Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Mimi sikwenda frontline; nilikuwa Communications Makao Makuu ya Brigade ya Magharibi (wakati huo) kama sehemu ya askari wa akiba tuliokuwa mobilized kwa ajili ya vita; ina fact mobilization ilianza kabla hata Nyerere hajatoa ile hotuba yake ya "uwezo tunao"Kiongozi kuna sehem umeongelea "Bato ya Lukaya"
Kuna sehem inaitwa "umulwekubyo" (Kona)
Hii "bato" wanasema ndo ilimaliza vita...
1. Mapambano ya Lukaya yaliendeleaa kwa muda gani....?
2. Inasemekan hapa Amin alipoteza Askari wengi hadi kufika 300 au 400 wakiwemo walibya zaidi ya 100 na wengne kutekwa
Katika mazingira ya vita nyie mnajickiaje kuona askari zaidi ya 300 wamelala..?
3. Kama ulishiriki hii "bato" unaweza tueleza nn ilkuwa "failure" ya waganda hapa kiasi cha kupotea wengi kiasi ikii....?
4. Vita uwa ina mengi je ni kweli uko frontline kuna makafara na matambiko yalikuwepo msitunii....??
5. Kuna mahali nilisoma kuwa Kamanda Nshimanyi alkula "ambush" ambayo ilimcost askari 25~35, nn ilkuwa tatzo...??
6. Ulikuwa chini ya Kamanda yupi na katika platoon ako au battalion ako...? Unakumbk "great loss" kwen ilkuwa kupoteza askari wangap katika pambano moja
Asantee
Sent using Jamii Forums mobile app
Baada ya vikosi vyetu kufika pale na kuteka ile kambi ya Mbarara, mapigano direct ya Lukaya yaliendelea usiku na mchana kwa kama siku tatu hivi; ila hiyo ndiyo yaliyoua watu wengi sana huenda kuliko mapigano mengine yoyote katika vita ile. Tatizo kubwa la mapigano ya Lukaya ilikuwa ni kwa vile walipigania kwenye matope 24 hours.
Failure ya waganda ni kuwa jeshi letu liliwaelemea kwa kila kitu; watu wanaweza kuja na sababu mbalimbali lakini jeshi letu lilikuwa imara sana kuliko wao. Tuliwabana mbavu sana
Askari kupigwa ambush na kuuwawa vitani ni jambo la kawaida kabisa; ningeomba lisitiliwe mkazo sana kama failure ya huyo Kanali Nshimanyi ingawa sina kumbukumbu zake.