Bwana Utam
JF-Expert Member
- Feb 15, 2016
- 19,559
- 36,514
NORTH KOREA na IRAN nimakoloni ya nchi gani !!!??Kwani Ukraine ni koloni la nchi gani.
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
NORTH KOREA na IRAN nimakoloni ya nchi gani !!!??Kwani Ukraine ni koloni la nchi gani.
Naomba orodhesha mafanikio ya Urusi toka avamie ukraine., andika kwa namba tafadhali, Umesikia ile habari ya majeshi 1000 ya urusi juzi kuzamishwa kwenye ule mto wakijarib kuvuka kuingia ukrain?sina uhakika kama unafuatilia kwa karibu hii vita. Urusi inafanikiwa sana kwenye malengo yake. Mpaka sasa Marekani na NATO wameufyata ndio maana kila wakati wanakutana kuongeza vikwazo dhidi ya urusi, askri wa ukrane, marekani na NATO wanauawa na kutekwa kila siku, silaha wanazopeleka ukraine zinaharibiwa na zinatekwa na warusi. Sasa hivi wanalia na Putin kama watoto
Kwani Finland na Sweden tayari ni wanachama wa nato? maajabu makubwaNaomba orodhesha mafanikio ya Urusi toka avamie ukraine., andika kwa namba tafadhali, Umesikia ile habari ya majeshi 1000 ya urusi juzi kuzamishwa kwenye ule mto wakijarib kuvuka kuingia ukrain?
Vipi kuhusu Finland na Sweden putin alisema wakijiunga na NATO atapiga nuclear ulaya, sasa jana rasmi wamepeleka maombi NATO, hizo nuclear ziko wapi?
Kwani Finland na Sweden tayari ni wanachama wa nato? maajabu makubwa
Safi sana mkuuView attachment 2227834
![]()
The Maastricht and Amsterdam Treaties | Fact Sheets on the European Union | European Parliament
Read about the Maastricht and Amsterdam Treaties. Fact Sheets provide an overview of European integration and the role of the European Parliament.www.europarl.europa.eu
Hiyo ni moja ya three pillars za EU walizokubaliana Kwenye ‘Maastricht Treaty’ wao wana foreign policy ya pamoja; among other things.
Elewa kwamba wanapoenda UN nyuma ya pazia wanakuwa washaafiki nini wana support kwenye foreign na madhara yake wana mitigating strategies za kusaidiana.
Wale sio kama waafrica wakifika UN kwenye kura huyu sijui ana abstain, huyu ana support na huyu kakataa. Wao kura yao yote moja based on continental intrest.
We mwafrika maskini unaenda huko unaambiwa usinunue mafuta Iran unaikubali tu, usinunue Venezuela haya na usinunue Russia haya; nchi zote hizo zina reserve kubwa uwepo wao sokoni bei ingeshuka sana.
Sasa kwa uchumi wetu ilipaswa tuwaambie na sisi either wafidie gharama za kupanda kwa bei ya mafuta kabla ya ku support ujinga wao; au wasitupangie soko la mafuta kwa migogoro usiyotuhusu ni uzwazwa kutokulinda continental intrests za bara kama wanavyofanya kwao.
Zimevamiwa na nchi gani?
Ana ushahidi gani kwa dai lake hilo.Akiondoa majeshi yake usalama wake dhidi ya MANAZI wenye misimamo mikali kwa taifa lake utalindwa nanani MKUU
RUSSIA asiondoe majeshi mpaka afikie malengo yake
Mungu awasimamie
Sent using Jamii Forums mobile app
mtu mwenye msimamo ni yule anaejitegemea, kama wewe ni tegemezi huwezi kuwa na msimamo wenye maana. Wazungu wamekosana sana na kiongozi au nchi inayoelekea kwenye kujitegemea. Wanapenda nchi na kiongozi ombaomba kwao maana watautumia udhaifu huo kupitisha agenda zAO ZENYE MANUFAA KWAO. usikubali kupewa msaada au mkopo na kuupeleka sehemu isiyozalisha kama vile kununua madawati, kujenga madarasa, kununua chakula, nk, ukifanya hivyo utaendelea kuwa tegemezi na ombaomba milele. hata marekani wanakopa China kwa riba ndogo na kukopesha wengine kwa riba kubwa, wanakopa na kwenda kuwekeza kwenye uzalishaji wa silaha za kivita halafu wanauza silaha hizo kwa wengine kwa bei kubwa.Sawa lakini aina maana kama nchi tusiwe na national and continental interest zetu katika siasa za kimataifa na maslahi hayo yanapochezewa tuwe na mbinu za kuyalinda au kupunguza athari zake kabla ya ku-support.
