Viongozi wa Uamsho wapo huru?

Status
Not open for further replies.
Wasirudie tena ule ujinga!

Ole wao tuanze kusikia mapadiri wanauawa tena
Hukumu ya anayeua ni kunyongwa siyo kuwekwa jela miaka 9 na kuachiwa
Hakuna ushahidi wa kuwahukumu hao masheikh kwa makosa yoyote, walibambikiziwa kesi tu kwa sababu walikuwa wanapinga ukoloni wa Tanganyika dhidi ya Zanzibar
 
Jamaa wameteseka sana.

Walipwe fidia sio wanaachiwa tu kibwege.

Sure niliwaonea huruma sana hawa jamaa.

Kama wameschiwa ni jambo jema. Wamtafute Ponda, hajawahi kuwaacha wala kuwasahau.

Waendeleze mapambano yao ya kutaka Zanzibar ijitenge na Tanganyika.
 
Walipwe fidia, watumishi wote waliosababisha kuwabambika kesi inatakiwa wawajibe wakatwe stahiki zao pesa zipatikanazo walipwe mashehe.
 
Siku zote tunasema kama ushahidi haujakamilika watu wasiwekwe ndani ni against humanity,ni matumizi mabaya ya Kodi zetu,only in afrika
 
Mwenye maelekezo ya kidhalimu kutokea juu yuko busy na malaika.

Hapa sasa mdogo mdogo mwendo wa haki bin haki.
Haki uinua taifa.Nchi ni masikini kwa sababu ya laana za kuwaonea watu, unamuweka ndani binadamu mwenzio miaka 8 bila ushahidi ushamuharibia future yake kizembe tu
 
Uzuri wake aliyewaweka ndani no muislam mwenzao hii inaondoa dhana potofu kwenye jamii ambayo ingeweza kuvunja umoja wetu.
 
Haki uinua taifa.Nchi ni masikini kwa sababu ya laana za kuwaonea watu, unamuweka ndani binadamu mwenzio miaka 8 bila ushahidi ushamuharibia future yake kizembe tu

Kuna mi mbumbumbu ambayo piga ua yanaona ni sawa kwa vile tu, hii kwao leo haiwahusu. Ubinafsi wa namna gani huo?
 
Gerezani miaka zaidi ya minane bila kesi kusikilizwa!!??
 
Uzuri wake aliyewaweka ndani no muislam mwenzao hii inaondoa dhana potofu kwenye jamii ambayo ingeweza kuvunja umoja wetu.

Sina hakika ukristo, ubaniyani, upagani, uislam, nk unakuja vipi katika hili.

Nakazia: haki huinua taifa. Dhana hii tulikuwa tumeikosa kwa muda mrefu.
 
Sina hakika ukristo, ubaniyani, upagani, uislam, nk unakuja vipi katika hili.

Nakazia: haki huinua taifa. Dhana hii tulikuwa tumeikosa kwa muda mrefu.
Unajua mazingira yaliyopelekea Hawa masheikh kuwekwa kizuizini yalikuwa tatanishi sana pia tuhuma zao zimekuwa kama za uonevu .

Kwa mazingira hayo, lawama huwa haziepukiki, lakini inapokuja kuonekana at least aliyewaweka ndani alikuwa wa dini moja basi dhana potofu inaondokq kwamba wameonewa au dini fulani inawaonea watu wa dini nyingine.

Hivyo basi sitarajii lawama zihame .
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…