Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?

Mimi sikwenda frontline; nilikuwa Communications Makao Makuu ya Brigade ya Magharibi (wakati huo) kama sehemu ya askari wa akiba tuliokuwa mobilized kwa ajili ya vita; ina fact mobilization ilianza kabla hata Nyerere hajatoa ile hotuba yake ya "uwezo tunao"

Baada ya vikosi vyetu kufika pale na kuteka ile kambi ya Mbarara, mapigano direct ya Lukaya yaliendelea usiku na mchana kwa kama siku tatu hivi; ila hiyo ndiyo yaliyoua watu wengi sana huenda kuliko mapigano mengine yoyote katika vita ile. Tatizo kubwa la mapigano ya Lukaya ilikuwa ni kwa vile walipigania kwenye matope 24 hours.

Failure ya waganda ni kuwa jeshi letu liliwaelemea kwa kila kitu; watu wanaweza kuja na sababu mbalimbali lakini jeshi letu lilikuwa imara sana kuliko wao. Tuliwabana mbavu sana

Askari kupigwa ambush na kuuwawa vitani ni jambo la kawaida kabisa; ningeomba lisitiliwe mkazo sana kama failure ya huyo Kanali Nshimanyi ingawa sina kumbukumbu zake.
 
Sijajua maswali haya unamuuliza nani nikijua itapendeza zaidi!!!
 
Kuna sehemu humu JF Historia yangu ya vita vya Kagera nilielezea kwa kirefu kuhusu KIPIGO CHA LUKAYA ikumbukwa pale Lukaya ilikuwa ni AMBUSH kwa maana pale tuliweka mtego wa kuvizia na kwa bahati nzuri waliingia mkenge na kupata kipigo cha mbwa koko!!Na si kweli kuwa mapigano ya hapo Lukaya yaliendelea usiku na mchana kwa siku tatu hiyo ilikuwa AMBUSH tu kwa lugha rahisi yalikuwa mapigano ya kushitukiza!!!.
 

Yaani jirani yako akija nyumbani kwako na kumbaka mke wako mbele yako utasema hakuna haja ya kumpigania mke wako? Nachukulia kama wewe ni mtoto wa kiume. Iwapo vita ile haikuwa na ulazima, basi hatuna haja ya kuwa na JWTZ tena
 
Mkuu pia niliwahi kusikia kwamba Ghadaffi alipeleka wanajeshi wake na vifaa vya kivita Uganda zikiwemo ndege za kivita baada ya Amin kuelemewa na kumuomba msaada. Hao pia walipata kipigo kitakatifu na wengi kutekwa lakini Mwalimu akawaachia huru na kuwarudisha kwao baada ya vita kuisha.

 
In fact walibya wengi sana waliuwawa na wengine walitekwa; Nyerere akaamuru wale mateka warudishwe kwao libya salama. Ghadaffi akatoa saluti kwa Nyerere.
 
Kichuguu Unaweza kuwa unakumbuka kosa jingine la kutaka kupeleka battalion msitari wa mbele bila tahadhari. Aliyetaka kufanya hivyo ni commander mmoja aliyeitwa Mlay. Nyerere alikuja kumkemea sana na kumwambia Mlay unataka kuua watu?
 
Si kweli kuwa Tanzania was caught unprepared for war nchi yetu ilikuwa imejiandaa vya kutosha ndiyo maana kuanzia 1977 na 1978 vijana wengi sana walichukuliwa na kuajiriwa kwenye kambi mbalimbali za Jeshi waliokuwepo enzi hizo wanaweza kukiri hilo.Kuhusiana na Msumbiji kutuma vikosi vyake kuja kusaidia katika vita vya kagera hiyo si kweli lakini kwa Mwandishi wa habari hiyo alikuwa yuko sahihi kwa juujuu tu.Ukweli ni kuwa sisi kama Tanzania tulikuwa na wanajeshi wetu huko Msumbiji walikuwepo huko kusaidia Ukombozi wa msumbiji na baada ya kupata uhuru waliendelea kubaki huko kusaidia Jeshi la FLELIMO kujenga nchi yao baada ya kutokea vita vya kagera ilibidi wanajeshi wetu warudi kusaidiana na wenzao ambao tuliokuwa nyumbani na ni kweli tulikuwa tunawahitaji sana hasa kuutumia uzoefu wao katika medani ya vita.Na mimi binafsi katika kikosi changu nilikuwa nao wanajeshi waliotoka msumbiji tulipigana nao bega kwa bega mpaka mwisho.Kwa hiyo kwa mtu wa nje anaweza kusema tulipata msaada kutoka msumbiji lakini kiukweli wale walikuwa wanajeshi wetu ambao walienda kusaidia mapambano ya Ukombozi wa msumbiji.Na huo ndiyo ukweli!!!
 