Ndio mabeberu yanavyo operate lazima tujifunze na sisi; yaani dunia ya leo bado kama bara, africa tuna support kila upuuzi huko UN bila ya kuwa na risk mitigation strategies za hayo maamuzi ndani ya nchi zetu. If you ask that is just incompetence of political knowledge and national security tactics.
Lengo la Urusi sio kuiteka Ukraine, kama lengo lingekuwa hilo angeshaiteka kwa siku tatu tu. Lengo lake kuu sio kuisambaratisha Ukraine bali kumaliza uwezo wake wa kijeshi anaotumia kuwapiga wale wazaozungumza Kirusi wanaotaka kujitenga. Anahakikisha kuwa analenga zana na vituo vya kijeshi tu na zile njia zinazotumika kuingiza silaha kutoka NATO baaasi, hii ndio inayosababisha achukue muda mrefu kufanisha hilo bila ya kuiharibu Ukraine. Kosa alilofanya Voladymil Zelensky ni kuwatumia raia wake kama askari kwa kuwapa silaha wapigane na Urusi, hii ndio inayosababisha Russia ipige hata majengo ya kiraia wanamoishi watu wa kawaida waliopewa silaha.Umepoteza muda mwingi kuandika hili porojo, kama urusi ina uwezo kuisambaratisha ulaya na marekani kwanza angefanikiwa kuiteka Ukraine japo kwa wiki moja sio sasa miezi 3 hajafanikiwa ata jampo 1 katika mahitajio yake.
Putin amejidhalilisha sana bora asingevamia ukraine mataifa ya Ulaya na Marekani wangeendelea kubaki na hofu ya Urusi lakini sasa ni kama vile uwezo wake wote ameuanika hadharani unamuumbua kutokana na ndaro zake alizokuwa akileta kabla.
Sweden na Finland wakiiogopa sana Russia na hawakutamanipo kujiunga na NATO wakihofia Russia lakini sasa baada ya uwezo wa Putin kujulikana na kila mtu jana mchana kweupee wamepeleka maombi ya kujiunga na NATO,
Hata wazungu ni wajinga, kwenye hili hesabu zao hazitakwenda vizuri. Wameshindwa kutofautisha kati ya Urusi na Afghanstan, au syria, au Iraq au Somalia au LibyaUmepoteza muda mwingi kuandika hili porojo, kama urusi ina uwezo kuisambaratisha ulaya na marekani kwanza angefanikiwa kuiteka Ukraine japo kwa wiki moja sio sasa miezi 3 hajafanikiwa ata jampo 1 katika mahitajio yake.
Putin amejidhalilisha sana bora asingevamia ukraine mataifa ya Ulaya na Marekani wangeendelea kubaki na hofu ya Urusi lakini sasa ni kama vile uwezo wake wote ameuanika hadharani unamuumbua kutokana na ndaro zake alizokuwa akileta kabla.
