Kweli wewe Ni mzushi unafikiri raisi ni kama vyicheo vyenu vya pale ufipa kutengua na kuteua Ni uamuzi wake atakapo ona msaidizi yupi atenguliwe yupi ateuliwe kumbe kwako ni big ishu ungedili Kwanza na matatizo ya Sacco's yenu ingekuwa Bora zaidi SUMU HAIONJWI KWA MDOMO
Watanzania wanaangamia kwa Corona wewe unahamasisha habari za CDM?Msiwatoe watu kwenye reli,tuambie tuanze lini Partial/Total Lockdown kama nchi?
Mliidharau Corona na kuifananisha na Malaria,ajali,Ebola na mapambio kuwa ni ka.Corona sasa mnajificha?Mnasisitiza maombi,nani kawaambia Virusi vinadhibitiwa kwa ibada?Hizi ibada tungeendelea kuzifanyia majumbani maana haikosi kina walioambukizwa katika siku tatu za maombi.
Mikusanyiko ingekuwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya tu.Wengine wote wangeenda majumbani kipindi tunafunga shule na vyuo,Bunge lisingekutana na hats mahabusu wanaodhaminika wangeachiliwa.
Ila kwa sababu za kizembe,Watanzania bado wanatengenezewa mazingira ya mikusanyiko kwa visingizio hafifu kama uchumi kuyumba,mtakufa njaa nk.
Corona inavyosambaa kwa kasi hii,tutajengaje huo uchumi?Twendeni lockdown, tupime Corona kwa watu wote,tuongeze motisha na risk allowances na special insurance policy kwa watakaopata corona kazini kwa watumishi wa afya,askari magereza,uhamiaji na polisi nk.
Corona siyo kacorana tujipange kikamilifu,tushikamane Watanzania wote na Nahodha wetu arudi kuongoza mapambano.