Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Asante kwa hoja hizi.Paulo alilalamikiwa na kuhofiwa Kama muuaji lakini Mwenyezi Mungu hakuangalia mapungufu yake aliendelea kumtumia na kubadili jina kutoka Sauli na kuwa Paulo,Leo hii hekima yake na mafundisho yake ndio sehemu ya Biblia takatifu.
Nabii Musa alijiona muuaji na mwenye mapungufu mengi lakini Mwenyezi Mungu akasema wewe ndio ntakutumia kuwatoa watu wangu kutoka utumwani Misiri.
Unataka kujua kuhusu Mtumishi wa Mungu DAUDI,mapungufu yake yalikuwa hayapimiki kibinadamu,pamoja na kumtanguliza Askari wake mstari wa mbele katika Vita ili auwawe na kweli akauwawa na yeye akamchukua mke wa Askari wake,bado Mwenyezi Mungu hakuondoa kusudi lake juu ya DAUDI.
Isaya : Mlango 1
18 Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
P