Uzima Tele
JF-Expert Member
- Jan 20, 2023
- 1,270
- 2,822
Ni Athuman Kapuya Foundation, taasisi ya Athuman Kapuya
Leo imeamuriwa na RC wa Mkoa wa Tabora ndugu Paulo Chacha, Athumani Kapuya akamatwe na kushitakiwa kwa taasisi yake kuingiza maelfu ya vitabu vya msaada na vifaa vingine kama gloves, pads za kike nk kupitia taasisi yake vyenye maudhui ya kufundisha watoto ushoga..
======
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paulo Chacha akiwa katika Wilaya ya Kaliua amesema vitabu hivyo vimewekwa kizuzini baada ya serikali kupitia watalamu wake kubaini kuwepo kwa uchafu wa maudhui katika vitabu hivyo ambayo vimeingizwa Wilayani humo na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Athumani Kapuya kwa lengo la kuvitoa msaada kwa shule za msingi na sekondari.
Akizungumza Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Dkt. Amini Joseph ameongeza kuwa Msaada huo wa vitabu uliingizwa Sanjali na vifaa tiba ikiwemo vilainishi na taulo za kike.
Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Dkt. Rashidi Chua chua amesema shehena hiyo imekamatwa ikiwa na vitabu zaidi ya elfu nane ambavyo huenda vingezifikia shule za msingi 139 na za sekondari 32 katika wilaya hiyo.
Kufuatia Sakata hilo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha ameifungia Taasisi hiyo isiyo ya kiserikali ya Athumani Kapuya kutokuendesha shughuli zake ndani ya Mkoa wa Tabora wakati huo akiagiza kukamatwa kwa waratibu na viongozi wa Taasisi hiyo.
Pia soma: