Vita ya Corona: Nahodha wetu katelekeza chombo Baharini, tutaponaje?

Vita ya Corona: Nahodha wetu katelekeza chombo Baharini, tutaponaje?

Upepo wa Pesa,
Wenyewe wanasema yupo likizo,kiongozi/kamanda mzuri hawezi kutenda hayo wakati wa vita.Tuna watawala wa ajabu sana huku wakitaka tuwaite Wazalendo.

Kama hawa ni Wazalendo kweli,ni bora Uzalendo ukanipitia mbali.
 
Ni uzembe mkubwa umefanyika katika jambo hili viongozi mkubali mkatae

Laiti kama Dar es salaam ingewekwa lockdown kipindi wagonjwa ndo wamefika watano hali isingekuwa mbaya kama ilivyo sasa

Ubishi, uzembe, na ukaidi wenu utasababisha vifo vya watu wengi na damu yao itakuwa juu yenu milele

Eeh! Mungu tusaidie twakuomba sana sisi ni waja wako!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Neno uzalendo limevuma saa nyakati hizi.
Nadhani hata Ile tafsiri halisi imebadilika na kuwa mtu anayeramba miguu ya wakubwa au kukubali kila wasemacho/wafanyacho.

Sasa corona imetinga. Ni kama nchi ipo vitani. Wale Wazalendo na hasa yule mkubwa wao kapotea jumla.

Nahodha katelekeza jahazi.

Huu ndiyo wakati wa kumwona nahodha akiwa na majeshi yake akiongoza kizalendo.

Sawa kawaachia wasaidizi wanahangaika kivyao. Wakifanikiwa, atachukua credit. Likibuma, atawalaumu kwa uzembe.
 
Yule bwana wa the one man show anaetaka apate credits zote hayuko kwenye dancing floor.
 
Gellangi, Sio Tanzania tu dunia nzima Ina hangaika na corona shida yako total lockdown? Unaufahamu sana kuliko wataalam wa afya? Ulaya American walifunga mipaka na lockdown juu sijui walikosea maana vifo havikukwepeka nchi Sasa watu wamegoma hawataki lockdown na uwezo wa kupata huduma zote muhimu wanazo hata asie kuwa na uwezo amewezeshwa Rudi huko ulipo.

Wewe ni Nani mwenye uwezo wa kukaa mwezi au zaidi ndani na familia yake bila kufanya kazi na akaweza kutimiza mahitaji yote ndani ya muda huo labda asilimia 20 tu ya watanzania na ndio maana hakuna alie jiajiri alie funga kazi yake au alie ajiriwa alieacha kazi yake jiulize kwanini?

Hakuna anae taka kufa kwa njaa ndio maana watu wanafanya kazi mimi binafsi siwezi kuacha kazi yangu nikakaa ndani Nani atanipa huduma za family yangu kwa asie na kazi lockdown kwake Ni muhimu maana ameshazoea kukaa nyumbani ukiona lockdown muhimu kwako jiweke wewe na familia yako hakuna atakae kuja kukutoa nyumbani kwako ukafanye kazi
 
Lakini hapa kila siku maagizo yanatolewa kua kama huna sababu ya kutoka usitoke bak nyumbani na kama unajua madhara ya hii ni bora ubaki kuliko kusubili kuambiwa hakuna mtu atake kuja lukwambia baki ndani ni wew na familia kuchukua hatua mapema na kufuata maagizo yanayotolewa na wataalamu wa afya hilo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa naandika kwa majonzi kwa kusikia jinsi Watanzania wenzetu wanavyougua Corona na wengine kupoteza maisha.Poleni nyote.

Kinachoumiza zaidi ni namna baadhi yetu tunavyoteteana hata kunapokuwa na uzembe kwenye hatua zinazochukuliwa kutulinda na Corona.

Kuna wanaosema Nahodha wetu ni shujaa,mwenye uthubutu na tupo salama ilhali abiria tunaona hatari iliyopo mbele yetu.

Nahodha wetu tunaambiwa yupo mapumzikoni,je tukisema kajitosa baharini na kutuachia chombo kielee kwenda kuzama tunakosea?

Corona bila lockdown itatumaliza, ilikuwa Arusha, Dar na Zanzibar hatukuona haja ya lockdown eti tutakufa njaa. Sasa tuna wagonjwa mikoani na hakuna kinachoonekana kufanyika, hatujaamua bado kulock maeneo yenye wagonjwa.

Tunafahamu kuwa hakuna dawa, chanjo, vifaa tiba, maabara za uchunguzi na vifaa vya kujikinga hasa kwa watoa huduma za afya.

