inasababisha uhaba wa madini hayo kwa mataifa mengine yanayotengeneza bidhaa zinazoyatumia madini hayo kama malighafi.

3. KUISAIDIA RUSSIA KATIKA VITA VYA UKRAINE
Nchi za G7 zinaituhumu Beijing kuwa imekuwa ikiisaidia jeshi la Urusi.
Washington imeishutumu Beijing kwa kusaidia Urusi kupitia uzalishaji wa pamoja wa drones na usafirishaji wa zana za mashine zinazohitajika kwenye utengenezaji wa makombora ya ballastic missiles na silaha zingine.

4. UBABE WA CHINA KATIKA SOUTH CHINA SEA NA ASIA-PACIFIC
Nchi za G7 zimesema vitendo vya China kama kuizunguka Taiwan na kufanya mazoezi ya kijeshi vinaweza kupelekea vita na mgogoro mkubwa sana.
Pia vitendo vya China kujenga visiwa bandia katika bahari ya Kusini ya China, militarization, migogoro ya kimipaka na kujitanua katika eneo la Asia-Pacific na vitisho dhidi ya Ufilipino.
Nchi zote (G7) zimekubaliana kwamba zitafikisha ujumbe huo kwa uwazi katika ngazi ya juu kabisa kwa taifa la China.
Je, ni nani anayeipa G7 mamlaka ya kuamuru lililo sawa au lisilo sahihi?