Viongozi wote duniani wana cha kujifunza kwa rais wa Ukraine Volodomir Zelenskyy, ukiwa kiongozi wa nchi usikubali kuwa mnyonge mbele ya kiongozi wa nchi nyingine hata kama imewazidi kila kitu, leo amemkabili Trump kikatili sana na kumuonesha maana ya ukinidharau nakukabili kama mbwai mbwai
Zelenskyy kamkabili Trump na makamu wake kiulalo ulalo bila hofu wala unyonge. Majibizano kati yao nmekuekea link hapo chini kwenye comments, ni aibu, Ikulu ya Marekani italazimika kutoa tamko kujisafisha. Kilichotokea jioni hii ni aibu na fedheha kubwa ya kidiplomasia kwa taifa hilo kubwa na lenye nguvu ulimwenguni
Trump na makamu wake walijaribu kumsiginya kibabe na kumshambulia kwa maneno makali ya kumshushia hadhi na kujaribu kumtupia lawama ila Zelenskyy amewashikisha adabu, amejibu kwa usahihi na kuwarudishia mashambulizi yao mpaka mkutano ukaharibika
Kiufupi viongozi hususan wa mataifa masikini wanapaswa kumuiga Zelenskyy, ukienda kwenye mataifa tajiri ukawa dhaifu unaburutwa ila ukisimama imara unaheshimika na kamwe taifa lako halitachukuliwa kama shamba la bibi
Hata wakombozi wa nchi zetu kama Mwalimu Julius Kambarage Nyerere walisimama imara mno dhidi ya mabeberu, haikuwa rais ila huo ndio uongozi uliotukuka unaoacha alama na uzalendo mkuu kwa taifa