Vita ya Corona: Nahodha wetu katelekeza chombo Baharini, tutaponaje?

Acha dhihaka kwa kiongozi wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Nimecheka had nimekaa chini.dah🤣🤣🤣...
 
JF Igolya!

Nawakumbusha tu Viongozi wetu, vifo na majanga havijawahi kutorokwa. Na tunapokuwa tunaweka msukumo katika kuwahaudumia watu ndiyo tunakuwa tunapunguza uwezekano wa hivo vifo na majanga. Usalama wa Viongozi unaanzia kwa Wananchi wao. Kwa kuwa Viongozi kazi yao ni kuhakikisha Ustawi wa watu wao.

Hivyo, watu wao wakidumaa na wao wapo katika hatari ya kudumaa. Maana haiwezekani hata siku moja, mtu mmoja au wawili ndo wakaji-isolate wakafikiri wako safe na wanaji-isolate bila kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya wengine. Roho zetu sote ni za nyama, na isifikie sehemu ikaonekana kwamba Kuna baadhi ya watu ndo wenye roho ya thamani, na wengine roho zao hazina thamani.

Kama ni kuchapa kazi kwa kuchukua tahadhari, basi wote tuchape kazi tukiwa field. Siyo wengine wanachapia kazi home, wengine wanachapia field.

Mfano, leo Mtumishi mmoja wa Wizara Elimu kakata kamba Dom, nyumba yake imefungwa utepe mwekundu. Sijui kilichomuua, na si kila kifo ni Corona, lakini hadi saivi ofisini ni taharuki.

Tusijijali wenyewe!

Kuna wengine walisema Wachina wataendelea kuja lakini hadi saivi nafikiri wako misitu ya Njombe wamejificha. Maana Viongozi naona hali ikiwa mbaya wanakimbia kwao. Wewe ambaye huna namna unaenda ofisini kuchapa kazi, kutii maelekezo ya waheshimiwa, sawa tutachapa kazi.

Lakini ukweli ni kwamba janga haliogopi kwao na mtu. Ipo siku inakuja kwetu sisi sote, mkiwemo ninyi tutatolewa kwenye jokofu kama bia. Tutageuzwa bila kujua tunageuzwa na Mwisho wa siku mchanga utatuhusu. Jeuri yote itakuwa imekoma.

Tuliwapa dhamana kwa upendo, turejesheeni upendo na siyo dharau na kiburi. Hata mnapozungumza, zungumzeni kwa staha, tumaini na kutia moyo. Lakini Maneno yenu kamwe hayana chembe ya kutia moyo na matumaini. Hayaleti faraja!

Duuuh. Siyo pouwa mjue!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli atakuwa rais wa kwanza Duniani kuingia kwenye kumbukumbu za guness book of records kwa kuwatelekeza watu wake na kujificha kijijini kwake wakati wa janga hili la corona. Hakika sidhani kuna rais yoyote dunini anaweza kufanya anachokifanya Magufuli.

Zaidi hapo akatoa hotuba ya hovyo kabisa kuweza kutolewa na kiongozi wa nchi from his private home in chato. Anaongoza nchi kutokea kiijini kwake. kweli.

Magufuli anapata wapi uthubutu huu wa kufanya anyofanya? Wanachi na viongozi mbali mbali akiwemo Kiongozi wa upinzani Mh. Mbowe,Mb Mh. Sugu. wanapaza saitu kwa magu achukue hatua dhidi ya corona na atoke chato, lakini magufuli kimya...

Wanachi tuchukue hatua tujikomboe, labda Magu kazi ya Urais imemshinda lakini hawezi kusema, zaidi ya kuwaambia watu waombe Mungu.
 
Mods shughulikieni hii takataka itupeni kule dampo kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Na wewe ni mmoja wa mangosha wanaoleta mambo ya kienyeji kwenye uongozi wa taifa hili? Binafsi sidhani kama kuna mkulu wa hovyo kama huyu kuwahi kutokea Afrika nzima, ni aibu kubwa ndio maana kakimbilia kwao.
 
Tofautisha viongozi na watawala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…