Vituo vya Mafuta hufanya nini na Risiti wanazobaki nazo?

Vituo vya Mafuta hufanya nini na Risiti wanazobaki nazo?

Kwamba wakaguzi wa hesabu huchukua risiti ilimradi?

Risiti halali kwa mkaguzi ni ile yenye namba ya gari husika ya taasisi anayoikagua.

Hakuna namna ambayo unaweza kuchukua risiti iliyotolewa kwa ajili ya gari nyingine(na mara nyingi hazina namba za magari) halafu ukapeleka halmashauri fulani na udai ni ya gari la serikali au taasisi nyingine yeyote iliyo chini ya ukaguzi.
Uko nje ya muda ndugu.....
 
Wakuu kwema?

Nimeona sehemu nyingi kwenye Vituo vya Mafuta kuna watu wakishanunua mafuta huwa hawachukui risiti, unakuta ndoo za taka au mabox yamejaa risiti za kutosha tu.

Huwa zinafanyiwa nini? Wanazipeleka wapi? Kuna sehemu nilisikia kuwa ni dili, anayejua undani wa hili atujuze.

We jamaa unashangaza sana. Sijui ni kutokujua au upunguani wako. Risiti ni haki ya mteja. Ukinunua mafuta, chukua risit yako uondoke.

Wengi hawachukui risiti ndio maana zinabaki pale.

Na ukienda ukizihitaji za magumashi wanakuuzi tu. Sasa unamlaumu nani? Chukua risit yako uondoke kuondoa huo upuuzi, sio kuja kupiga kelele humu.

Mjini hapa, hata ukitaka muhuri wa Ikulu unapata.
 
HiO mashibe zipo connected automatic mafuta yakitoka lazima risiti itoke pia so wateja wengi hawapend kuchukua risti ndio maana zibabakia palepale shell kama inavooneka
Yani ni zimesetiwa automatic ukiweka mafuta lazima risiti itoke
 
Kama ulikuwa hujui hao wakaguzi ndio wanaoziagiza hizo risiti..,..

Basi kama kuna mkaguzi anaiamini risiti isiyo na utambulisho kwamba ni nani alikusudiwa kupewa, basi naye huyo mkaguzi ni wa mashaka.

Mfumo wa utoaji risiti vituoni huwa unaandika kiasi cha mafuta na fedha bila kuwekwa namba ya chombo husika.

Iwapo mteja anahitaji kuandikiwa namba ya chombo anatakiwa amtaarifu mtoa huduma.
 
HiO mashibe zipo connected automatic mafuta yakitoka lazima risiti itoke pia so wateja wengi hawapend kuchukua risti ndio maana zibabakia palepale shell kama inavooneka
Yani ni zimesetiwa automatic ukiweka mafuta lazima risiti itoke
Angalau wewe nimekuelewa.
 
Tuache unafiki km umeona zima maan ukijaza mafuta uwe unaomba risit yako unapewa sio unakuja humu kuandika unafiki

We unazani kla mtu ni mkuda na mnafiki km ww unauliza maswali ambayo majb yake unayo

Maisha ni rahisi sana dunian ila wanafiki km ww ndo usababisha maisha kua magumu kwa wenzako
 
unakuta ndoo za taka au mabox yamejaa risiti za kutosha tu.

Ukiziona kwenye ndio za taka ujue hazina kazi
 
Tuache unafiki km umeona zima maan ukijaza mafuta uwe unaomba risit yako unapewa sio unakuja humu kuandika unafiki

We unazani kla mtu ni mkuda na mnafiki km ww unauliza maswali ambayo majb yake unayo

Maisha ni rahisi sana dunian ila wanafiki km ww ndo usababisha maisha kua magumu kwa wenzako
Watu kama wewe ndio mnafanya wizi unaendelea na wengine kuishi kwa tabu. Mnakula majasho ya watu na hata hamuoni tatizo. Maisha yawe rahisi kwa kuminya wengine? Fanya kazi ya halali Mkuu
 
niliwahi kupata tunzo ya mfanyakazi bora wakati Fulani, nikapewa cheti na nikaambiwa niende kwa muhasibu kuna bahasha yangu pia.

Nilipoenda kwa muhasibu nikamuonyesha cheti, akanambia nenda kalete risiti ya kiasi fulani ata kama ni hamsini hamsini but make sure zinafika kiasi fulani cha fedha...

nikamuuliza ntazipata wap akanambia sheli, nikaenda sheli wakanipiga elfu5 nikachukua risiti zangu , nikapeleka kwa muhasibu nikapewa mkwanja wangu nkasepa...

So izo risiti ni deal šŸ’šŸ’
Noma sana... kuna mwenye biashara yake anabisha vikali
 
We jamaa unashangaza sana. Sijui ni kutokujua au upunguani wako. Risiti ni haki ya mteja. Ukinunua mafuta, chukua risit yako uondoke.
Wengi hawachukui risiti ndio maana zinabaki pale.
Na ukienda ukizihitaji za magumashi wanakuuzi tu. Sasa unamlaumu nani? Chukua risit yako uondoke kuondoa huo upuuzi, sio kuja kupiga kelele humu.
Mjini hapa, hata ukitaka muhuri wa Ikulu unapata.
Hii ndio shida ya kukurupuka. Kunywa maji upunguze mihemko kidogo kisha usome vizuri kilichoandikwa na urudi kwenye mada Mkuu
 
Hizo risiti ni dili sana kwa madereva wa serikali.
Ukipiga piga kwa mwezi hukosi milioni 1 ya bure.
Zinauzwa hizo
Hujui gari za serikali mafuta hutolewa kwa milage?
Hujui GPSA au vituo walivyoingia navyo ubia ndo pekee hufanya hivyo?
 
Hujui gari za serikali mafuta hutolewa kwa milage?
Hujui GPSA au vituo walivyoingia navyo ubia ndo pekee hufanya hivyo?
Najua kuwa kila gari ina account yake GSPA na kuna log book.
IlĆ  hizo risiti madereva wanakwenda kuzinunua zina kazi yake mkuu.
Labda kwenu TO mnoko hapo sawa ila jua tu bado kuna government drivers wana kazi nazo zile risiti
 
Lengo la kutoa risiti ni kulipa kodi kwa huduma inayotolewa, unapoweka mafuta na risiti ikatoka, uichukue usiichukue tayari Lengo husika limetimia.

Zile risiti zinazobaki pale nikwamba wateja hawakuzichukua na hazina kazi.

Ila tupo wazee wa retirement, ulipewa 100,000 ununue mafuta, unanunua ya 20,000 alafu unamuomba mtoa huduma akutafutie risiti ya 100,000. Unaweza kumpoza kwanzia 3000 kuendelea kwa usumbufu.

Mara nyingi hiyo biashara ya risiti hufanywa baina ya mtoa huduma na dereva, vituo vingi hawaruhusu hii biashara ya risiti
 
Kwamba wakaguzi wa hesabu huchukua risiti ilimradi?

Risiti halali kwa mkaguzi ni ile yenye namba ya gari husika ya taasisi anayoikagua.

Hakuna namna ambayo unaweza kuchukua risiti iliyotolewa kwa ajili ya gari nyingine(na mara nyingi hazina namba za magari) halafu ukapeleka halmashauri fulani na udai ni ya gari la serikali au taasisi nyingine yeyote iliyo chini ya ukaguzi.
Wakaguzi wa hesabu huwa wanafata ada,bati,nk na sio hayo makaratasi yako
 
Back
Top Bottom