Viongozi wa G7 wailaumu China kwenye mkutano wao unaofanyika Italy

Wamesahau kwamba wao ndio walipigia chapuo soko huria?

Wao ndio waasisi wa free market wache nguvu ya soko ndio iamue bei,
Umesema vyema wachumi wao ndio waliotufundisha kuwa market force ya demand and supply inaamua bei ya bidhaa sokoni

Wao pia walianzisha WTO ili kuhakikisha global trade inakuwa na fairness

Je, Marekani kuweka tariffs hadi 100% kwa bidhaa za China kama EVs ni sawa?
 

Haijalishi ubabe wa marekani kuweka base zake duniani lakini CHINA kwenda kuziambia nchi ambazo nazo zina hiyo bahari kuwa hii bahari yote ni yangu ni uwendawazimu
 
Haijalishi ubabe wa marekani kuweka base zake duniani lakini CHINA kwenda kuziambia nchi ambazo nazo zina hiyo bahari kuwa hii bahari yote ni yangu ni uwendawazimu
Hakuna mahali China imewanyang'anya mataifa ya Asia-Pacific mipaka yao

China inalinda mipaka yake tu

Ni baadhi ya nchi kama Ufilipino zimekuwa zikitumika kama US vassal states ili kuitishia China

Marekani hataki China iwe na ushawishi kwenye hilo eneo ni kama anataka kuwagombanisha na China

Hili suala limekaa ki-geopolitic
 
Hivi vikao vyao vilishakuwa vikao vya harusi, wao kila wakikuta ni China Urusi tu
 
Katika viongozi wote wa G7 waliohudhuria huo mkutano, sioni ambaye tutamwona tena akiwa raisi wa nchi kwenye mataifa yao wote wanakalia kuti kavu hawana dalili za kushinda ucjshuzi ujao na kuhudhuroa mkutano mwingine tena wa G7 zaidi ya huyo mwanamama wa Italia
 
Sina hakika kama China kajipa miliki ya SCS yote mgogoro wa SCS unahusisha mistari ya kimipaka hapa ndio mgogoro ulipo.

Nakukumbusha madai ya China Beijing na madai ya China Taiwan katika miliki za mistari ya kimipaka yana shabihiana sana tu tena China Taiwan ana madai mazito ni vile tu sio powerful kama China Beijing wenda hata baadhi ya madai yake hayana mashiko sana katika vyombo vya habari.

Hata madai ya kimipaka ya kiardhi China Taiwan ana madai makubwa sana ni vile yupo weak tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…