Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Msimu uliopita tumekwazika sana, pengine katika maisha yetu ya soka hasa kwa vijana wa kizazi hiki wasioijua simba msimu uliopita tulipoteana sana, sisi ndio tumewafanya Yanga waonekane wako juu kutokana na kuhujumiana, kusalitiana, migogoro ya wenyewe kwa wenyewe nk.
Hata hivyo mambo yote hayo tumesahau kabisa kabisa, tumekubali yaishe na kuanza upya kuiunga mkono timu yetu.Hii ni timu yetu tunayoipenda katika mioyo yetu, hatupati chochote zaidi ya furaha tu.
Wenzetu wako vizuri dimbani lakini uwanjani hawaendi, wanashinda kila mechi, wanacheza soka zuri, wana migogoro lakini haina athari sana kama sisi lakini huwezi kuamini hawataki kwenda uwanjani kuiangalia timu yao.
Sisi pamoja na matatizo yetu wenyewe lakini leo tumefanikiwa kuujaza uwanja.Wao kesho ndio wanaanza mishe mishe kule Mbagala, kwa vyovyote vile mpango na mkakati wao utakuwa kuruhusu watu waingie bure.
Bw.Manara aliyekuwa anajisifu kujaza uwanja ameshindwa kufanya kazi hiyo, utajazaje uwanja kwa kwenda Wasafi fm, sio kila mtu anasikiliza redio, nenda field kawahamasishe mashabiki kama anavyofanya Mashiine ya Kuongea Ahmed Ally.
Hivyo basi nawaomba sana viongozi wangu wa Simba, tuongeze umoja na nguvu ili turudishe heshima yetu.
Shukrani na pongezi sana Ahmed Ally kwa hamasa na kufanikiwa kujaza uwanja.Kweli wewe ni jeshi la mtu mmoja.
Sasa tunahitaji furaha jamani.Msisalitiane, sisi washabiki tumeweka silaha chini na kuwaunga mkono.