Viongozi wastaafu walishtukizwa kuongea na wameongea ukweli

Acha unafiki. Ni kweli kipindi cha Kikwete hapakuwa na matatizo hayo? Tuwe wakweli, Kikwete alivurunda kwa namna yake na huyu naye anavurunda kwa namna yake. Lakini tangu enzi ya JKN hadi leo kila mmoja ana dosari zake.

Ni Kikwete aliyesema wafanyakazi waandamane wakione. Kuna watu wamepotea kimyakimya.
Please, leta majina ya waliopotea.
 
Mkwere sio mnafiki. Anaongea ukweli. Nakumbuka miaka yake walikuwa wakipingana kwa hoja bungeni baadae anawaita ikulu anasikiliza hoja za kila upande then wanamaliza. Hakukuwepo kupigana risasi, kutekana au kupotea kwa watu kwa miaka yote 10. Hongeraaa rais Kikwete.

Una hakika unachokiandika? Nimejifunza mtu akitoka madarakani anaanza kuwa na hekima.
 
Hapo ndipo ninapoichukia siasa. Mkwele kwa sababu amesema kile unachokipenda ameshakuwa mtu safi.
Mimi nakikumbuka kipindi hicho sana, wakati ambao Ridhiwani alitamba nchi nzima kama mwana wa mfalme. Kila duka jenereta iliunguruma mbele yake, yaliundwa makampuni ya kuiuzia umeme TANESCO. TANESCO ilikuwa sehemu ya kuchuma pesa watu walitajirika, walinunua malori, madawa ya kulevya yaliuzwa kama njugu, walitengeneza pesa kwa njia haramu, hospitali kubwa zote zinatibu vijana waathirika was madawa, hawa watu walikuwa peponi, leo ndio wanaosifiwa. Kama tumefika mahali tunalinganisha na haya anayofanya Magufuli na hao wengine, basi hakutatokea kiongozi atakayetufaa.
Hata Lisu akabahatika kuwa rais, naye sio malaika nina uhakika naye hatachukuwa muda atatukanwa matusi mengi. Ninachokiona ni kwamba wakosoaji wakubwa hawakosoi kwa lengo jema, Bali kutafuta zamu ya kutawala basi. Watanzania tunahitaji kuwa macho na Huyu kiumbe anayeitwa mwanadamu.

Hawa wazee si ndio wameongoza enzi zote na wametengeneza haya matatizo yote? Rushwa imelifilisi Taifa hili wasifikiri tumesahau
 
Mkwere sio mnafiki. Anaongea ukweli. Nakumbuka miaka yake walikuwa wakipingana kwa hoja bungeni baadae anawaita ikulu anasikiliza hoja za kila upande then wanamaliza. Hakukuwepo kupigana risasi, kutekana au kupotea kwa watu kwa miaka yote 10. Hongeraaa rais Kikwete.
Lakini akiwa Rais nyie ndio mlimuita dhaifu ushasahau
 
“Mkapa ndiye amefanya kazi kubwa sana kukuza uchumi baada ya kuchukua nchi kutoka kwa Rais Mwinyi ikiwa na uchumi goigoi sana. Alipambana,” -J.M.Kikwete
___________________________

"MAGUFULI Ni wa kipekee Sana, aliikuta nchi iko vibaya Sana kiuchumi yeye ndio katufikisha kwenye uchumi huu mzuri wa Kati"
Rais A.H.Mwinyi.

*Hii inaitwa ukimwaga mboga......🤣*

"Ukimwaga mboga namwaga Pombe"
 
Nilikuwa nafuatilia mazishi ya hayati BW Mkapa tangu mwanzo hadi mwisho. Niliona jinsi ambavyo rais wetu alivyo mtaka rais wa Zanzibar kuzungumza na wananchi wa Masasi na Sheina alionesha kushtuka kwa hilo kwani hakuwa amearifiwa lakini alikwenda. Pia akafuata Kikwete na baadaye Mwinyi. Wote walionesha kutofurahishwa na kitendo cha kukurupushwa kuongea bila kutaafiwa.

