Vitu ambavyo mwanaume unatakiwa uvijue kabla havijakuua

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,778
Reaction score
8,232
Mwanaume hukuzaliwa kuwa mtumwa wa tamaa ya mwili wako
Lakini usipozinduka mapema, tabia zako sio tu zitakuua bali zitakuzika ukiwa hai.

Wengi wa wanaume hawaharibiwi na maadui zao....bali na tabia zao...

Zifuatazo ni tabia, uraibu na fikra ambazo zinawaua wanaume kimya kimya

1. Ngono (sex):
Wanaume wengi wameharibu na kuzika hatma zao kwa sababu ya ngono.

Ngono ni mtego wa adui wa kukuangusha. Wanaume wengi tena mashujaa wenye nguvu waliangushwa kwa mtego kidogo tu wa ngono.

Usipoudhibiti uume wako utakuzika ukiwa hai.

2. Kukimbizana na wanawake (chasing women):
Unafikiri na kujiona ni bingwa na mshindi kwa sababu unatafuna kila mwanamke mzuri anayepita mbele yako?

Nikuambie ukweli mchungu wewe sio mshindi bali wewe ndiye uliyeshindwa. Unachofanya ni kupoteza muda wako, kupoteza fedha zako, kupoteza nguvu zako na muhimu zaidi kupoteza malengo, mission na hatma yako.

Wanaume halisi hukimbizana na fursa za kiuchumi, hujenga himaya zao, hukimbizana na kujenga legacy itakayoishi milele. Wavulana hukimbizana na makalio makubwa wakidhani ndio ubingwa.

3. Picha, video na filamu za ngono (porn):
Hii ni sumu inayoua udhabiti wa fikra. Kutazama maudhui haya huua motisha (motivation) iliyoko ndani yako, inadhoofisha uhitaji wako wa kupata mwanamke halisi. Kutazama picha hizi hukufundisha kuwa mtazamaji badala ya kuwa mshindi.

4. Kupiga punyeto (masturbation)
Unadhoofisha nguvu zako za misuli (masculine energy) kwa sababu ya raha ya sekunde 10?
Hakuna mwanamke anayemheshimu mwanaume anayefika kileleni ndani au chini ya dakika moja. Inakera, ni aibu, ni fedha.
Utachagua kutawala tamaa yako ya kupiga punyeto au ikutawale.

5. Madawa ya kulevya mihadarati na bangi (drugs and weeds):
Vitu hivi havikupi starehe, havikusahaulishi shida zako, havikuondolei shida zako bali vinakufanya uukwepe ukweli, ukwepe kuongezeka.

6. Pombe (alcohol):
Kuwa mlevi hakukufanyi kuwa mjanja bali kunakufanya uwe mdhaifu na utakayesahaulika. Ulevi ni miongoni mwa vitu vinavyoondoa heshima ya mtu. Ulevi ni sumu inayokuua polepole lakini kwa uhakika (kills slow but sure).

7. Kutaka kila mtu na kila mwanamke akuone mwema (nice guy):
Mara nyingi ukiona wanawake wanakusifu sana kuwa wewe ni nice guy, ni understanding ujue wanamaanisha wewe ni mwepesi na rahisi kutumika. Wanamaanisha wanakutumia kirahisi tu. Sisemi usiwe mtu mwema, nasema acha kutaka kuonekana mwema kwa kila mtu hata pale ambapo wema huo unakuumiza.

8. Kula starehe kila weekend
Wakati unapoteza muda na fedha zako kila weekend kufanya starehe huko night clubs, bar na disco, kuna mwanaume mwingine anatumia pesa zake, nguvu zake na muda wake kujenga aina ya maisha na uchumi ambao utaishi ukiutamani maisha yako yote.

Jitoe kafara leo au ujute milele. Kumbuka tu majuto ni mjukuu.

9. Kukubali kuishi maisha ya chini (low standards)
Kila unachotafuta unatafuta cha low standards. Ni mwanamke low standards ni marafiki low standards, ni malengo low standards yani kuanzia malengo yako ni ya hali ya chini na hata heshima yako binafsi ni low standards. Acha kufikiri kimasikini, unawaza kimasikini mno.

Pandisha viwango vyako, jiongezee thamani, kataa kuzungukwa na mediocrity.

10. Kuishi bila malengo
Unaishi tu, unaamka huna malengo, huna muelekeo, huna mkakati, huna hata dili unayoisikilizia.
Huo sio uhuru ni kufeli maisha.

11. Kuogopa kuwa watu watasemaje, kuogopa kuwa watu watakuonaje, kuogopa kuhukumiwa.
Kila unalotaka kufanya unaanza kuwaza watu watasemaje au watanionaje. Huo sio uanaume, huo ni ukibaraka (puppet). Unataka uwafurahishe watu? Unadhani utafaulu?

12. Kuahirisha mambo na kusema nitafanya kesho, nitafanya siku sio nyingi, nitafanya nikipata hiki au kile.
Muda haukusubiri. Anzia hapo ulipo, Anza na ulichonacho.

Mwenyekiti nimalize kwa kusema kuwa mwanaume usipoua hizi tabia, zitaua morali yako, zitaua nguvu zako za msukumo, zitaua kesho yako, zitaua hatma yako na zitaua uanaume ulioko ndani yako. Na si tu kuwa zitakuua bali zitakuzika ukiwa hai.

Utabaki kuwa mwanaume wa kutazama wanaume wengine wakiishi maisha ambayo wewe ulipaswa kuyaishi.

🔥 Ziue tabia hizi sasa hivi — au zikuue polepole lakini kwa uhakika

🔥 Kill them now — or die slowly but sure
 
Attachments

  • Screenshot_20250806_164550~2.jpg
    Screenshot_20250806_164550~2.jpg
    78.2 KB · Views: 41

Kwahiyo huyo ni mchungaji katika ubora wake sio?
 
Nakula starehe kila weekend post mali zako hapa na zangu naposti na familia yenye afya na furaha halafu wadau waseme nan katisha
 
Wapi nimesema nimekamilika bwashee ? Tuanzie hapo kwanza
Nimekuuliza kwa mtu yeyote aliokamilika aishije yaani asiwe na mwanamke wala asipige nyeto hizo spam ziende wapi? Nisaidie kumjibu ndugu mwandishi
 
Back
Top Bottom