Vita ya kugombea mali za aliyekuwa Mchungaji, Marehemu Getrude Rwakatare sasa imeshika kasi

Tuna kitu cha kujifunza.
Kwa mtizamo wangu;
1. Kw sababu pamoja na kusoma, inawezekana lengo moja wapo ni kusaka utajiri basi muda wote wa kusoma sharti watoto wajifunze kile baba/mzazi anachofanya
2. Kuna muda watoto kutokana na kuwa isolated na shughuli za mzazi, inawezekana wakawa hawana shughuli za kufanya wakitegemea wazazi wakienda mbele ya haki waanze kuvurugana. Ni vizuri mzazi kuhakikisha watoto wote wana kazi zao either ajira binafsi au kuajiriwa ila atleast wawili au mmoja wakawa/akawa included kwenye system ya biashara za familia kwa sababu haiwezekani watoto wote wakawa wafanyikazi au CEOs
3. Kugawa shares kwa kila mtoto (equally), kwa wale waliopo kwenye system wapewe mshahara wawe kwenye ajira kama wafanyikazi wengine kwenye biashara
4. Biashara za familia zirasimishwe kikatiba kifamilia ili kujua nini muundo wa biashara na namna familia inavyofungamana nayo na namna kizazi cha kwanza mpaka cha nne na kuendelea kimeainishwa kinavyonufaika (equally).
5. Familia ijikite zaidi katika mashauriano ya kifamilia katika jambo lolote linalotokea badala ya kujikita zaidi kwenye sheria katika kutafuta haki. Familia ikubaliane hasa kwenye utamaduni wa kutumia wazee maalumu wa kuwashauri katika mashauriano yoyote pale mgogoro unapotokea badala ya kukimbilia mahakamani, twaweza kujifunza kutoka uhindini na umasaini au ukuryani

NB: kwa uzoefu wangu, mtoto toka mdogo akiwa karibu na mzazi mzazi akimpa mwongozo wa kile anachofanya mtoto si rahisi kukengeuka japo inawezekana kwa kuzingatia mfano wa mwanamfalme wa uingereza.
 
Huyo Tibe ni mbinafsi SANA eti kiss mtoto wa kwanza ndo alizimishe Mali zote ziwe zake
 
hii dunia ukitafuta mali sana ni kama unaanzisha vita ya watoto baadae....cha muhimu ni kuandika urithi mapema
Mirathi inakuwa challenged mahakamani

Kuomba Mungu tu

Afrika kuna kitu kimejificha unakuta wazazi wengi wenye akili sana ziwe za darasani ,kutafuta mali nk huzaa mitoto haina akili.Mfano ni huyo marehemu Mama Rwakatare
 
Mama alikuwa na watoto wangapi? Je watoto wote hao ni kwa mwanaume mmoja ? kama ni mwanaume mmoja kwa nini wafikie hatua hii?

ni maswali tu ndugu zangu tukipata majibu yake pasi tunaweza kupata pa kuanzia.
 
Watoto ni Wanne na Wote Baba mmoja.
Mama alikuwa na watoto wangapi? Je watoto wote hao ni kwa mwanaume mmoja ? kama ni mwanaume mmoja kwa nini wafikie hatua hii?

ni maswali tu ndugu zangu tukipata majibu yake pasi tunaweza kupata pa kuanzia.
 
Hivi kweli mali zote hizo za mama bado unagombea udiwani kuna shida sio bure.

Udiwani una faida kubwa sana. Maana mkurugenzi wa manispaa uliyopo anakuwa rafiki yako. Uwekezaji wako unakuwa hausumbuliwi sumbuliwi na watu wa serikalini. Na pia kwenye ma viwanja yakigaiwa wewe unapewa tu kwa urahisi
 
Wenyewe waarabu wanamkabidhi m1 ndio kiongozi wao.

Huwa wanaanza mapema sana kuwafundisha watoto wao biashara. Unakuta mtoto mdogo yupo dukani na wazazi wake. Alishafika miaka 20 anajua karibu kila kitu jinsi ya kuendesha biashara.

Ukweli wanaamiana sana, hawadhulumiani kama sisi. Hata wasomali na Igbo wako hivyo.
 
Hizi mali za kupata kwa janja janja huwa hazina mrithi. Angalia jinsi familia nzima ilivyoacha kupambana kwa kusubiri mali za mzazi. Wataziuza zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…