Anyway, kilichonifurahisha ni kitendo cha mh. Kikwete kuweka mambo sawa kuhusu ukuaji wa uchumi na mambo mengine mengi kama ninavyoyaweka hapa chini kwa kifupi:
1. Mpango wa kufikia uchumi wa kati uliasisiwa na Mkapa na lengo ni kufikia $3000 mwaka 2025 na kusema mpango huo serikali zote zimeufanyia kazi kwa hatua na sio jambo la serikali hii tu
2. Kikwete alionesha ujasiri mkubwa kwa kusema Mkapa alifanya mengi sana lakini hakuwa anapenda kusifiwa. Alitumia neno la kiingereza "populist" na kusema wazi kuwa Mkapa hakuwa populist ila wengi hawakumwelewa alimaanisha nini. Ukiwa kiongozi halafu ukawa populist ni mbaya sana na populist wanaochukiwa sana popote.
3. Kiwete aliweka wazi wazi kuwa mwaka 1995 kwenye round ya kwanza ya kura za maoni alimshinda Mkapa ila maamuzi ya chama yalimwelekea Mkapa. Na kwamba hata baada ya mchuano huo mkali Mkapa baadaye alifanya kazi kwa karibu na Kikwete na hapakuwepo na uadui. Rejea hatima ya Membe mwaka huu ndani ya CCM.
4. Kikwete aliweka wazi kuwa bado serikali hii ina kazi kubwa kufikia lengo la $3000 mwaka 2025 na kwamba sasa wamefikia $1080 tu

Kikwete alimaliza hatuba yake kwa kusema kuwa hiyo ndio gharama ya kukurupushwa kuongea. Ama kweli Kikwete aliuweka wazi ukweli bila kuogopa, sikutegemea hayo tena mahali pale.
Hasira zote zimeishia Rufiji na Kibiti. Hadi tunavyoongea sasa hivi watu wanajisaidia kwa DED na DC.

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
Hapo ndipo ninapoichukia siasa. Mkwele kwa sababu amesema kile unachokipenda ameshakuwa mtu safi.
Mimi nakikumbuka kipindi hicho sana, wakati ambao Ridhiwani alitamba nchi nzima kama mwana wa mfalme. Kila duka jenereta iliunguruma mbele yake, yaliundwa makampuni ya kuiuzia umeme TANESCO. TANESCO ilikuwa sehemu ya kuchuma pesa watu walitajirika, walinunua malori, madawa ya kulevya yaliuzwa kama njugu, walitengeneza pesa kwa njia haramu, hospitali kubwa zote zinatibu vijana waathirika was madawa, hawa watu walikuwa peponi, leo ndio wanaosifiwa. Kama tumefika mahali tunalinganisha na haya anayofanya Magufuli na hao wengine, basi hakutatokea kiongozi atakayetufaa.
Hata Lisu akabahatika kuwa rais, naye sio malaika nina uhakika naye hatachukuwa muda atatukanwa matusi mengi. Ninachokiona ni kwamba wakosoaji wakubwa hawakosoi kwa lengo jema, Bali kutafuta zamu ya kutawala basi. Watanzania tunahitaji kuwa macho na Huyu kiumbe anayeitwa mwanadamu.
Mimi nakumbuka Escrow,Richmond, Buzwagi,Bomba la Gesi,Vitalo vya Gesi aslia,Pesa za Gaddafi.Msitu wa Mwipande,Katiba mpya hewa.
Yawezekana JK alikuwa hahusika mmoja kwa mmoja na kashfa hizo lakini alishindwa kufuatilia wasaidizi wake.Wali take advantage ya yeye mara kwa mara kuwa safari za nje.
 
Mchakato wa Katiba mpya haukuwa hewa.
Ni Magufuli ndiye aliyezuia mchakato usiende mbele kwa kukataa kuitisha kura za maoni, kitu pekee kilichokuwa kimebaki kwenye process ili tupate katiba mpya!
 
Kwanza mimi nilishangaa serikali hii ilishindwa hata kumpa nafasi Rasmi kwenye ratiba aliyekuwa waziri wake Mkuu yaani Ndugu Sumaye nafasi ya kuongea machache juu ya Marehemu raisi Mkapa, naona kama ni uchoyo fulani wa baadhi ya watu kuhodhi msiba wa marehemu.

Hata wastaafu nao hawakuwekwa rasmi kwenye ratiba ili kumzungumzia mwenzao, uchoyo wa namna gani huu. Eti ni mpaka Magufuli alipojisikia ndo akawastukiza!

