Viongozi wa G7 wailaumu China kwenye mkutano wao unaofanyika Italy

China kakopa sana kujenga china, anadaiwa sana kuliko mnavyodhani. Na viwanda vingi China siyo mali ya china, mahusiano aliyo sign WTO ndiyo yalifanya aonekane hivyo alivyo leo, sasa anataka kujitia uchizi, na atakuwa chizi kweli.
Anadaiwa na nani ?
 
Labda huelewi, viwanda vilivyoko china vingi ni vya kutoka nchi zilizoendelea siyo mali ya CHINA. Waliposema hata viwanda vyao ataviua ni kwa misimamo yake China siyo kwamba anatechnologia au viwanda vingi hapana, wanaongelea akiendelea ku behave hivyo, mahusiano yakifa maana yake watalazimika kuondoa makampuni na viwanda vyao CHINA. Usidhani China ni taifa imara sana , madeni aliyo nayo migogora ikianza hayalipiki, labda kama anataka kujilipua asilipe madeni, lakini ataumia sana.
Mgawanyo wa viwanda China upoje kati ya wachina na watu wa nje ? njoo na data
 
Na viwanda vingi China siyo mali ya china, mahusiano aliyo sign WTO ndiyo yalifanya aonekane hivyo alivyo leo
Tutajie viwanda vya China ambavyo sio mali yao?

Unaweza kututajia kazi za WTO na kwa nini China alijunga WTO?
 
Labda huelewi, viwanda vilivyoko china vingi ni vya kutoka nchi zilizoendelea siyo mali ya CHINA. Waliposema hata viwanda vyao ataviua ni kwa misimamo yake China siyo kwamba anatechnologia au viwanda vingi hapana, wanaongelea akiendelea ku behave hivyo, mahusiano yakifa maana yake watalazimika kuondoa makampuni na viwanda vyao CHINA. Usidhani China ni taifa imara sana , madeni aliyo nayo migogora ikianza hayalipiki, labda kama anataka kujilipua asilipe madeni, lakini ataumia sana.
Stori za vijiweni
 
Leo ni siku ya tatu na ya mwisho ya mkutano wa mataifa yanayounda G7; ambao umewakilishwa na maraisi wa USA, U.K, France, Germany, Italy, Japan na Canada na mawaziri wa fedha kutoka nchi hizo.

Ajenda kuu ilikuwa China.

Maeneo ambayo yamejadiliwa kuhusu China:

1. CHINA INAHATARISHA VIWANDA NA MAKAMPUNI YA NCHI ZAO
Mataifa hayo yameilalamikia China kuwa imekuwa ikifanya industrial overcapacity, hivyo soko la dunia limefurika bidhaa za China hasa kwenye sekta ya green technology kama magari ya umeme, green tech kama solar panels na wind turbines na uzalishaji wa chuma.

Bidhaa hizo zimekuwa zikiuzwa kwa bei nafuu sana kuliko bidhaa za aina hiyohiyo za nchi za Magharibi hivyo inahatarisha viwanda vyao kwani vinashindwa kushindana na bidhaa za China kwenye soko la mataifa yao na la dunia.

Nchi hizo zimesema kuwa hawataacha kushirikiana kibiashara na China wakitambua kuwa ni nchi muhimu duniani kwenye global supply chain.

Ila wataendelea kuchukua hatua ili kulinda biashara, wafanyakazi na viwanda vyao dhidi ya bidhaa za China zenye ubora ambazo zinauzwa kwa bei rahisi.

2. KITENDO CHA CHINA KUDHIBITI MADINI MUHIMU
China imekuwa ikidhibiti uuzaji nje (exportation) madini ya gallium, germnium na graphite ambayo ni muhimu sana kwenye viwanda vinavyotengeneza vifaa vya umeme na mawasiliano kama smartphone (LED), chips, electronic circuits, transistors, solar cells na kwenye magari ya umeme.

Nchi hizo zimeishutumu China kwa kufanya hivyo kwani inasababisha uhaba wa madini hayo kwa mataifa mengine yanayotengeneza bidhaa zinazoyatumia madini hayo kama malighafi.

