Vita iliyoanzishwa na Marekani dhidi ya Iran yaleta changamoto kubwa kwa Afrika

Vita iliyoanzishwa na Marekani dhidi ya Iran yaleta changamoto kubwa kwa Afrika

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
199
Reaction score
322
VCG111625190600.jpg
Marekani na Israeli zimeanzisha vita dhidi ya Iran zikipuuza sheria za kimataifa. Ingawa bara la Afrika liko mbali na uwanja wa vita katika Ghuba ya Uajemi, lakini kutokana na utandawazi wa uchumi duniani, umbali si dhamana ya usalama. Bara la Afrika lina wasiwasi mkubwa: ingawa halitahusika moja kwa moja katika mapambano ya kijeshi, msingi wake wa kiuchumi na hata usalama wa kijamii vinaweza kuathiriwa na vita hiyo.

Athari ya moja kwa moja na kubwa zaidi iliyoletwa na vita hiyo kwa Afrika ni soko la nishati. Mlango bahari wa Hormuz ni njia muhimu ambayo zaidi ya asilimia 20 ya mafuta na gesi zinasafirishwa kupitia mlango huo, ikimaanisha kwamba, tukio lolote lililotokea huko litaleta athari kwa bei za nishati duniani. Kwa nchi nyingi za Afrika zinazoagiza mafuta na gesi kutoka Mashariki ya Kati, vita hiyo inamaanisha ongezeko kubwa la bei ya nishati, na huenda italeta mfumuko wa bei. Hali ambayo si kama tu itaathiri maisha ya watu, bali pia inaweza kuleta matatizo kwa uchumi wa nchi hizo.

Kuhusu mnyororo wa kiviwanda, kabla ya hapo, mgogoro kati ya Israel na Kundi la Houthi katika eneo la Bahari Nyekundu tayari umeathiri minyororo ya usambazaji wa kimataifa. Mzozo wa Marekani na Iran utazidisha ugumu wa usafirishaji baharini, na kuongeza gharama za kusafirisha bidhaa baharini kwa nchi za Afrika. Jambo baya zaidi ni kwamba kupanda kwa gharama za mizigo na mafuta hatimaye kutasababisha upungufu wa chakula, na kuleta changamoto zaidi kwa nchi za Afrika.

Kwa upande wa mambo ya kifedha, vita kati ya Marekani na Iran pia itasababisha upungufu wa dola za Kimarekani katika nchi za Afrika. Hivi sasa kiwango cha ubadilisha wa dola za Kimarekani kimeanza kuongezeka tangu kutokea kwa vita hiyo. Hali hii itaongeza ugumu wa nchi za Afrika kulipa madeni ya nje. Hivi sasa, zaidi ya nchi 20 za Afrika tayari ziko katika hatari ya kushindwa kulipa madeni, kwani madeni yao ya karibu dola bilioni 90 za Kimarekani yanahitaji kulipwa ndani ya miaka miwili ijayo.

Ikikabiliwa na changamoto zinazoletwa na vita iliyoanzishwa na Marekani dhidi ya Iran, ni wazi Afrika haiwezi kubaki mbali. Nchi za bara hilo zinapaswa kuratibu misimamo yao, na kutafuta ushirikiano wa kikanda na kimataifa ili kushinda changamoto hizo.
 
Sisi ni Mideko, na tukiona changamoto huko nje tunakuwa proud kujitokeza na kuziongelea ila muda wa kujitokeza na kuongelea kinaga ubaga mikakati mikubwa ya maendeleo walipo tulipokuwa, tulipo na wapi tunaenda hilo hakuna.

We angalia corona ilivyopewa kipao mbele na hata sasa bado inalazimishwa itrend ila inabuma, angalia wakat Ukraine inaanza vita vna Urusi.

Hii inanikumbusha kijijini zilipokuwa zinanyesha mvua za mawe na baadae njaa ikaja kutokea hapo mbele wale wavivu wote husingizia kwamba walilima ila mvua za mawe ziliharibu mazao yao.
 
Afrika kuna sehemu nyingi twachimbA mafuta na gesi...ifike pahala tuanze kujitegemea mwanzo ni mgumu lakini matunda yake ni ya vizazi vingi...
AFRIKA TUACHE MAMBO YA KISENGYE
TUUNGANE
 
Afrika kuna sehemu nyingi twachimbA mafuta na gesi...ifike pahala tuanze kujitegemea mwanzo ni mgumu lakini matunda yake ni ya vizazi vingi...
AFRIKA TUACHE MAMBO YA KISENGYE
TUUNGANE

Kuungana ni mojawapo ya ushirika wa kikanda ambao muanzisha uzi ameshauri. Sasa swali ni kwamba 'je watawala wana maono hayo?!'
 
Kuungana ni mojawapo ya ushirika wa kikanda ambao muanzisha uzi ameshauri. Sasa swali ni kwamba 'je watawala wana maono hayo?!'
Kabisa
Baadhi wapo tayari
Baadhi bado wana ubinafsi na choyo,,,,lakini waafrika (wananchi) wapo tayari,,hawana neno kabisa kabisa
 
Back
Top Bottom