Vivutio vya utalii Tanzania na faida za utalii wa ndani

6.Ziwa manyara.

Hifadhi hii ya Taifa ya Ziwa Manyara ni maarufu kwa Simba wanaopanda miti na lipo ndani ya hifadhi ambayo ina ndege wengi zaidi ya aina 400 wanaovutia wakiwemo ndege aina ya Korongo ambao huonekana kama pazia kubwa jeupe.


Idadi kubwa ya wanafunzi hapa nchi wanatembelea hifadhi hii na kujionea maajabu yaliyopo ambapo ni pamoja na kujionea wanyama kama Simba, Nyati, Tembo, Nyani, Chui, Pundamilia, na wanyama wengine wanaokula majani na wanaona chemichemi za maji moto yanayobubujika kutoka ardhini bila kukauka kwa mamilioni ya miaka.


Hifadhi hii ipo umbali wa kilomita 126 kutoka Arusha mjini, na wakati mzuri wa kutembelea hifadhi hii ni kuanzia mwezi June hadi Desemba.

 
7. Ruaha.
Hifadhi ya Ruaha ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania ambapo ina ukubwa wa kilomita za mraba 20,226 na ni ya pili kwa ukubwa katika Bara la Afrika baada ya hifadhi ya Kafue iliyopo nchini Zambia.


Ni maarufu kwa kuwa na wanyama aina ya Kudu wakubwa na wadogo ambao hupatikana kwa wingi ambapo hustawi wa hifadhi hii unategemea mto ruaha ambao aina mbalimbali za Samaki, Mamba na viboko hupatikana katika mto huu.


Wanyama kama Pofu na swala hunywa maji katika mto huo wa Ruaha ambao ni mawindo makubwa ya wanyama wakali wakiwemo Simba, Chui, Mbweha, Fisi na Mbwa mwitu. Pia eneo hili Tembo hukusanyika kwa wingi kuliko eneo lolote la hifadhi zilizopo katika nchi za Afrika Mashariki.


Katika hifadhi hii utajionea Magofu yanayosadikiwa kuwa yalikuwa makazi ya watu wa kale katika Kijiji cha Isimila kiasi cha Kilomita 120 kutoka Iringa. Magofu haya ni miongoni mwa historia ya kale barani Afrika.


Wakati mzuri wa kutembelea hifadhi hii ili kuangaliwa wanyama wakubwa ni wakati wa kiangazi kuanzia Mei hadi Desemba, lakini kuangalia ndege na maua wakati wa masika ni Januari –April .


 
8. Rubondo.


Hifadhi hii ya Taifa ni kisiwa ambacho kipo pembezoni mwa Ziwa Victoria, ziwa ambalo ni la pili kwa ukubwa duniani likiwa linazungukwa na nchi Tatu, Tanzania, Uganda na Kenya.


Kisiwa hiki kinaundwa na visiwa tisa vidogo vidogo ambapo kisiwa hiki cha Rubondo ni makazi na mazingira muafaka ya kuzaliana Samaki wakiwemo Sato na Sangara wenye ukubwa wa uzito wa kilo hadi 100.


Wanyama wanaopatikana katika hifadhi hiyo ni pamoja na Viboko,Pongo, Nzohe, Fisi maji, Mamba na Pimbi, wanabadilishana makazi na wanyama wengine waliohamishiwa katika hifadhi hii kama Sokwe, Tembo, Mbega weusi na weupe na Twiga.


Wakati mzuri wa kutembelea ni wa Kiangazi June-Agosti aidha wakati wa masika Novemba-Machi kwa ajili ya kuona maua na vipepeo na vile vile Desemba-Februari kwa kuwaona ndege wahamiaji.

Rubondo inajulikana pia kama JURASSIC ISLAND...
 
9.Saadani.

Hifadhi hii ipo ufukweni mwa bahari ya Hindi na ni hifadhi pekee Afrika Mashariki inayoungana na Bahari na ipo umbali wa Kilomita 100 kaskazini Magharibi mwa Dar es Salaam na umbali kama huo kusini Magharibi mwa bandari ya Tanga.


Ilianzishwa kama pori la akiba mwaka 1960 na ilitangazwa rasmi kuwa hifadhi ya Taifa mwaka 2005 na ukifika hapo unaweza kuona wanyama kama Simba, Chui, Fisi, Tumbili, swala na ngedere na mtalii mbali ya kuona wanyama pia unapata nafasi ya kuogelea na wakati wa kutembelea ni wakati wowote kwa mwaka ingawa wakati wa masika barabara zinaweza kutopitika kirahisi.


 
10. Udzungwa.

Hifadhi hii ya Milima ya Udzungwa ina hazina nyingi za mimea, ndege na wanyama ambao hazipatikani sehemu nyingine duniani.


Kati ya aina sita za jamii ya nyani wanapatikana katika hifadhi hii, mbili hupatikana katika hifadhi hii pekee; Mbega mwekundu wa Iringa (Iringa red colobus Monkey) na Sanje Crested mangabey’’ ambaye alikuwa hajulikani hadi mwaka 1979 na ndege mbalimbali.


Kivutio kikubwa zaidi ni Mto Sanje ambao unatoa maporomoko ya maji yenye urefu wa mita zipatazo 170 yakianguka kupitia msituni na kutua mithili ya mianzo ya ukungu bondeni.


 
11. Kitulo.

Awali hifadhi hii ilijulikana kwa jina la Elton Plateau baada ya Mvumbuzi Fredrick Elton kupia eneo hili mnamo mwaka 1870, mwaka 1960 Shirika la Chakula na Kilimo (FAO)ilichukua eneo hili kwa ajili ya ukulima wa ngano na ufugaji wa Kondoo.


Baadaye likageuzwa kuwa shamba la Ng’ombe ambalo lipo hadi leo. Mwaka 2005 Kitulo likatangazwa kuwa hifadhi ya Taifa na ni hifadhi ambayo ina maua aina mbalimbali na zaidi ya aina 30 hupatikana Kitulo pekee.


Pia ndiyo eneo pekee Tanzania ambapo ndege aina ya Tandawala machaka (Denhams Bustard) wana makazi na ndani ya hifadhi hii kuna miti aina ya Cidar yenye urefu wa zaidi ya mita 50 na inakadiliwa kuwa mirefu kuliko yote duniani.


Kitulo inafikiwa kwa gari kutoka Chimala kilomita 78 Mashariki mwa mji wa Mbeya. Reli ya TAZARA hupita karibu na hifadhi hii.


 
Naomba kuona ramani Nyerere national park
 
Hee!kumbe huu ni ubunifu😅
Aiseeh! jamaa kaja na wazo zuri sana. 😎 juzi hapa nilikuwa nafanya utalii wa ndani na mimi hususani katika wilaya ya RUNGWE, kiukweli hii wilaya imebarikiwa sana na yenyewe kwa vitu vingi. Changamoto nipale sisi wenyewe tumeshindwa kuvitangaza vivutio vyetu.

Ya laiti huu uzi nao siku zausoni ukawa na mwenendo mzuri kama wa walevi na wanywa pombe, tutaweza kufahamu vitu vingi sana.

Labda kwa uchache tu Rungwe Kuna ziwa Ngosi, kijungu, daraja la Mungu, water falls za aina tofauti tofauti, Msitu wa asili, mazao ya kilimo ya kila aina.
Rungwe pia ndio wilaya pekee ambayo msimu wa Parachichi duniani, upo katika kipindi ambacho hakuna nchi yeyote Duniani inayozalisha kwa wakati huo kuanzia mwezi 11 - 3.
 


Hivi ndo lile ziwa wanalosema watu huruhusiwi kuoga...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…