Vituo vya utangazaji vyatakiwa kuomba kibali TCRA kurusha matangazo ya Vyombo vya Habari vya Nje

Vituo vya utangazaji vyatakiwa kuomba kibali TCRA kurusha matangazo ya Vyombo vya Habari vya Nje

Return Of Undertaker,
Magufuli ni mwoga kupitiliza, haijawahi kutokea huko nyuma. Anataka asifiwe tu na kila mtu hata Mungu kuna wanaompinga iweje kiumbe mortal kama yeye
 
Kwani huko YouTube
Kusema ukweli serikali ni wabaya sana.Mtu kuanzisha channel yake YouTube eti mpaka leseni utafikiri wao ndo wanamiliki youtube.
Kwani huko YouTube mkianzisha huwa hampati faida,

Mbona mna anzisha vichwa vya habali kisha ukiingia ndani unakuta kitu kingine na tayari mb zako zimekatwa,
Lipeni kodi nchi iendelee,

Unakuta mtu kaandika victorie kagongwa supper yaani ya draft, lakini ukiingia na mhemko kuona unakuta mambo mengine kabisa, hasara kabisa.

Wacha walipe leseni.
 
Maji hayazuowi kwa mkono.


ULIMWENGU huu wa Maendeleo ya sayansi na teknolojia huwez kuzuia taarifa.
 
Imagine mimi leo nianzishe page YouTube ya hata kufundisha tu biology let say. Eti lazima nipate leseni kutoka TCRA. Bando langu,muda wangu,YouTube wala sio ya serikali.
Yaani sisi wengine wenye akaunti za biashara Instagram pia nasikia tunatakiwa kujisajili.

Hivi ni kweli au
 
Hizi sheria za habari ni laana kubwa kwa Taifa.kama kuna mwana CCM anaona kinacho fanyika ni sahihi ahurumiwe.Na kama kweli hizi ndio mbinu tulizoona zina faa basi chama kimeangamia.

Narudia tena uchaguzi mwaka huu c lelemama.
anajimaliza, bado hawaoni kuwa Waatanzania si wajinga. Wametishwa miaka 5, lkn ya Singida, JNIA, ya DDM bado hawajashituka!
 
Bado kidogo internet zinazimwa! Zitafunguliwa baada ya kuapishwa Rais. Slowslow na HB hovyo kabisa.
 
Hata Marekani wanadhibiti kwa kasi sana, urusi pia, uhuru bila mipaka ni hatari kwa usalama wa nchi.Twende na JPM gari la uhakika

Mmeanza kuwaiga lini Marekani? Wao wana tume huru ya uchaguzi na rais wao anashitakiwa, mbona hamuigi hayo?
 
Yaani CCM na TCRA wameona vyombo vya habari vya ndani vikijiunga na vile vya nje kwa matangazo kuna uwezekano wa habari za mgombea wa upinzani ( Lissu) kupata airtime, sasa walichoamua kufanya ni kuwanyima watanzania haki yao ya kikatiba ya kupata habari ili wajinufaishe wao CCM kupitia hao vibaraka wao TCRA.

Hili linathibitisha ni kwa jinsi gani, CCM na taasisi zake walivyomstari wa mbele kukandamiza haki za raia wa nchi hii, ni wakati sasa wa kumuondoa huyu mkoloni mweusi na vibaraka wake wote.
Huo ni ujinga. Ina maana siku zote hizo vyombo vyetu vya habari vilikuwa vinavunja sheria za nchi? Kama ni hivyo basi Uongozi wa TCRA wawajibiske au wawajibishwe kwa kushindwa kusimamia vyombo vyetu vya habari. Watu wasipoangalia tutakuwa kama North Korea au China, hawa jamaa wanadhibiti mpaka maadmin wa WhatsApp utafikiri ni waajiriwa wao!
 
Back
Top Bottom