Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Wanaposema hausambazwi kwa hewa, huku wanadai ukiwa unapiga chafya uzibe mdomo,huwa sielewagi.
 
1584778067498.png
 
Nina jirani yangu ni msabato kanitembelea leo kwa mshangao maana siyo kawaida yake kunitembelea siku za jumamosi, nimemuuliza kulikoni leo hajaenda kanisani (make aliwahi nambia wao ibada ni jioni hadi jioni) kanijibu walienda lakini leo wamefunga saa sita na ili kuepuka mikusanyiko wameamua wasirudi ibada ya jioni.

nikamuuliza kati ya asubuhi na jioni ni ibada ipi inakua na watu wengi? akajibu asubuhi nikamuuliza kama ni corona kwa nini wasifunge tu kanisa mpaka corona idhibitiwe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni hatarii sanaa japo wengine sijui ni kuelewa au kwa maksudi wanafanya mzaha mzaha .labda niwambie tu binadamu ukiomba jema likukute inaweza kuchukua hata miaka mia usilipate lakini omba baya uone hata mwaka huwa hauishi jamani niwaombe ndugu zangu watanzania tuwe serous kidogo.

Sasa tuombe mungu corona ifike pote lakini isifike kariakoo litakuwa janga kubwa sanaa la kitaifa

Mosi. Biashara kubwa nchii ipo kariakoo kuanzia bidhaa zote zenye ugumu wa kupatikana zinapatikana kariakoo hata kama hutoipata basi ukifika utafanikiwa kupewa hata connection ya namna ya kuipata hata kwa masoko mengine ya njee ya nchi kwa bei nzuri sio zile bei za online . .....Kariakoooo.

Pili . Soko kubwa la ununuzi wa bidhaa kama mazao ya chakula lipo kariakoo sasa fikiria hata huku kiijijini wafanyabiashara wote wa mchele huwaza kufikisha mizigo kariakoo kwanza kabla ya tandale au mahakama ya ndizi _ manzese hivyo lazima turudi na corona huku vijijini kufuata zahanati tu ni kilomita 9, kituo cha afya 46 kms daahhhh....kariakooo

Tatu: manunuzi ya bidhaa nyingine kwa mfano nguo na viatu upatikanaji wake kwa bei nzuri na rahisi ni kariako hakuna namna lazima ufike ubanane na usigane na wafanyiabisahara wenzio madukani ili utoke na mzigo wa kueleweka na kuuzika kwa urahisi huko uendako ......karikaoooo

NNE. mwingiliano wa watu wa mataifa mbali mbali pale kariakoo ndo shida utakuta watu mmbanana pale shimoni kariakoo shimoni huyu anaongea kihindi,kisomali ,kinyarwanda .kirundi kichina halafu wote mnanunua bidha zinazofanana kwa kuzishika na kuziona a dahhhh......kariakooo

Mwisho. tuendelee kumuomba mungu atuepushe na hili janga .

Mungu bariki Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali imepiga marufuku mikusanyiko. Ina maana hapo Kariakoo bado watu wanafanya biashara tu kwa wingi wao?
 
Corona ikifika Kariakoo halafu ikakutana na wale TRA wanaoomba rushwa kwa yule jamaa wa Kiha sujui itakuwaje?!
 
Watanzania wenzangu. Tumieni maarifa. Ujinga utatumaliza.

Epuka mikusanyiko yote. Kwa hivi sasa ugonjwa unasambaa. Siyo kwamba ni tatizo dogo. Tatizo ni kubwa mno na vurusi vipo nchini ila kwa sasa tunaambukizana. Patakuwa hapatoshi.

Tuache ujinga. Epuka mikusanyiko hata ya kwenye ibada. Kule Italy hata pope ameagiza tusali majumbani kwetu na maungamo tujifanyie wenyewe. Huyo ndo kiongozi wa kanisa na hapo alipo ndipo alipozikwa Paulo na Petro. Sikiliza wataalam, siyo Rais Magufuli.
 
Moja ya suluhisho la corona ni kukaa majumbani na kuepuka kabisa kundi kubwa la watu hasa kwenye masoko, sehemu za burudani, harusi nk.

Naishauri Serikali sasa ihakikishe kuwa maeneo yote katika nchi hii umeme haukatiki ili kutuwezesha kukaa majumbani bila bughudha vinginevyo kama hatuna umeme majumbani itabidi kuzurura tu.
 
Back
Top Bottom