3. KUISAIDIA RUSSIA KATIKA VITA VYA UKRAINE
Nchi za G7 zinaituhumu Beijing kuwa imekuwa ikiisaidia jeshi la Urusi.

Washington imeishutumu Beijing kwa kusaidia Urusi kupitia uzalishaji wa pamoja wa drones na usafirishaji wa zana za mashine zinazohitajika kwenye utengenezaji wa makombora ya ballastic missiles na silaha zingine.

4. UBABE WA CHINA KATIKA SOUTH CHINA SEA NA ASIA-PACIFIC
Nchi za G7 zimesema vitendo vya China kama kuizunguka Taiwan na kufanya mazoezi ya kijeshi vinaweza kupelekea vita na mgogoro mkubwa sana.

Pia vitendo vya China kujenga visiwa bandia katika bahari ya Kusini ya China, militarization, migogoro ya kimipaka na kujitanua katika eneo la Asia-Pacific na vitisho dhidi ya Ufilipino.

Nchi zote (G7) zimekubaliana kwamba zitafikisha ujumbe huo kwa uwazi katika ngazi ya juu kabisa kwa taifa la China.

Je, ni nani anayeipa G7 mamlaka ya kuamuru lililo sawa au lisilo sahihi?
Yan katika haya yote naona kabisa Putin ameamua kuiangamiza USA na washirika wake ....Kwanzia ishu ya Mkataba wa mafuta wa USA na Saudi Arabia, ishu ya kusupport overthrow za serikali za nchi kama BurkinaFaso n.k, kupartner na China yan ...ishu ya capitalism ipo katika danger zone na Putin is the master mind of all these ...sad enough huyu mwisho wake hauwezi kua wa kishamba kama kina Gaddafi ..he is winning slowly his mission.
 
Walitakiwa wajifunze kwa nini China inafaulu kutengeneza bidhaa za high tech kwa gharama ndogo tofauti na wao
Hakuna cha kijifunza, China bado ni nchi inayoendelea hivyo wafanyakazi wanalipwa ujira mdogo kuganga njaa, China pia vyama vya wafanyakazi havina nguvu. Marekani, Ulaya na Japan ziko kwenye saturation point linapokuja suala la viwanda vya bidhaa. Huduma kama IT, filamu, muziki mpira, utalii, matibabu, elimu n.k kwa sasa hivi ndio zinalipa zaidi kwao.
 
China bado ni nchi inayoendelea hivyo wafanyakazi wanalipwa ujira mdogo kuganga njaa
Unaijua vizuri concept ya Purchasing Power Parity (PPP). Kaisome vizuri hiyo halafu tuje tuzungumze.

Ndio ujiulize kwa nini China imeipita USA kwenye GDP in PPP?

Kati ya Ulaya, Marekani na China ni wapi pana high cost of living?

Unaweza kusema Mchina analipwa mshahara mdogo ukilinganisha na Marekani au Ulaya lakini Mchina huyohuyo anapata mahitaji yaleyale sawa na anayelipwa mshahara standard pale Marekani au Ulaya

Hawa ndio Wachina waganga njaa:

Waganga njaa ndio top international tourism spenders
Screenshot_20240616-152119_Chrome.jpg

Unapozungumzia global luxury market waganga njaa wamezidi hata mataifa ya Ulaya na wanaenda kuizidi Marekani na kuwa top kufikia 2025
Coresight-bites-Global-Luxury-Market-768x771.jpg
 
Hakuna cha kijifunza, China bado ni nchi inayoendelea hivyo wafanyakazi wanalipwa ujira mdogo kuganga njaa, China pia vyama vya wafanyakazi havina nguvu. Marekani, Ulaya na Japan ziko kwenye saturation point linapokuja suala la viwanda vya bidhaa. Huduma kama IT, filamu, muziki mpira, utalii, matibabu, elimu n.k kwa sasa hivi ndio zinalipa zaidi kwao.
Haa wee kwaiyo tuachae hata kulima wote tuingie bongo muvi.
 
Huduma kama IT, filamu, muziki mpira, utalii, matibabu, elimu n.k kwa sasa hivi ndio zinalipa zaidi kwao.
Kwenye filamu unajua total box office ya China?

Kwenye IT ukizungumzia nchi zinazofanya vizuri duniani utaitoa China kweli?

Kwenye utalii, unapozungumzia foreign tourists visiting each year unajua China ni ya ngapi kwenye top 5 ya most visited countries?
 
