Vita ya Corona: Nahodha wetu katelekeza chombo Baharini, tutaponaje?

Vita ya Corona: Nahodha wetu katelekeza chombo Baharini, tutaponaje?

Kocha mkuu kakimbia timu, kocha msaidizi naye kaisusa timu, Timu imebaki na keputeni na kiungo mchezeshaji, Benchi la ufundi wanalia ukata wa zana za kufanyia mazoezi, Dactari wa timu amekimbia kisa vifaa tiba kwa wachezaji, mchezaji akiumia uwanjani anatibiwa na wachezaji wenzie

Mechi imekuwa ngumu mashambulizi toka kila upande wa uwanja kulekea upande wetu je tutatoboa hii mechi?

Je kocha atalejea baada ya timu kushinda mechi au atajiuzulu moja kwa moja?
Inaitwa both team to score

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kama anaongoza kikosi kwanini anatoka hadharani kuwaita wenzake wapuuzi?Kwamba wanakosea hiki na kile as if yeye sio sehemu ya hiyo timu?Kwanini asingewasiliana nao kuwaambia fanyeni hivi na vile mpaka aje hadharani kututajia sisi madhaifu ya timu yake?Shame!
Hili la watu kuitwa wapuuzi ni mada nyingine kabisa, ifungulie uzi utapata wachangiaji na mimi nitakuwa mmojawao.
 
Kocha mkuu kakimbia timu, kocha msaidizi naye kaisusa timu, Timu imebaki na keputeni na kiungo mchezeshaji, Benchi la ufundi wanalia ukata wa zana za kufanyia mazoezi, Dactari wa timu amekimbia kisa vifaa tiba kwa wachezaji, mchezaji akiumia uwanjani anatibiwa na wachezaji wenzie

Mechi imekuwa ngumu mashambulizi toka kila upande wa uwanja kulekea upande wetu je tutatoboa hii mechi?

Je kocha atalejea baada ya timu kushinda mechi au atajiuzulu moja kwa moja?
Naona nafsi yako inafurahii maana ulikuwa unaomba huu ugonjwa uje. Umekuja sasa furahii maana "timu imebaki na keputeni"
 
Hakuna kitu kama hicho, collective responsibility ndio inayoliongoza baraza la mawaziri likiongozwa na rais.
Hujaona alivyorusha shutuma juzi?As if yeye sio sehemu ya hao aliowapa majukumu waongoze mapambano!PM,Makonda na Spika walionekana wanapuliziwa dawa kwenye mashine alizotoa Rostam!JPM anakuja kusema huo ni upumbavu kwani wanaua viroboto tu!Kweli hapo kuna collective responsibility?
 
Mkuu hukumuelewa mkuu, kabla ya kupinga kitu jaribu kuelewa kwa undani nini kinaongelewa.

Rais hakuongelea vitu alivyotoa Rostam, hajaongelea zile machine maalum ambazo zinatumiwa na Bakhresa kwa kuwapulizia wasafiri wake.

Rais aliongelea fumigation iliyofanywa mitaa ya kariakoo kama wiki mbili zilizopita ambao mabwana afya walipulizia baadhi ya maeneo, akasema ile labda iwe ni kwa ajili ya mende na wadudu wengine lakini haiwezi kuua virusi vya corona.
 
Kocha kachoka na mbinu zimemuishia akishambulia timu huku nyuma inafungwa kiurahisi akipaki basi mambo yanamuendea kombo watu wanashambulia mpaka anachanganyikiwa kifup pumzi imekata hana namna isipokuwa kufurushwa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi huyo kocha ni mzuri sana. Pamoja na kwamba yuko kando ya uwanja lakini timu yake haija panic wala nini. Kama unavyoona wanapiga pasi golini kwao hadi adui anatoka udenda kua labda mpira utamtoka mguuni wauchukue kumbe kocha utadhani anasumaku, yaani mpira haumtoki hata!
Ni kweli timu haijapaniki labda kwasababu wanamuelewa vizuri kocha wao. Lakini kwa haraka haraka ni kama wanasua sua kuingia uwanjani maana tangu kipenga kipulizwe tunamuona kapteni tu akijaribu kuteta na refa. Huenda anajaribu kumnong'oneza kuwa wawape ushindi tu timu pinzani maana wachezaji hata jezi tu hawana, wanaingiaje uwanjani bila jezi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh! okay uzi open hv halafu kuna watu hawajaelewa?
Nahodha wetu haiyumkini kashaliwa na Papa Ana Nyangumi?Rada zote zamulika upeo wa usawa wa habari Naye haonekani.Nahodha msaidizi hana ???uzoefu au alionywa kutogusa usukani???

Hapa inabidi tujitahidi kuomba mawimbi yatuhurumie ndiyo salama yetu.
Bado napenda kuwauliza wahenga,Nahodha akirejea chomboni kwa mbwembwe tumshangilie?Tumpongeze?Tumtendeje?Bado anatufaa huyu huyu kuongoza chombo chetu?

Nani atatunusuru siye Watanzania?
Napendekeza tudai/tutafute Katiba ya Wananchi kwa maslahi mapana ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom