Vitu/vifaa gani ulivinunua kwa mihemko na umejikuta huvitumii kabisa?

Pods nilifata mkumbo nimeshindwa kabisa kutumia na nikagawa

Kitu kama situmii sikai nacho

Hapo kwenye mkanda wa ngozi nilinunua coco beach kwa wamasai
Kufika home mkanda mkubwa nimeshindwa kutoboa mpka leo nimgumu 🙌🙌
Huna haja ya kutoboa,kata kuke kwenye buckle kwa kupima saizinyake na ufunge tena kwa star screw driver
 
Nilinunuaga min oven nilitumia mara chache tu, nikapata lile jiko lenye oven yake
Sasa kale ka min oven sikatumii kapo tu

Nikanunua baking tins kwamba naanza kutengeneza keki, ubusy umezidi sijawahi kuzitumia hadi leo.
 
Nimenunua outlander 2450cc afu mafuta yamepanda, naona mzigo, nlikiwa natumia passo 990cc na kila week nlikuwa nasafiri 500 to 600 km sasa hili dubwasha mhhj. Watu walikuwa wananicheka nadrive gari sio ya hadhi yangu, nlinunua kuwanyamazisha sasa inanikomesha mafuta ila naitumia hivohivo
 
Kuna gari la mafuta lilidondoka lenye mafuta yameandikwa JET A1 yakawa yanatiririka, nikaufuata nikazoa kama lita 80 hivi,mpaka wa leo miaka 3 imepita sijui niyafanyie nini na nimuuzie nani.
HAyo ni mafuta ya ndege,huko mjini watu wananusa ili walewe
 
Vaccum cleaner.
Cofee machine.
Dish machine.
Home gym imejaa makorokoro kibao ya mazoezi ila hayatumiki.
Grass cutter.


Roho inaniumaga nikiwazia hela zilizopotea bure😭
 
Laptop nilipewa na idara ya kazi kwa ajili ya kutafutia kazi
Sikuitumia kabisa ingawa nilipata kazi
Nilimtumia kijana wa chuo imsaidie

Kama huna kazi nacho toa
 
Kuna gari la mafuta lilidondoka lenye mafuta yameandikwa JET A1 yakawa yanatiririka, nikaufuata nikazoa kama lita 80 hivi,mpaka wa leo miaka 3 imepita sijui niyafanyie nini na nimuuzie nani.
Duu jet hio zi inact tu kama wese la taa
 
massage gun
wifi yenu nlimnunulia mkanda wa post natal havai nikaanza kuuvaa na msuli
Sasa tangu nmepasua shipa sivai misuli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…