Vitu gani husababisha Wanawake wanune?

Vitu gani husababisha Wanawake wanune?

Inategemea huyo anayenuna ni wa level gani. Kama ni matawi ya juu inabidi tu umbembeleze, kumsifia na mabusu kem kem.

Kama ni wa huku Mbagala kichemchem, nunua mchele wa Kyela kilo tatu, nyama iliyonona huku umeweka elfu tano mezani.

Ndugu kwanza utapelekewa maji bafuni ili uondoe kiwingu wakati anakatakata nyama huku amevaa khanga moja iliyorojoka na mdomoni anaimba taarab.

Kama ni wa Kimara mpigie simu bodaboda wako huku ukimuambie apitie kilo tatu za kitimoto hapo kwa Masawe kwani ulishazilipia asubuhi. Ghafla utaona manka anaanza kutabasamu na kuvaa nguo fupi fupi zinazoonyesha magoti.
 
Alafu man usipende kutafuta suluhu kwenye makosa ambayo hujasababisha wewe hawa viumbe ukiwajali sana wanakudharau mwanaume unatakiwa ukaze siyo kila ukitikiswa unatikisika akigundua udhaifu wako ulipo atapiga hapo hapo mara kwa Mara kwahiyo hata Kama kagusa kwenye udhaifu wako usiwahi kumdhihirishia kuwa kakugusa pabaya Kama unataka kulia kalilie mbali ila ukirud hom mikausho ataongea tu mwnyewe ni kawaida hiyo
Umameliza kila kitu [emoji122][emoji122]

Sent from my TECNO BC2 using JamiiForums mobile app
 
...Kwa nini anaku avoid mkuu??? au kasikia una mchepuko???lol...unahitaji kuongea nae openly, umuulize nini tatizo..?, kuwa direct and specific...Labda ukienda kazini, mwambie leo nikirudi nina mazungumzo na wewe..au mwambie tutoke nina mazungumzo na wewe, tafuta sehemu nzuri isiyo na kelele..ambayo unaona mnaweza mkaongea na kureflect kwenye muelekeo wa uhusiano wenu.....kisha mmuulize akuambie nini tatizo....mwambie siku hizi mwenendo wako siuelewi, kila nikirudi huna furaha, umenuna nini tatizo mke wangu, usionyeshe kukasirika wala kutumia lugha ya kumu accuse...lazima a
Ushauri murua sana namimi nimechukua point kwa matumizi ya baadae.
 
Kusema ni ngumu kwa kuwa anataka kubembelezwa wewe ndio uanze kwa kumuuliza kuwa' babe mbona kamaaa.....hauko sawa" na bado utakuta anakujibu"hakuna kitu kawaida tu" hapo anahitaji kubembelezwa
Haka kamtindo anako my wangu, utaskia " niko kawaida tu" hahhaha ukibembeleza kidogo tu anaanza kufunguka tuvitu tudogo tudogo ulivyofanya.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
 
Dah! mwanangu sisi mabachela tukiingilia kati mnapaniki mnataka kutuua, sasa imagine huyo sio mke wangu ila najua ni nini kinachomsumbua wewe hujui.
[emoji23][emoji23][emoji23] dah nakubal dam yang
 
Jamani nataka niulize ni week sasa Mke wangu kanuna na sina kitu chochote nimemfanya,

Hivi vitu gani vinasababisha wanawake kununa kwani na mimi nimebaki kimya tu sasa sielewi huku kununa kwa mwenzangu kutaisha lini[emoji854]

View attachment 2254298
Picha kutoka maktaba
Wanawake ndo tulivo..... Ndo tuneumbwa tu hvo..... Ndo upuuzi wetu huo....mkeo akifanya hvo mkomeshe usimchekee, usimsemeshe ovyo, usimshirikishe chchte. Hapo atazid kununa alf badae atakuchekea....Akikuchekea hapo mwambie hadi anune tena
 
Duuu wanawake sijui tunakwama wapi,,, kuna jamaa nae alikuwa anasimulia kuwa mkewe alimnunia week nzima kisa tu mwanamke alivaa nguo mpya na jamaa hakumsifia kuwa kapendeza mbaya zaidi jamaa hakujua kosa lake ni kutotambua kuwa mkewe kavaa nguo mpya.