Sweden na Finland wakiiogopa sana Russia na hawakutamanipo kujiunga na NATO wakihofia Russia lakini sasa baada ya uwezo wa Putin kujulikana na kila mtu jana mchana kweupee wamepeleka maombi ya kujiunga na NATO,
Lengo la Urusi sio kuiteka Ukraine, kama lengo lingekuwa hilo angeshaiteka kwa siku tatu tu. Lengo lake kuu sio kuisambaratisha Ukraine bali kumaliza uwezo wake wa kijeshi anaotumia kuwapiga wale wazaozungumza Kirusi wanaotaka kujitenga. Anahakikisha kuwa analenga zana na vituo vya kijeshi tu na zile njia zinazotumika kuingiza silaha kutoka NATO baaasi, hii ndio inayosababisha achukue muda mrefu kufanisha hilo bila ya kuiharibu Ukraine. Kosa alilofanya Voladymil Zelensky ni kuwatumia raia wake kama askari kwa kuwapa silaha wapigane na Urusi, hii ndio inayosababisha Russia ipige hata majengo ya kiraia wanamoishi watu wa kawaida waliopewa silaha.
Ni ngumu kujua NATO imepanga nini juu ya Russia, yeye ndo mwenye kauli ya Russia ashinde au asishinde. Hivi sasa russi amenza tumia laser weapons, hypersonic missiles n.k hii inaashiria pale maji yamekuwa kina kirefu kwake.Yaan unawaza Russia kuziangusha nchi za ulaya ila huwazi Ukraine kumwangusha Putin upo serious mseeee? Yaan leo hii Ukraine wanashambulia mpaka ndani ya Russia tofauti na mwanzo hulioni hilo?
Huoni kuwa saiz warusi wana hasira na Putin mpaka wanasubiri waingie barabarani wamtoe kwa nguvu sababu maisha yamekuwa magumu na uwezekano wa kushinda haupo?
jana hujaona battalion nzima imepigika na Ukraine na most of them died?
In short acha story za kwenye kahawa tafuta vyanzo mbalimbali vya habari hutaleta tena humu hizi story za vijiweni
Hawawezi kukuelewa ila huu ndio ukweli.Ulaya na American kukiwa na maisha magumu, Warusi watakuwa na maisha magumu Mara mia zaidi,
Ni vile russia vyombo vya habar kote vimepigwa pini, la sivyo tungesikia mengi yanayofukuta huko russia.EU inamwona Putin kama adui zaidi kuliko China.
Inajua inahitaji umoja wao ili kubaki kuwa na sauti duniani.
Wanachama wa EU ni waumini wa demokrasia kitu ambacho Putin amekipa kisogo.
Wazungu wanajua athari za utawala wa kiimra kama wa Putin ,,,
hii vita isingetokea kama Urusi wangekuwa waumini wa democracy.
Warusi walio wengi hawapendi vita anayoiendesha Putin kwasasa.
Naweza sema hili ni game ambalo limetokea katika wakati mzuri kwa wamarekani kwani wanae Biden ,,, ni matokeo ya upuuzi wa Trump kukosa jicho la karibu kuichunga Urusi na washirika wake akiwemo China.
alichofuata kyiv ilikuwa kusambaratisha miundombinu yote inayotumika kuchochea vita kama maghala na viwanda vya silaha, njia za kurukia ndege, miundombinu ya mawasiliano ili iwe vigumu kuratibu vita. alipofanikisha hilo hakuona umuhimu wa kukaa kule tena, maana lengo sio kumkamata Rais Zelensky bali kudhoofisha nguvu za kijeshi za Ukraine na washirika wake. Kama Ukrane na NATO wangekuwa na ubavu wangeifukuza Urusi pale Mariupol na kuwaokoa askari wao waliokwama kwenye kiwanda cha chuma. Kumba pale kwenye kiwanda kuna askari wengi sana wa kigeni (US, UK, Canada) na waukraine wenyewe. Kama NATO na Ukraine ingekuwa na uwezo basi wangewaokoa watu wao pale, lakini wameshindwa hadi askari wale wakajisalimisha kwa majeshi ya urusi,Sasa mbona mizigo ya silaha inaendelea kumiminika Ukraine? Nakumbuka siku ya kwanza ya uvamizi alisema Donbas ishakuwa huru watu wa miji ile wakasherehekea na kupeperusha bendera imekuwaje tena saivi bado anapapatua na alishatangaza kabla kwamba ni huru?
