Unachokisema wewe ni sawa na mbuzi kupatana wagome kuchinjwa na binadamu. Harakati za waafrika kuwa na msimamo dhidi ya misimamo ya wazungu zilikuwepo tangu zamani lakini hazivua dafu. Zilianzia kwa akina Mkwawa, Isike, Rumanyika, Kimweri, Kinjekitile, Nyerere na akina Nkruma, Gadaffi, nk lakini wote walishindwa. Ikabakia if you can not fight them join them. Waafrika lazima tuamue kuunga mkono upande mmoja (ujamaa au ubepari) kama tunataka hatima yetu itabirike. Nionavyo mm sisi waafrika maisha yetu na tabia zetu zinafanana zaidi na Urusi, china, India, N.Korea kuliko Marekani, UK, France, Italy, au German. Hapa lazima tuachane na uvuguvugu ili tujulikane tuko baridi au tuko moto. Let us join the Putin's side tutafika mbali sana badala ya tabia ya kuomba sukari kutoka Marekani, majani ya chai kutoka Urusi, kijiko N.Korea, kikombe na kichujio kutoka UK. Tunaonekana kama malaya, hatuaminiki kwa mabepari wala kwa wajamaa.