JF Igolya!
Nawakumbusha tu Viongozi wetu, vifo na majanga havijawahi kutorokwa. Na tunapokuwa tunaweka msukumo katika kuwahaudumia watu ndiyo tunakuwa tunapunguza uwezekano wa hivo vifo na majanga. Usalama wa Viongozi unaanzia kwa Wananchi wao. Kwa kuwa Viongozi kazi yao ni kuhakikisha Ustawi wa watu wao.
Hivyo, watu wao wakidumaa na wao wapo katika hatari ya kudumaa. Maana haiwezekani hata siku moja, mtu mmoja au wawili ndo wakaji-isolate wakafikiri wako safe na wanaji-isolate bila kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya wengine. Roho zetu sote ni za nyama, na isifikie sehemu ikaonekana kwamba Kuna baadhi ya watu ndo wenye roho ya thamani, na wengine roho zao hazina thamani.
Kama ni kuchapa kazi kwa kuchukua tahadhari, basi wote tuchape kazi tukiwa
field. Siyo wengine wanachapia kazi
home, wengine wanachapia
field.
Mfano, leo Mtumishi mmoja wa Wizara Elimu kakata kamba Dom, nyumba yake imefungwa utepe mwekundu. Sijui kilichomuua, na si kila kifo ni Corona, lakini hadi saivi ofisini ni taharuki.
Tusijijali wenyewe!
Kuna wengine walisema Wachina wataendelea kuja lakini hadi saivi nafikiri wako misitu ya Njombe wamejificha. Maana Viongozi naona hali ikiwa mbaya wanakimbia kwao. Wewe ambaye huna namna unaenda ofisini kuchapa kazi, kutii maelekezo ya waheshimiwa, sawa tutachapa kazi.
Lakini ukweli ni kwamba janga haliogopi kwao na mtu. Ipo siku inakuja kwetu sisi sote, mkiwemo ninyi tutatolewa kwenye jokofu kama bia. Tutageuzwa bila kujua tunageuzwa na Mwisho wa siku mchanga utatuhusu. Jeuri yote itakuwa imekoma.
Tuliwapa dhamana kwa upendo, turejesheeni upendo na siyo dharau na kiburi. Hata mnapozungumza, zungumzeni kwa staha, tumaini na kutia moyo. Lakini Maneno yenu kamwe hayana chembe ya kutia moyo na matumaini. Hayaleti faraja!
Duuuh. Siyo pouwa mjue!
Sent using
Jamii Forums mobile app