Kama mpango sio kuiteka Ukraine kule Kyiv ambako alipata kichapo na kurudi zake Donbas alienda kufanya nini hasa? Kwanini tuliambiwa Kyiv imezingirwa na akawataka jeshi la ukraine lijisalimishe na mpaka kutoa masaa mara kadhaa ivi putini alipatwa na nini hasa kule Kyiv, em kokomoka tujue alichofata lakini kwanini alichomoa baadae na yale masaa yalipita na kupitiliza hadi leo ni ipi adhabu yake baada ya majeshi ya Ukraine kukataa kusarenda masaa yalipoisha?
Je unayo habari ya Finland na Sweden?
Upo sahihi kabisa, na sio vijana tu, hata watu wazima, ndo maana china, nchi za falme za kiarabu, russia wenyewe n.k wanakimbilia saaana kula bata la nchi za Ulaya na US.Acha Uwongo,,Chancellor wa Ujerumani alitangaza muda kwamba Hatogombea tena...Russia nu muda tu utasema. USA NA ULAYA Magharibi haijawahi kushindwa,,unajua sababu ni nini?? Vijana kutoka nchi zinazofuata siasa za mkono.wa chuma kama Russia, China,Ulaya mashariki,na hata Uarabuni,,wanapenda mtindo na siasa za Kimagharibi...Putin atatoka kama alivyokwenda Mikhail Gorberchiv...Mtindo na siasa za Kimagharibi zinzavutia Vijana weengi kutoka nchi za Kikomunisti na Ki shoshalist.
Baada ya ndege kudunguliwa akaanza kurusha makombora ya masafa marefuTena Russia wamesema wanasubiri kura ya maoni ya lile jimbo la Mashariki (wakikubali kujitenga na Ukraine, watakuwa wamefanikiwa lengo lao, wataacha kupigana), lakini ukweli Urusi mambo yapo shingoni, anatafuta mlango wa kutokea bila aibu.
Ni vigumu sana Russia yenye uchumi dhaifu kiulinganifu, kuwashinda wenzake wengi wenye uchumi mzuri, walioungana.
Ndege za Urusi zilizotunguliwa, zimeonekana kutumia GPS za kawaida za kusafiria kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha kuhudumia ndege zake za kivita. Kwa sasa ndege zake kila zikiruka zinadunguliwa. Wamebakia tu kurusha makombora, lakini siyo kuruka angani kama mwanzo.
Je, nguvu ya kijeshi ya Ukraine sasa imedhoofika? kama lengo ni kuvuruga miundombinu kwanini viongozi wa ulaya na marekani hutembelea Kyiv muda wowote huwa wanatua kwenye viwanja vipi? niliwaona uropean union, boris johnson, katibu mkuu wa umoja wa mataifa, mke wa rais wa marekani na wengine hawa wote walipitia wapi?alichofuata kyiv ilikuwa kusambaratisha miundombinu yote inayotumika kuchochea vita kama maghala na viwanda vya silaha, njia za kurukia ndege, miundombinu ya mawasiliano ili iwe vigumu kuratibu vita. alipofanikisha hilo hakuona umuhimu wa kukaa kule tena, maana lengo sio kumkamata Rais Zelensky bali kudhoofisha nguvu za kijeshi za Ukraine na washirika wake. Kama Ukrane na NATO wangekuwa na ubavu wangeifukuza Urusi pale Mariupol na kuwaokoa askari wao waliokwama kwenye kiwanda cha chuma. Kumba pale kwenye kiwanda kuna askari wengi sana wa kigeni (US, UK, Canada) na waukraine wenyewe. Kama NATO na Ukraine ingekuwa na uwezo basi wangewaokoa watu wao pale, lakini wameshindwa hadi askari wale wakajisalimisha kwa majeshi ya urusi,