Nakumbuka mwaka 1999 kwenye kifo cha Mwalimu, pale uwanja wa Taifa mzee Mwinyi aliwekwa kwenye ratiba ya kumzungumzia mwalimu, mstaafu mwenzie. Lakini cha ajabu safari hii Ratiba yote ilikuwa centred juu ya Magufuli tu!
Na kumbuka kuwa wakati wa utawala wa Mkapa, Sumaye alikuwa boss wa Kikwete na Magufuli.
Ndiye aliyekuwa mtendaji wake wa karibu kama Waziri mkuu
 
Mchakato wa Katiba mpya haukuwa hewa.
Ni Magufuli ndiye aliyezuia mchakato usiende mbele kwa kukataa kuitisha kura za maoni, kitu pekee kilichokuwa kimebaki kwenye process ili tupate katiba mpya!
Alikuwa na muda wa kutosha,ilitakiwa katiba mpya itumike kwenye uchaguzi mkuu lakini akapiga chenga huku akimwandaa kaka mdogo avae viatu vyake kwa katiba ya zamani.
Hata kama angeweza kuharisha uchaguzi hadi katiba mpya ilikuwa inawezekana.Majuto mjukuu,tunalia sote yeye na sisi.
 
Mtu wa kwanza kukumbusha malengo halisi ya 2025 alikuwa Zitto, sio kwamba watu awakufahamu target, walijisahaulisha tu kwa malengo ya kufanya siasa, na walishaiteka hoja.

From no where mtu anakurupuka na kuingilia mambo kwani wenzake anadhani awajui; au wanachofanya ni kwa makusudi ya siasa.

Mbona wao kila siku wanajaribu ku justify manunuzi ya ndege na miradi yao mingine inayopondwa na upinzani.

Siku wakinyimwa mikopo upande wa pili shangwe na wanaongezea chumvi zao kwanini wamenyimwa. Serikali wanapambana mpaka kuipata na kuwajibu.

Wewe ushakuwa mstaafu wacha wanaofanya siasa watumie matukio yanayojitokeza kwa faida zao, that is what politicians do.
 
Kwanza mimi nilishangaa serikali hii ilishindwa hata kumpa nafasi Rasmi kwenye ratiba aliyekuwa waziri wake Mkuu yaani Ndugu Sumaye nafasi ya kuongea machache juu ya Marehemu raisi Mkapa, naona kama ni uchoyo fulani wa baadhi ya watu kuhodhi msiba wa marehemu.

Hata wastaafu nao hawakuwekwa rasmi kwenye ratiba ili kumzungumzia mwenzao, uchoyo wa namna gani huu. Eti ni mpaka Magufuli alipojisikia ndo akawastukiza!

Nakumbuka mwaka 1999 kwenye kifo cha Mwalimu, pale uwanja wa Taifa mzee Mwinyi aliwekwa kwenye ratiba ya kumzungumzia mwalimu, mstaafu mwenzie. Lakini cha ajabu safari hii Ratiba yote ilikuwa centred juu ya Magufuli tu!
Unashangaa nini. Hata form ya kugombea urais ilikuwa moja. This is one man show. Hakuna mwingine kilakitu ni mtu mmoja tu. Hata budget haifuatwi inatumika kwa utashi wamtu mmoja tu.
 
Hivi kwa mfano, JK akijiunga ACT halafu ateme nyongo vizuri kwenye kampeni hivi itakuwaje?
Nauliza tu.

NB: Hata Yeye si msafi.
 
Alikuwa na muda wa kutosha,ilitakiwa katiba mpya itumike kwenye uchaguzi mkuu lakini akapiga chenga huku akimwandaa kaka mdogo avae viatu vyake kwa katiba ya zamani.
Hata kama angeweza kuharisha uchaguzi hadi katiba mpya ilikuwa inawezekana.Majuto mjukuu,tunalia sote yeye na sisi.

Serikali ni taasisi, anapoishia mwenzako na wewe unaendeleza. Ndiyo maana aliacha madaraja kama vile ya Kigamboni na Kilombero yakijengwa yakamaliziwa Magufuli, sasa kwa nini Magufuli kagoma kumalizia katiba mpya wakati alipokea kijiti kutoka kwa mwenzie na sheria inayoguide mchakato huo wa katiba mpya ipo wazi tu?
 
Ulimboka je?