Tafuta mwenyewe nadhani utazipata kwasababu unaelewa kila kitu kuhusu China na globafinance , and economy.
Kwa nini usitusaidie kutafuta mkuu? Wewe umeleta hoja yako ingependeza uitetee basi ili wote tuone kama unachosema ni cha kweli

Kama umeshindwa basi habari yako ni uongo kama uongo mwingine
 
Leo ni siku ya tatu na ya mwisho ya mkutano wa mataifa yanayounda G7; ambao umewakilishwa na maraisi wa USA, U.K, France, Germany, Italy, Japan na Canada na mawaziri wa fedha kutoka nchi hizo.

Ajenda kuu ilikuwa China.

Maeneo ambayo yamejadiliwa kuhusu China:

1. CHINA INAHATARISHA VIWANDA NA MAKAMPUNI YA NCHI ZAO
Mataifa hayo yameilalamikia China kuwa imekuwa ikifanya industrial overcapacity, hivyo soko la dunia limefurika bidhaa za China hasa kwenye sekta ya green technology kama magari ya umeme, green tech kama solar panels na wind turbines na uzalishaji wa chuma.

Bidhaa hizo zimekuwa zikiuzwa kwa bei nafuu sana kuliko bidhaa za aina hiyohiyo za nchi za Magharibi hivyo inahatarisha viwanda vyao kwani vinashindwa kushindana na bidhaa za China kwenye soko la mataifa yao na la dunia.

Nchi hizo zimesema kuwa hawataacha kushirikiana kibiashara na China wakitambua kuwa ni nchi muhimu duniani kwenye global supply chain.

Ila wataendelea kuchukua hatua ili kulinda biashara, wafanyakazi na viwanda vyao dhidi ya bidhaa za China zenye ubora ambazo zinauzwa kwa bei rahisi.

2. KITENDO CHA CHINA KUDHIBITI MADINI MUHIMU
China imekuwa ikidhibiti uuzaji nje (exportation) madini ya gallium, germnium na graphite ambayo ni muhimu sana kwenye viwanda vinavyotengeneza vifaa vya umeme na mawasiliano kama smartphone (LED), chips, electronic circuits, transistors, solar cells na kwenye magari ya umeme.

Nchi hizo zimeishutumu China kwa kufanya hivyo kwani inasababisha uhaba wa madini hayo kwa mataifa mengine yanayotengeneza bidhaa zinazoyatumia madini hayo kama malighafi.

3. KUISAIDIA RUSSIA KATIKA VITA VYA UKRAINE
Nchi za G7 zinaituhumu Beijing kuwa imekuwa ikiisaidia jeshi la Urusi.

Washington imeishutumu Beijing kwa kusaidia Urusi kupitia uzalishaji wa pamoja wa drones na usafirishaji wa zana za mashine zinazohitajika kwenye utengenezaji wa makombora ya ballastic missiles na silaha zingine.

4. UBABE WA CHINA KATIKA SOUTH CHINA SEA NA ASIA-PACIFIC
Nchi za G7 zimesema vitendo vya China kama kuizunguka Taiwan na kufanya mazoezi ya kijeshi vinaweza kupelekea vita na mgogoro mkubwa sana.

Pia vitendo vya China kujenga visiwa bandia katika bahari ya Kusini ya China, militarization, migogoro ya kimipaka na kujitanua katika eneo la Asia-Pacific na vitisho dhidi ya Ufilipino.

Nchi zote (G7) zimekubaliana kwamba zitafikisha ujumbe huo kwa uwazi katika ngazi ya juu kabisa kwa taifa la China.

Je, ni nani anayeipa G7 mamlaka ya kuamuru lililo sawa au lisilo sahihi?
Kenya itawapatia!
 
Umepata madeni ya China sasa au haidaiwi?
Taifa linapokuwa na deni la nje na linazidi GDP ujue hapo kuwa kiuchumi wanasema is very risk

Iko hivi China wana deni dogo sana la nje ukilinganisha na Marekani deni la nje la China ni 2.5 USD Trillion, Marekani ni 34 USD Trillion

Kwa hiyo China's government debt only accounts for 13.7% of GDP, which is very healthy

USA external debt to GDP ni 123% hii ni unhealthy kwa uchumi wa nchi
 
Hahaha tafuta taarifa zaidi za madeni ya china, utaelewa tu acha kurukaruka.
 
Back
Top Bottom