Hapana mkuu,yapo mambo ambayo yaliishia Calvary,na hili ni moja wapo,kama vile talaka nk..Nimekupa maandiko ambayo yule mwanamke Msamaria mzinzi Bwana Yesu mwenyewe hakumhukumu,soma tena.Haya hapa.
Yohana 8:3-11
3 Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati.
Yohana 8:3
4.Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini.
Yohana 8:4
5. Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje?
Yohana 8:5
6. Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
Yohana 8:6
7. Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
Yohana 8:7
8.Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
Yohana 8:8
9. Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati.
Yohana 8:9
Tatizo ni kwamba hukumu zetu,si za haki,ndio maana Mungu amekataza tusihukumu.Naomba usome maandiko yafuatayo.
Mathayo 7:1-5
1 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.
Mathayo 7:1
2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa
Mathayo 7:2
3 Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?
Mathayo 7:3
4 Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?
Mathayo 7:4
5 Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.
Mathayo 7:5