Vituo vya utangazaji vyatakiwa kuomba kibali TCRA kurusha matangazo ya Vyombo vya Habari vya Nje

Vituo vya utangazaji vyatakiwa kuomba kibali TCRA kurusha matangazo ya Vyombo vya Habari vya Nje

Hili la kuzuia hizi redio za majuu kuungana na local radio stations za hapa kusudi kuwanyima wapinzani jukwaa la kushushia nondo zao kwa utawala wa Magufuli naona kama ni kazi bure tu vile...
NI KWELI UNACHOSEMA ILA UJUE REDIO NYINGI ZA SIKU HIZI NI DIGITAL, NYINGI ZINA FM TU HAZINA SW.
 
Joka linazidi kupatika kabla halijafa.

Kazi tunayo
 
DW, BBC nasikia ni vyombo vinaisema vibaya sana serikali ya Mh. JPM, hasa DW ni pro upinzani 100% kwa Tanzania, pia mabeberu ni vyombo vyao hivyo, kwa maana hiyo niseme tusitegemee kabisa vyombo vyao vimtetee mtanzania wa kawaida, haaa ila tungekuwa na uwezo tungeifungia hata vyombo vya nje.. Haaaa 😅😅
 
Simu zetu zinashika redio za nje kupitia internet,tunapaswa kuwa na leseni pia?
 
Kingine wamesahau kuwa sikuhiz dunia iko kiganjani naweza soma chochote hata cha korea kaskazini
 
Kinachofanywa na TCRA ni uvunjaji wa katiba ya nchi, katiba imetamka habari hazina mipaka, wapinzani wanaongezewa hoja washindwe wenyewe
 
Inachokifanya serikali ni ushahidi kamili kuhusu kuminywa kwa uhuru wa kutoa maoni na vyombo vya habari.

Limeongelewa sana hili lkn serikali ilikuwa ikikataa.

Mfalme Juha ni mzigo.

Mithali 28:16
Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana
 
Nilisema ninasema na nitasema tena. Sioni namna magufuli atashinda uchaguzi wa mwaka huu. Nasema sioni. Watanzania hatujazoea haya. Hatujazoea kamwe!
 
Mpaka huyu mtu atoke madarakani sijui ni kanuni ngapi za ukandamizaji zitakuwa zimetungwa.

Kwa mtindo huu kutakuwepo na uchaguzi huru kama wanavyodai!!
 
Katika hali ya kushangaza na, vyombo vya habari ambavyo awali vilikuwa vinajiunga na vyombo vya nje kurusha matangazo sasa vimesitisha urushaji huo. Leo Radio One, Abood Radio na baadhi leo havijajiunga na vyombo hivyo vya kimataifa kurusha matangazo yao.

Hii inawezekana ni kutokana na mkwara wa TCRA ambao wameanza kwa kuichapa faini Radio One Stereo ya shilingi milioni 15. Hali inaanza kuwa mbaya sasa katika uhuru wa habari
 
Back
Top Bottom