Viongozi wastaafu walishtukizwa kuongea na wameongea ukweli

Please, leta majina ya waliopotea.
 

Una hakika unachokiandika? Nimejifunza mtu akitoka madarakani anaanza kuwa na hekima.
 

Hawa wazee si ndio wameongoza enzi zote na wametengeneza haya matatizo yote? Rushwa imelifilisi Taifa hili wasifikiri tumesahau
 
Lakini akiwa Rais nyie ndio mlimuita dhaifu ushasahau
 


"Ukimwaga mboga namwaga Pombe"
 
Hasira zote zimeishia Rufiji na Kibiti. Hadi tunavyoongea sasa hivi watu wanajisaidia kwa DED na DC.

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nakumbuka Escrow,Richmond, Buzwagi,Bomba la Gesi,Vitalo vya Gesi aslia,Pesa za Gaddafi.Msitu wa Mwipande,Katiba mpya hewa.
Yawezekana JK alikuwa hahusika mmoja kwa mmoja na kashfa hizo lakini alishindwa kufuatilia wasaidizi wake.Wali take advantage ya yeye mara kwa mara kuwa safari za nje.
 

Mchakato wa Katiba mpya haukuwa hewa.
Ni Magufuli ndiye aliyezuia mchakato usiende mbele kwa kukataa kuitisha kura za maoni, kitu pekee kilichokuwa kimebaki kwenye process ili tupate katiba mpya!
 
Na kumbuka kuwa wakati wa utawala wa Mkapa, Sumaye alikuwa boss wa Kikwete na Magufuli.
Ndiye aliyekuwa mtendaji wake wa karibu kama Waziri mkuu
 
Mchakato wa Katiba mpya haukuwa hewa.
Ni Magufuli ndiye aliyezuia mchakato usiende mbele kwa kukataa kuitisha kura za maoni, kitu pekee kilichokuwa kimebaki kwenye process ili tupate katiba mpya!
Alikuwa na muda wa kutosha,ilitakiwa katiba mpya itumike kwenye uchaguzi mkuu lakini akapiga chenga huku akimwandaa kaka mdogo avae viatu vyake kwa katiba ya zamani.
Hata kama angeweza kuharisha uchaguzi hadi katiba mpya ilikuwa inawezekana.Majuto mjukuu,tunalia sote yeye na sisi.
 
Mtu wa kwanza kukumbusha malengo halisi ya 2025 alikuwa Zitto, sio kwamba watu awakufahamu target, walijisahaulisha tu kwa malengo ya kufanya siasa, na walishaiteka hoja.

From no where mtu anakurupuka na kuingilia mambo kwani wenzake anadhani awajui; au wanachofanya ni kwa makusudi ya siasa.

Mbona wao kila siku wanajaribu ku justify manunuzi ya ndege na miradi yao mingine inayopondwa na upinzani.

Siku wakinyimwa mikopo upande wa pili shangwe na wanaongezea chumvi zao kwanini wamenyimwa. Serikali wanapambana mpaka kuipata na kuwajibu.

Wewe ushakuwa mstaafu wacha wanaofanya siasa watumie matukio yanayojitokeza kwa faida zao, that is what politicians do.
 
Unashangaa nini. Hata form ya kugombea urais ilikuwa moja. This is one man show. Hakuna mwingine kilakitu ni mtu mmoja tu. Hata budget haifuatwi inatumika kwa utashi wamtu mmoja tu.
 
Hivi kwa mfano, JK akijiunga ACT halafu ateme nyongo vizuri kwenye kampeni hivi itakuwaje?
Nauliza tu.


NB: Hata Yeye si msafi.
 

Serikali ni taasisi, anapoishia mwenzako na wewe unaendeleza. Ndiyo maana aliacha madaraja kama vile ya Kigamboni na Kilombero yakijengwa yakamaliziwa Magufuli, sasa kwa nini Magufuli kagoma kumalizia katiba mpya wakati alipokea kijiti kutoka kwa mwenzie na sheria inayoguide mchakato huo wa katiba mpya ipo wazi tu?
 
Ulimboka je?

Ilijulikana kuwa alitekwa kwa sababu ya kuitisha mgomo. na kipindi hicho kulikuwa na vyombo vya habari ambavyo vilikuwa huru. Mwanahalisi walitoa majina ya mtu aliyemteka namkumbuka alikuwa anaitwa Juma Ighondu mzaliwa wa Dodoma. Siku hizi vyombo vyote huru vya habari vimefungwa. tumesahau hata bei za magazeti maana ukinunua hakuna habari zaidi ya taarifa za serikali.
 
Hakuna Sehemu yeyote ambayo kikwete amesema uongo , ni ukweli mtupu.....Lengo la Mkapa 2025 tufikie usd 300 bado sana!!

Japo alichuana na Mkapa kwenye urais lakin Mkapa alimuweka kwenye wizara ambayo unaonekana sana ,Mkapa hakunata JK hapotee kama siasa za sasa sio kupotea bali unapotezwa kabisa.
 

Marehemu hasifiwi kwa kudanganya bali kwa kueleza ukweli wa alichokifanya.

Huwezi kumsifu marehemu kuasisi mpango wa Taifa wa maendeleo wa vision 2025 halafu ukadanganya eti vision hiyo imefikiwa wakati bado!

Maendeleo ya kweli hayajengwi kwa uongouongo. JK alikuwa sahihi kumuelezea marehemu kwa muktadha huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…