Hii ni hatarii sanaa japo wengine sijui ni kuelewa au kwa maksudi wanafanya mzaha mzaha .labda niwambie tu binadamu ukiomba jema likukute inaweza kuchukua hata miaka mia usilipate lakini omba baya uone hata mwaka huwa hauishi jamani niwaombe ndugu zangu watanzania tuwe serous kidogo.
Sasa tuombe mungu corona ifike pote lakini isifike kariakoo litakuwa janga kubwa sanaa la kitaifa
Mosi. Biashara kubwa nchii ipo kariakoo kuanzia bidhaa zote zenye ugumu wa kupatikana zinapatikana kariakoo hata kama hutoipata basi ukifika utafanikiwa kupewa hata connection ya namna ya kuipata hata kwa masoko mengine ya njee ya nchi kwa bei nzuri sio zile bei za online . .....Kariakoooo.
Pili . Soko kubwa la ununuzi wa bidhaa kama mazao ya chakula lipo kariakoo sasa fikiria hata huku kiijijini wafanyabiashara wote wa mchele huwaza kufikisha mizigo kariakoo kwanza kabla ya tandale au mahakama ya ndizi _ manzese hivyo lazima turudi na corona huku vijijini kufuata zahanati tu ni kilomita 9, kituo cha afya 46 kms daahhhh....kariakooo
Tatu: manunuzi ya bidhaa nyingine kwa mfano nguo na viatu upatikanaji wake kwa bei nzuri na rahisi ni kariako hakuna namna lazima ufike ubanane na usigane na wafanyiabisahara wenzio madukani ili utoke na mzigo wa kueleweka na kuuzika kwa urahisi huko uendako ......karikaoooo
NNE. mwingiliano wa watu wa mataifa mbali mbali pale kariakoo ndo shida utakuta watu mmbanana pale shimoni kariakoo shimoni huyu anaongea kihindi,kisomali ,kinyarwanda .kirundi kichina halafu wote mnanunua bidha zinazofanana kwa kuzishika na kuziona a dahhhh......kariakooo
Mwisho. tuendelee kumuomba mungu atuepushe na hili janga .
Mungu bariki Tanzania.
Sent using
Jamii Forums mobile app