Ilijulikana kuwa alitekwa kwa sababu ya kuitisha mgomo. na kipindi hicho kulikuwa na vyombo vya habari ambavyo vilikuwa huru. Mwanahalisi walitoa majina ya mtu aliyemteka namkumbuka alikuwa anaitwa Juma Ighondu mzaliwa wa Dodoma. Siku hizi vyombo vyote huru vya habari vimefungwa. tumesahau hata bei za magazeti maana ukinunua hakuna habari zaidi ya taarifa za serikali.
 
Nilikuwa nafuatilia mazishi ya hayati BW Mkapa tangu mwanzo hadi mwisho. Niliona jinsi ambavyo rais wetu alivyo mtaka rais wa Zanzibar kuzungumza na wananchi wa Masasi na Sheina alionesha kushtuka kwa hilo kwani hakuwa amearifiwa lakini alikwenda. Pia akafuata Kikwete na baadaye Mwinyi. Wote walionesha kutofurahishwa na kitendo cha kukurupushwa kuongea bila kutaafiwa.

Anyway, kilichonifurahisha ni kitendo cha mh. Kikwete kuweka mambo sawa kuhusu ukuaji wa uchumi na mambo mengine mengi kama ninavyoyaweka hapa chini kwa kifupi:
1. Mpango wa kufikia uchumi wa kati uliasisiwa na Mkapa na lengo ni kufikia $3000 mwaka 2025 na kusema mpango huo serikali zote zimeufanyia kazi kwa hatua na sio jambo la serikali hii tu
2. Kikwete alionesha ujasiri mkubwa kwa kusema Mkapa alifanya mengi sana lakini hakuwa anapenda kusifiwa. Alitumia neno la kiingereza "populist" na kusema wazi kuwa Mkapa hakuwa populist ila wengi hawakumwelewa alimaanisha nini. Ukiwa kiongozi halafu ukawa populist ni mbaya sana na populist wanaochukiwa sana popote.
3. Kiwete aliweka wazi wazi kuwa mwaka 1995 kwenye round ya kwanza ya kura za maoni alimshinda Mkapa ila maamuzi ya chama yalimwelekea Mkapa. Na kwamba hata baada ya mchuano huo mkali Mkapa baadaye alifanya kazi kwa karibu na Kikwete na hapakuwepo na uadui. Rejea hatima ya Membe mwaka huu ndani ya CCM.
4. Kikwete aliweka wazi kuwa bado serikali hii ina kazi kubwa kufikia lengo la $3000 mwaka 2025 na kwamba sasa wamefikia $1080 tu

Kikwete alimaliza hatuba yake kwa kusema kuwa hiyo ndio gharama ya kukurupushwa kuongea. Ama kweli Kikwete aliuweka wazi ukweli bila kuogopa, sikutegemea hayo tena mahali pale.
Hakuna Sehemu yeyote ambayo kikwete amesema uongo , ni ukweli mtupu.....Lengo la Mkapa 2025 tufikie usd 300 bado sana!!

Japo alichuana na Mkapa kwenye urais lakin Mkapa alimuweka kwenye wizara ambayo unaonekana sana ,Mkapa hakunata JK hapotee kama siasa za sasa sio kupotea bali unapotezwa kabisa.
 
Mtu wa kwanza kukumbusha malengo halisi ya 2025 alikuwa Zitto, sio kwamba watu awakufahamu target, walijisahaulisha tu kwa malengo ya kufanya siasa, na walishaiteka hoja.

From no where mtu anakurupuka na kuingilia mambo kwani wenzake anadhani awajui; au wanachofanya ni kwa makusudi ya siasa.

Mbona wao kila siku wanajaribu ku justify manunuzi ya ndege na miradi yao mingine inayopondwa na upinzani.

Siku wakinyimwa mikopo upande wa pili shangwe na wanaongezea chumvi zao kwanini wamenyimwa. Serikali wanapambana mpaka kuipata na kuwajibu.

Wewe ushakuwa mstaafu wacha wanaofanya siasa watumie matukio yanayojitokeza kwa faida zao, that is what politicians do.

Marehemu hasifiwi kwa kudanganya bali kwa kueleza ukweli wa alichokifanya.

Huwezi kumsifu marehemu kuasisi mpango wa Taifa wa maendeleo wa vision 2025 halafu ukadanganya eti vision hiyo imefikiwa wakati bado!

Maendeleo ya kweli hayajengwi kwa uongouongo. JK alikuwa sahihi kumuelezea marehemu kwa muktadha huo
 
Back
Top Bottom