Vitu vya uongo tunavyoonyeshwa kwenye muvi za kizungu

Vitu vya uongo tunavyoonyeshwa kwenye muvi za kizungu

Hii ipo mkuu in real life sema haitokei ovyo na wabongo wengi huiforce..

wakati nitendo linakujaga automaticaly bila wahusika kujielewa mnajikuta tu..

Unatembea zako njiani uko bize na simu. Ghafla unagongana na mdada aliebeba makorokoro kibao na yanaanguka chini (always huyu mdada lazima awe pisi kali). Anachuchumaa kuyaokota na wewe unamsaidia.

Wakati mnayaokota unamshika mkono.. anakuangalia usoni na wewe unamuangalia macho yanagongana... mnaangaliana kama dakika mbili halafu taratibu mnaanza kusogeleana mpaka midomo inakutana mnakiss, mvua inaanza kunyesha na kuanzia hapo mnakua wapenzi! Kesho yake mnaonekana mko beach mnakimbizana na kumwagiana maji....Life is so easy kwenye movies.😂😂
 
🤣🤣🤣🤣 au anatokea mtu kwa nyuma anampiga gongo la kichwa , kama sivyo unaskia mlio wa risasi paaaaaaah! unajua staring amekufa ivo. mara adui anadondoka taratiiibu huku steringi haamini amini kilichotokea , ndipo anapojitokeza mpenzi wake na kabastola mkononi , wanakumbatiana na denda juu, huku maandishi ya movie kuisha yakiwaziba msione kilinachoendelea. yan hawa sijui wanatuonaje?
Na unakuta dakika mbili zilizopita huyo adui (ambae ni muuaji wa kutisha) alikutana na huyo mpenzi wa staring kwenye ngazi, akampiga ila hamuui anamuacha amelala hapo na bastola ipo pembeni ndio anamfata staring. 🤣🤣🤣 Jamaa wanatuona maboya sana
 
1. Bunduki kutokuisha risasi. Ushawahi ona kwenye muvi mtu ana ki bastola au SMG anamwaga risasi lisaa lizima na haziishi? Uongo mtupu.

Na hiyo Movie inakuwa ya masaa 3 au 5?

Wazungu wanatudanganya sana kwenye movie zao ni kweli kabisa ila ni Uwongo wenye kufanana na kweli kabisa mpaka kuja kugundua umedanganywa ujue umedanganywa kweli kweli.
 
Mdada Mhusika Mkuu wa muvi (queen wa muvi) lazima awe mrembo tena lazima awe na uhusiano wa mapenzi na star wa kiume. Kadhalika star wa kiume lazima awe handsome. Kisha muvi nyingi wawili hao ndo wanakuwa kila kitu wanakijua hapo mtaani kwao na hakuna anayewazidi

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Hahahaaa mkuu huwa nashangaaga majambazi wa aina hiyo yaani anaacha kumuua sterling on the spot anaanza kumuongelesha na kujitamba huu ni uongo kabisaa
Yaani wanaudhi sana hawa jamaa. Unakuta jambazi kaingia home kwa mtu kimyakimya usiku, anamkaba na mito au anamchoma kisu mtu anakufa. Hakuna mtu aliemuona jambazi kupo kimya kabisa. Cha ajabu jambazi akirudi kwenye gari/pikipiki yake aliyopaki kichochoroni kwenye giza, anaifurumsha kwa mwendo wa kasi ajabu na makelele kama yote. Mbele kidogo anawapita maaskari waliopaki zao pembeni wameuchapa usingizi mpaka wanashtuka na kuamka wanaanza kumkimbiza 🤣🤣🤣🤣 Hapo unakuta eti huyo ni serial killer wa kimataifa ameshawasumbua sana polisi, interpol, CIA, KGB mpaka JWTZ wanamtafuta miaka nenda rudi 😂😂😂
 
😂😂😂😂😂kubabae
 
Mdada Mhusika Mkuu wa muvi (queen wa muvi) lazima awe mrembo tena lazima awe na uhusiano wa mapenzi na star wa kiume. Kadhalika star wa kiume lazima awe handsome. Kisha muvi nyingi wawili hao ndo wanakuwa kila kitu wanakijua hapo mtaani kwao na hakuna anayewazidi

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app

Na star wa muvi hata awe kijana mdogo mwanafunzi wa chuo, ila lazima ukute anajua kuendesha kila aina ya usafiri kuanzia gari, pikipiki, boti, edikopta, treni.... yaani hata umpe kifaru anagonga gia...😂😂😂😂
 
Star anapigwa risasi hata 15+ lakini hafi.
Jambazi sasa, risasi moja chaliiii
 
Muvi za kutisha sasa: 😳

Ni usiku wa manane, giza totoro, umeme umekatika, mvua inanyesha huko nje na radi. Mtu anashtuka usingizini anasikia kitu kinagusagusa kwenye banda la nje ambalo liko umbali kama wa kilometa moja kutoka main house. Cha ajabu huyo mtu anatoka na kuanza kwenda kwenye hilo jengo bila chochote usiku huo kuangalia kuna nini!! 🤣🤣🤣🤣 Yaani hata kama nyumba imejaa watu hawezi amsha mtu amwambie amsindikize. Asubuhi ndio watu wanaanza kumtafuta hawamuoni, wanakuja kukuta kiganja cha mkono tu ndio kimebaki😀
 
I'll Ni filamu tu,na huo uongo unaendana na ukweli ndo unaoburudisha na kuleta msisimko.....
Ni kweli mkuu kuburudika tunaburudika ila ifike mahali tuseme enough is enough jamaa waturudishie chenji zetu 😀😀. Haiwezekani inapotokea star labda ametekwa halafu anasafirishwa kwenye msafara ma magari kama matatu manne hivi. Mara anatokea jamaa na rocket launcher anaanza kuyalipua yale magari. Haijawahi kutokea gari ambalo star yupo ndio likawa la kwanza kulipuliwa! Yaani magari yote yatalipuliwa ila lakwao litabaki na watatoka wazima au watatoroka somehow. 😂
 
Kuna ile eti unakuta jamaa kakutana na demu, hata hawajuani. Wanaongea maneno mawili matatu jamaa anaanza kumuangalia demu usoni halafu anamsogezea uso taratibu. Eti demu nae anasogeza mpaka wanakiss. Hii ijaribu mitaani uone utakavyolambwa makofi [emoji1787]
Ongezea wanabanduana bila kondomu na wakimaliza mbanduano hawaogi
Anatokea adui jamaa wanapgana then anashinda maadui wote.
Hawapati mimba, wanaobanduliwa na mtongozo wa kwenye movie ni mwepesi

Na kama nyumba zote wanazoingia lazima ziwe na wall colour painting za ukweli iwe kwa tajiri mpaka kwa maskini wa kutupwa
 
Na ikitokea akapata mimba ni siku hiyohiyo tayari tumbo linakua kubwa mtu hawezi kutembea na kiuno kinamuuma. 😀
 
Back
Top Bottom