Mwanamke anaweza kununa kwa sababu ya kitu kidogo sana na asiweze kumwambia mwenza wake ni nini tatizo , na wengi hudhani kununa ni suluhisho kumbe wanaume wanachukulia powa tu
Umewakilishe vyema sana mrembo, Naomba ujengewe sanamu la heshima pale wilaya ya idununde kata ya kashibwa, karibu na nyumba ya mjumbe wa shina mzee mathayo[emoji41]
 
Kama bado kanuna asubuh ukiondoka muachie kalamu na karatasi aandike kinachomsibu.
 
Kaka wanawake ni kama waves(mawimbi) ya maji baharini kuna muda yanajaa kuna muda yanapungua, ndo walivyoumbwa kun a wakati anakuonesha kujali, utachati naye vizuri tu, mnacheka lakini utashangaa kesho hajibu text zako wala calls, amekununia ghafla, hii hali inawatokea hata wenyewe wanakuwa hawaelewi kwann, wewe mwanaume hapo unachohitaji ni kutodeal naye kabisa mpe mda wala usimuulize why amenuna kama unajua kabisa haujamfanyia something wrong, unajua wanawake wao ili wawe free kuonesha upendo wao kwa wenzi wao wanahitaji kujifeel comfortable kufanya hivyo,

ama tu atakua hayuko huru,hana amani maybe labda kuna vitu vyake nje ya mahusiano yenu haviko sawa, ndo maranyingi huwa wanachange, sasa vita inaanza ukimuuliza kwanini amekuwa hivyo, yaani kama unataka hali iwe mbaya zaidi wewe jaribu kutaka kujua kinacho mtatiza, hapo ndo ugomvi huwa mkubwa, kama nitakushauri kitu wewe mwanaume ukiona mwenzi wako anapitia hii hali ya kununa bila ya wewe kumfanyia kosa usimuulize chochote wewe muache, yeye mwenyewe akiwa sawa atarudi katika hali. Not every ploblems needs to solved, sometimes solving a problem can be a problem.
 
Mwanamke anaweza kununa kwa sababu ya kitu kidogo sana na asiweze kumwambia mwenza wake ni nini tatizo , na wengi hudhani kununa ni suluhisho kumbe wanaume wanachukulia powa tu

Au ile amekuona asubuhi anakunywa uji wa mtoto, hakuambii ila atanuna utahisi kaona sms za mchepuko,kumbe yasiyo ya maana makasiriko
 
Mara nyingi Kama mwanamke amenuna, mkifanya Hadi akatema cheche, ile Hali ya kununa nuna inaisha.
Sasa ole wako asiteme (kojoa) cheche, ndio ataanza upya akiamini Kuna unae mtoa cheche somewhere.
 
Atakuwa ameachwa na mpenzi wake...🍃
Jamani nataka niulize ni week sasa Mke wangu kanuna na sina kitu chochote nimemfanya,

Hivi vitu gani vinasababisha wanawake kununa kwani na mimi nimebaki kimya tu sasa sielewi huku kununa kwa mwenzangu kutaisha lini[emoji854]

View attachment 2254298
Picha kutoka maktaba
 
Jamani nataka niulize ni week sasa Mke wangu kanuna na sina kitu chochote nimemfanya,

Hivi vitu gani vinasababisha wanawake kununa kwani na mimi nimebaki kimya tu sasa sielewi huku kununa kwa mwenzangu kutaisha lini[emoji854]

View attachment 2254298
Picha kutoka maktaba
Kama hamna housegirl, yupo dada mmoja kutoka Zanzibar apa ana taqo ni hatari anatafuta kazi za ndani, naweza kukuunganisha nae huenda mkeo kachoka kazi kila siku afue, apike, kudeki anahitaji msaidizi
 
Inaweza ikawa humpi ela yakutosha , au Kuna kitu Huwa unamfanyia hujamfanyia [emoji28][emoji28],au kapata habari mbaya znazokuhusu hko njee
 
Sababu yaweza kuwa;

1. Mapokeo, kwamba katika malezi yake na kukua amekuwa akiona wake kuwa na tabia ya kununuia wanaume zao Kwa hiyo nae akapokea hivyo kuwa ndivyo ipasavyo kuwa na yeye akiolewa.

2. Traumatic disorder

Kwamba huenda kuna mtihani anaupotia mfululizo matharani changamoto ya uzazi, ugonjwa wa yeye mwenyewe au mtu wake wa karibu.

3. Ujinga , akipata mafundisho sahihi na kuwa tayari kuyapokea ataweza kubadilika.

4. Hakupendi.


5. Mmerogwa , mmetupiwa mfaraka baina yenu na mahasidi.

6. N.k.
 
Back
Top Bottom