Hapo ndipo ninapoichukia siasa. Mkwele kwa sababu amesema kile unachokipenda ameshakuwa mtu safi.
Mimi nakikumbuka kipindi hicho sana, wakati ambao Ridhiwani alitamba nchi nzima kama mwana wa mfalme. Kila duka jenereta iliunguruma mbele yake, yaliundwa makampuni ya kuiuzia umeme TANESCO. TANESCO ilikuwa sehemu ya kuchuma pesa watu walitajirika, walinunua malori, madawa ya kulevya yaliuzwa kama njugu, walitengeneza pesa kwa njia haramu, hospitali kubwa zote zinatibu vijana waathirika was madawa, hawa watu walikuwa peponi, leo ndio wanaosifiwa. Kama tumefika mahali tunalinganisha na haya anayofanya Magufuli na hao wengine, basi hakutatokea kiongozi atakayetufaa.
Hata Lisu akabahatika kuwa rais, naye sio malaika nina uhakika naye hatachukuwa muda atatukanwa matusi mengi. Ninachokiona ni kwamba wakosoaji wakubwa hawakosoi kwa lengo jema, Bali kutafuta zamu ya kutawala basi. Watanzania tunahitaji kuwa macho na Huyu kiumbe anayeitwa mwanadamu.