True story.
Kuna dogo alikuwa anafanya vibaya shuleni.
Akapeleka ripoti kwa baba yake. Ripoti mbaya.
Baba akamuuliza, imekuwaje umefanya vibaya hivi?
Mtoto akajibu, mimi sina akili, sina kumbukumbu. Nikisoma nasahau.
Baba akawa kama kakubali jibu. Hakuhoji zaidi.
Siku mbili zikapita, yule mtoto akaona mtu anasoma gazeti. Akaomba yule mtu akimaliza kusoma ampasie gazeti.
Dogo akawa anafunguka, anasema anataka kuangalia msimamo wa ligi, kwani Simba ina pointi hizi, Yanga ina pointi hizi, magoli ya kufunga mangapi, michezo iliyobakia mingapi, akawa anatiririka data nyingi za soccer pale.
Sasa yule baba yake pale pale akamuuliza. Wewe si umesema huna akili, shuleni ukisoma unasahau? Sasa haya mambo ya msimamo wa ligi mbona unayakumbuka vizuri sana?
Baba akasema, wewe tatizo lako si akili, akili unazo nzuri tu, tatizo lako huna interest na shule.