Kichuguu Unaweza kuwa unakumbuka kosa jingine la kutaka kupeleka battalion msitari wa mbele bila tahadhari. Aliyetaka kufanya hivyo ni commander mmoja aliyeitwa Mlay. Nyerere alikuja kumkemea sana na kumwambia Mlay unataka kuua watu?
Kabla vita haijaaza baada kuvamiwa, amri zilitoka kwa Yusuf Himid aliyekuwa brigade commander wetu (Magharibi); kwa hiyo inawezekan yule kanali alikuwa anatekeleza amri halali ya brigedia simkumbuki tena. Kumbukumbu zangu za makanali wengi ni ndogo sana sasa hivi labda kwa sababu walikuwa wengi, ninajua zaidi matendo ya Mabrigadier na mameja General na makanali wachache waliongara tu, kama Ben Msuya kwani ndiye aliyeiteka Kampala na akang'ara sana; Lupogo na Kitete- yes huyu ndiye aliyekuwa chief tactician kabla hajapanda kuwa brigadier na kuongoza brigade mojawapo kwenye frontline; huko nyuma niliandika Lupogo lakini tactician alikuwa Kitete.
 
Sasa kama binam yako alipigana mbona yeye hakufa kama hao wengine,tatizo alikufunga kamba umuone na yeye mwamba kumbe alikuwa anashinda camp akipanga panga silaha hakuna hata siku moja ameenda kwenye uwanja wa vita kujua kinachoendelea.

Unasemaje wamekufa watu wengi serikali ikaficha hali ya kuwa wote tunajua vita haina macho yeyote na idadi yoyote wanaweza kufa kwanini ifichwe?
 
Mkuu unaamini wakati wa vita ya Kagera tulikuwa na viongozi wachawi? Makanali, brigadiers, major generals, etc.,?
 
Unaweza kuta alikuwa mfagizi hata zilipokuwa silaha haruhusiwi hata kusogelea.
 
Mkuu unaamini wakati wa vita ya Kagera tulikuwa na viongozi wachawi? Makanali, brigadiers, major generals, etc.,?
hapana; kuna stori nyingi za kupikwa mitaani. Kuna watu waliwahi kusema Brigadier Mayunga alikuwa ana uchawi fulani kwamba alikuwa anaweza kuingia kwenye vikosi vya maadui bila kuonekana, lakini hizo zote ni conspiracy theories tu. Siyo kweli
 
hapana; kuna stori nyingi za kupikwa mitaani. Kuna watu waliwahi kusema Brigadier Mayunga alikuwa ana uchawi fulani kwamba alikuwa anaweza kuingia kwenye vikosi vya maadui bila kuonekana, lakini hizo zote ni conspiracy theories tu. Siyo kweli
Lakini Mayunga hakuwa na mambo yanayotia shaka wakati wa vita? Yaani yasiyokuwa ya kawaida?
 
Mkuu Kichuguu shukrani kwa kumbukumbu nzuri post #12 na #14,watoto wadogo wanajazwa ujinga na story za kuunga unga kutoka kwa watu ambao hata hawajui bunduki inashikwaje.

Mimi ni kizazi baada ya hii vita early 80s but siwezi kukaa kubishana eti “walikufa watu wengi sana” nani asiyejuwa vita ni kifo?huyo mzazi mwenyewe anamruhusu mwanae kwenda jeshini kichwani akijua muda wowote ataletewa badge yake kwamba mwanao kumbukumbu yake hii hapa kuwaje tukatae watu kufa,je hao Uganda ndo walipoteza watu wachache sana?vita tulishinda hatukushinda hiyo ndo habari ila kwamba watu walikufa wangapi siyo habari waliifia nchi na wanaenziwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…