Tuamini kuwa tupo salama?Tuamini kuwa Nahodha hajajitosa na kuacha chombo katikati ya mawimbi makali?
Si kweli kwamba hakuna kinachofanyika labda wewe huoni wala husiki kwa hiyo huna habari na kinachofanyika kuhusu Corona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuliyemwamini tarehe 25/10/2015 kuwa atatuvusha kakimbilia mafichoni, hata salamu za rambirambi zinatumwa kwa EMS. Sijawahi ona kiraja wa kaya akienda likizo kaya ikiwa imeingia vitani. Huyu hatufai kabisa!
 
Hewa ilichaguliwa 25/10/2015 na imethibitika uhewa wake sasa. Kumbe zile push up zilikuwa za kujiandaa kukimbia matatizo ya wapiga kura.
 
Leo nilibahatika kupanda daladala jirani yangu alikuwa anakula, nikamwambia kwa ugonjwa huu wa corona siyo vizuri kula kwenye daladala 'tulikuwa kwenye kiti cha nyuma cha coaster' akasema sawa lakini bado aliendelea kula bagia zake hapa tunajifunza kwamba watu wengi hawana elimu ama nikuishi kwa mazoea
Makosa yalitokea pindi tulipoufuta unyapara... lakini ifike wakati tukemeane vilivyo na elimu itolewe ipasavyo maana hata suala la kunawa ni kama bado halijaeleweka vema
 
Nakwenda CHATO kupitia bandiko hili,siendi CHATO kutazama mji ulivyokuzwa haraka kwa vitu wala siendi chato kutazama uwanja wa kisasa wa ndege.

Nakwenda chato kumuona amiri jeshi mkuu yes ndiye mh JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Amiri Jeshi Mkuu tunajua uko likizo hilio ni jambo jema hasa kwa kazi kubwa ulionayo ya kuliongoza Taifa hili lenye matatizo lukuki

Mh Amiri jeshi mkuu wakati unakwenda likizo dunia ilianzwa kutikiswa na ugonjwa uitwao corrona Tanzania tulikuwa amepatikana mmoja tu Arusha bado haikuwa tishio japo usambaaji wake kwa nchi zilizoendelea ulionesha kuanza kwa taratibu mwishowe unachanganya kwa haraka

Mh Rais kuna nchi zilidharau huuu ugonjwa Leo zimegeuka vilioo tupu na sisi tulikuwa na cha kujifunza sitaki kulaumu huu sio muda wa kulaumiana ni muda wa kuziba makosa yetu wenyewe.

Ulipokwenda likizo mh Rais mgonjwa alikuwa mmoja hata ww ukiwa kanisani ulituambia ni kagonjwa kadogo hata mwanao makonda alituaminisha pia japo juzi kasarenda mwenyewe
Hivi Leo jumla ya visa 254 vimeripotiwa na 10 washafariki kupitia huu ugonjwa

Najua dhamira yako njema ya ujenzi wa miradi mikubwa ambayo imekupelekea ukashindwakuzuia ndege na kufungwa mipaka najua kwa mujibu wa katiba yetu ww ni chief comforter yaani mfariji mkuu na hili Taifa liendelee lazima afya za watu wake ziwe imara ndio uchumi utapanda.

Mh Rais waziri wa afya chini ya waziri mkuu amefanya kazi kubwa sana madaktari wauguzi wako kazini usiku na mchana Hilo halina shida tuwaombee kwa mungu waendelee na wito
Mh Rais ujumbe wangu kwa kwako katiza likizo njoo kwenye uwanja wa vita adui ameshajitanua sasa rudi DSM ama DODOMA njoo uongoze vitaa hii najua praise team watakwambia usijali Dada yangu ummy mwalimu yupo.

Nikwambie mh Rais kutukuwepo kwako kumepelekea mkuu wa mkoa Dar es saalam akiongea wanadhani umemuachia jahazi mara zote amekosea amegeuza gonjwa hili kuwa siasa rejea alipotoa Siri ya mgonjwa mtoto wa mh freeman mbowe kuwa kapatwa corrona rejea kauli zake za kuudharau maambukizi haya Leo anatuambia watu wa DSm tujadiliane jee tunataka kufa na corrona ama la kwa kauli yake ashakata tamaa.

Mh Rais rudi uzibe gape kati ya waziri wako na ww njoo uwafariji wananchi wako wameumia na wanazidi kuumia na hili gonjwa. Baba mh Rais ugonjwa huu sio aibu kwa serikali yako rudi upiganie afya za wananchi wako sitaki kutaja marais wanaopigana vita wakiwa ofisini nitakuwa sikutendei haki kama ulivyootuomba tufanye maombi tumefanya ni muda wakuja kuongeza nguvu ktk kuukabili ugonjwa huu

Mh Rais hakuna vita nyepesi hakika ww kama jemedari mkuu tunakutegemea sana njooo ufute zile kauli zako za “haka kagonjwa ni kadogo”

Wako dizzo mtawala
0f7d54a9-a7e5-4359-88ab-65b01d354a9d.jpg




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom