Vivutio vya utalii Tanzania na faida za utalii wa ndani

Vivutio vya utalii Tanzania na faida za utalii wa ndani

upload_2016-10-21_16-34-16.png

upload_2016-10-21_16-35-55.png

upload_2016-10-21_16-36-35.png

Kwa miaka mingi sasa sekta ya utalii nchini imeshindwa kuchangia pato la taifa kama inavyostahili. Kuna changamoto nyingi sana ambazo zimesababisha jambo hilo lakini naomba nitaje chache kisha na wenzangu mnaweza kuchangia na kuishauri serikali hatua za kuchukua ili kuimarisha sekta hii muhimu kwa ustawi wa uchumi wetu.

1. Sekta hii haijatangazwa ipasavyo ndani na nje ya nchi na serikali

2. Sekta hii imekumbatiwa na watu wachache na kupitia umoja wao wameifanya sekta hii kuwa kama mali yao binafsi na ni wao wanaoishauri serikali kuweka masharti magumu ili kuendelea kunufaika wao peke yao.

3. Kuna masharti magumu yanayokwaza wafanyabiashara wadogo kuingia kwenye sekta hii na hivyo kunufaisha wadau wachache

4. Miundo mbinu katika hifadhi zetu ni kikwazo katika kukuza biashara hii ya utalii

5. Vyuo vyetu vya utalii ni vichache vinatoa mafunzo duni yasiyoendana na ukuaji wa sekta hii na wahitimu wengi wanaomaliza kusoma wanakuwa na uwezo wa kufanya kazi za chini na zile nafasi kubwa kushikwa na wageni

6. Kutokuwepo kwa vivutio na mahoteli makubwa katika miji mikuu yenye hadhi ambayo ipo jirani na mbuga zetu za wanyama

7. Kutokuwepo au kutoboreshwa kwa maeneo yenye historia ya miji mbalimbali hapa nchini

8. Maonyesho ya utalii kutopewa kipaumbele na kufanywa katika mikoa miwili tu Kilimanjaro na Arusha

9. Kutokuwepo kwa taarifa za mara kwa mara kuhusu takwimu za watalii wanaoingia nchini na nchi wanazotoka zaidi ya kupatikana kwenye hotuba za waziri bungeni.

10. Ushiriki mdogo wa maonyesho ya utalii nje ambapo serikali haisaidii kuwawezesha wafanyabishara wadogo wa utalii kushiriki maonyesho haya

Nini kifanyike:

1. Serikali ijikite kwa nguvu zote kutangaza utalii katika mataifa mbalimbali ili kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea nchi zetu. Juhudi hizi ziende sambamba na kutoa mialiko maalum kwa watu maarufu duniani kutembelea vivutio vyetu na serikali kuchangia baadhi ya gharama na ziara hizo ziwekwe mwenye vyombo vya habari vya hapa nchini na nje.

2. Kuna fukuto la mgawanyiko katika umoja wa wafanyabiashara ya utalii kati ya wale wafanyabiashara wakubwa na wale wadogo. Na mgawanyiko huu unatokana na wafanyabishara wakubwa kutetea maslahi yao zaidi na kuwaacha wafanya bishara wadogo wakikosa pumzi. Serikali inatakiwa kutengeneza mazingira yatakayowawezesha wafanyabishara wa utalii kuwa na mazingira mazuri ya kufanya bishara zao bila kujali uwezo wao wa kimtaji, lakini pia kuwe na utaratibu wa kuwatambua wafanyabishara wanaouza safari kupitia mitandao ya kijamii na utaratibu huo iwe ni pamoja na kuwapatia leseni na utaratibu wa kulipa kodi, hii itasaidia serikali kuongeza mapato kwa ukusanyaji kodi kwani kwa miaka mingi sekta hii imekuwa ni kichaka cha wafanyabiashara wasio waaminifu kukwepa kodi kwa mbinu mbalimbali, Tunaweza kufanya utafiti kwa nchi kama Afrika Kusini na visiwa vya Mauritius na Shelisheli au Botswana ili kujua wenzetu wamewezaje kuboresha sekta ya utalii katika nchi zao na serikali inanufaikaje na mapato ya utalii katika nchi zao

3. Serikali ilegeze masharti ya kupata leseni za kuanzisha kampuni za utalii kwani siku hizi kuna aina nyingi za kuuza safari ambapo huduma nyingine zinaweza kufanywa na mtu mwingine kama huduma za ndege, huduma za magari kuna makampuni mengi ya kukodisha magari nk. Iwapo serikali itabadilisha masharti ya usajili wa makampuni ya utalii itaongeza wafanyabishara wengi katika sekta hiyo na hivyo kujiongezea kipato cha uhakika.

4. Tuna miundo mbinu mibovu sana katika vivutio vyetu vya utalii na mfano halisi ni ilipo mbuga ya Selous. Hii ni mbuga ambayo ingetumiwa na wageni wanaokuja jijini Dar kutembelea na kuona wanyama mbalimbali ukiwemo mto Rufiji. Hii ni mbuga ambayo ingeweza kutuingizia kipato kama kungetengenezwa mazingira ya kuwepo kwa Treni itakayokuwa inafanya safari zake hadi Kisaki na kurudi kila siku na pale kukawa na Hoteli kubwa na wawekezaji wa utalii wakapewa maeneo ya kujenga ofisi zao na kuboreshwa kwa barabara inayoingia Selous ingerahisisha watalii kutumia treni hadi Kisaki na pale wanapokelewa na kupelekwa mbugani na magari kwa kupitia barabara zilizoboreshwa. Naamini wageni wengi wanaoishi jijini Dar wangetumia fursa hii kutembelea Selous kila mwishoni mwa wiki. Kwa sasa njia ya usafiri wa gari unachukua saa kumi kupitia Matombo na saa 7 kupitia Rufiji ili kuingia mbugani huku ndege ndogo zikitumia dakika 45 lakini ni ghali sana watu wenye kipato cha kawaida kumudu. Serikali inaweza kuwashirikisha wadau wa utalii ili kupata mawazo yao namna nzuri ya kuboresha miundo mbinu yetu katika hifadhi zetu

5. Serikali iongeze vyuo vya utalii ikiwa ni pamoja na kuboresha mitaala ili kuinua elimu inayotolewa na vyuo hivyo. Kwa sasa vyuo vyetu vya utalii ni vichache na elimu inayotolewa humo ni ya kuwaandaa vijana wetu kuja kuwa vibarua na siyo kuwa viongozi katika sekta hiyo. Kwa sasa sekta ya utalii ndiyo inayoajiri wageni wengi kuliko sekta nyingine hapa nchini huku wengine wakiingia na kufanya kazi kiujanja. Tunahitaji mkakati makini ambao utaboresha elimu ya utalii kwa vijana wetu ili kupunguza ukosefu wa ajira. Zipo baadhi ya nafasi katika mahoteli yetu na makampuni ya utalii ili kuzishika labda ukapate elimu hiyo nje ya nchi au upate mafunzo kazini. Hii ni aibu kwa nchi yetu yenye vivutio vingi vya utalii kutegemea nguvu kazi kutoka nje huku vijana wetu wakiendelea kuwa vibarua

6. Tunahitaji katika mikoa ambayo iko karibu na vivutio waalikwe wawekezaji wa kuwekeza katika mahoteli na pia katika mikoa hiyo yatengwe maeneo ya historia ya makabila ya mkoa huo na maeneo mbalimbali yatengwe kwa ajili ya utalii na yaboreshwe ili watalii wanapokuja kabla ya kutembelea vivutio vyetu huko mbugani wapate fursa ya kujifunza utamaduni wa eneo husika na kujua asili ya eneo hilo na watu wake.

7. Serikali kwa kushirikiana na wadau wa utalii iboreshe maeneo yenye historia ya miji mbalimbali hapa nchini na kuitangaza ikiwemo ujenzi wa masanamu ya watu walioacha historia katika miji hiyo kama kule Tabora kina Mtemi Milambo au kina Kishosha Ng’wanamalundi

8. Kuwe na mkakati wa kutoa kipaumbele kwenye maonyesho ya utalii na yawe yanafanywa katika mikoa yote yenye vivutio ili kuimarisha utalii wa ndani hii iwe ni tofauti na ile ya kimataifa inayofanyika Arusha na Moshi, lakini hata hiyo ya Arusha na Moshi inapaswa kuboreshwa kwa kuiga wanavyofanya katika nchi za wenzetu

9. Taarifa za mara kwa mara kuhusu takwimu za watalii wanaoingia nchini na nchi wanazotoka ni muhimu ili kuwarahisishia wafanyabishara wa utalii kujua soko liko wapi, uwepo wa kitengo kitakachokuwa kinakusanya taarifa hizo na kuziweka mtandaoni kutasaidia kujua ni wapi tumejitangaza na wapi hatujajitangaza ili kuelekeza nguvu zetu huko.

10. Kuwe na mkakati wa kuhakikisha wafanyabishara wa utalii wanashiriki kwa wingi kwenye maonyesho ya utalii katika nchi mbalimbali ili kupata fursa ya kutangaza vivutio vyetu.

Naomba nipishe michango mingine kutoka kwa wadau mbalimbali ili tuweze kuishauri serikali namna nzuri ya kuboresha sekta hii ya utalii.

TOVUTI MBALIMBALI ZINAZOHUSU UTALII NCHINI

Tovuti Kuu ya Serikali: Watoa huduma za Utalii

National College of Tourism (NCT) | Tanzania

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Tovuti Kuu ya Serikali: Utalii

....
  1. kujenga hovyo hovyo mahoteli ndani ya hifadhi bila kutumia EIA
  2. vijiji kuziba ushoroba (Mapito ya wanyama) mfano Tarangire Manyara Selela Esimongori...Arusha National park -Sinya -Amboseli
  3. siasa kushamiri maeneo ya hifadhi
  4. Tour guides kulipwa chini ya viwango
  5. wapambanaji mstari wa mbele tour guides Tour leader kutoshirikishwa kama wadau MUHIMU katika sekta hii
  6. kutokuwepo kwa kituo maalum cha kuwapeleka watalii mfano Tanzania visitors Center
  7. kodi za viwanja vya ndege kuwa juu
  8. sekta zenye mahusiano na utalii kufanya kazi kwa kujitenga
  9. kutowapa mafunzo maalum waongoza Watalii ya kutangaza utalii na vivutio muhimu Tanzania
  10. kutokuwa na watu professinal waliobobea katika biashara ya utalii huku Ng'ambo balozini
  11. kutokuwa na mtandao wa pamoja wa wadau wote wa utalii utakao zungumzia changamoto na kuzitatua
ntakuja baadae wacha nikale mtada na togwaulaya
 
I Concur and support the thread...

TATO is dead or sleeping deep sleep

TATO wanacharge Flat rate Membership fee, This is very wrong......

TATO ni wavivu, hawataki kujifunza South Africa Association of Tour Operators au KATO ya Kenya...hawa wana categories katika membership

TALA License Flat rate fee n Wrong

Makampuni Makubwa kama Ranger Safaris, Thompson Safaris, Kudu, A & K, Leopard Tours, Zara Travel....wana magari zaidi ya 200, wana wageni zaidi ya 10000 kwa mwaka...How comes walipe TALA License ya 2000 $ sawa na Tour Operator Ndogo

Tour Operator Ndogo wanatakiwa walipe TALA License 1000 $ ili waweze kumudu ushindani na ili wakue...

Tour OPerator Ndogo ni za Wazawa na zinaajiri wazawa....uchumi wa Tanzania unarudi Tanzania

Watanzania wengi wakiingia katika biashara ya utalii, nchi itaingiza FOREX nyingi na pato la utalii litaongezeka kwa serikali

Utitiri wa Kodi...Inatakiwa Serikali iweke kodi moja kwa Tour Operator..yaani kuwe na Kodi moja jumuishi.

Hii Kodi moja ni rahisi kuifuatilia na ukwepaji wa kodi hautakuwepo
 
Mara kadhaa nimejaribu kutumia namba za simu zilizopo kwenye website ya TANAPA ili kuweza kuwasiliana na maafisa wa TANAPA waliopo katika baadhi ya hifadhi ili kupata maelekezo ya kuwezesha kufanya maamuzi fulani lakini unakuta hizi namba hazipatikani.

Sasa kwa taasisi ambayo ilitakiwa iweze kuwa na urahisi wa mawasiliano na wadau wake hili ni tatizo kubwa.

Pia kwa utaliii wa ndani bado hakujawa na hamasa ya kuamsha ari ya Watanzania kufika kwenye hizi hifadhi.

Wengi huchukulia utalii ni jambo la matajiri na wageni kutoka nje.
 
Sijakuelewa mkuu, sijui unamaanisha nini hapo
Wewe ndo afisa mawasiliano wa tourism industry?
Kama ndiyo, basi Idaara ya maliasili ina budget ya kugharamia kupata taarifa na kero na maoni za wateja, itumie kulipia hii thread then JF mod wapin juu.
 
Mimi ni mwananchi wa kawaida na nimetumia uhuru wangu kuishauri serikali na nikaona ni vyema niwashirikishe na wengine
 
ILI KUWEKA KUMBU KUMBU SAWA:

SEHEMU NDOGO YA HOTUBA YA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MHESHIMIWA PROF. JUMANNE ABDALLAH MAGHEMBE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KWA MWAKA 2016/2017

Sekta ndogo ya Utalii 26.

Mheshimiwa Spika,

Sekta ndogo ya Utalii imeshika nafasi ya kwanza katika kuliingizia Taifa fedha za kigeni kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo (2012 – 2015). Fedha hizo ni sawa na wastani wa Dola za Kimarekani milioni 2,002 kwa mwaka ambayo ni asilimia 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni nchini. Kwa mwaka 2015, idadi ya watalii waliongia nchini ilikuwa 1,102,619. Sekta huchangia takriban ajira 500,000 za moja kwa moja na ajira 1,000,000 ambazo si za moja kwa moja. Aidha, Sekta imeendelea kutoa ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi katika Sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, elimu, mawasiliano, miundombinu, burudani, usafirishaji na uzalishaji wa bidhaa na huduma kwa watalii. Maendeleo ya Sekta ya utalii nchini yamechangiwa na uwepo wa amani na utulivu; ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano; uboreshwaji wa miundombinu; na ubora wa huduma za malazi na ukarimu. Vivutio vikuu vya Utalii wa Tanzania ni wanyamapori, upandaji milima, utamaduni, malikale, mandhari na fukwe.

27.
Mheshimiwa Spika,

Sekta ya utalii inakabiliwa na changamoto ya kutokuwa ya miundombinu bora katika maeneo yenye vivutio ikiwemo
huduma za maji, umeme na barabara. Aidha, hatuna Shirika la Ndege lenye uwezo wa kuleta watalii moja kwa moja kutoka katika nchi ambazo ni masoko makuu ya utalii. Hivyo, Wizara inaishukuru Serikali kwa mpango wa kununua ndege tatu katika mwaka ujao wa fedha ili kukidhi haja hii katika kipindi cha mpito wakati Serikali ikiimarisha Shirika la ndege la Taifa.

28.
Mheshimiwa Spika,

matumizi ya kadi za kielektroniki kuingia katika maeneo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya utalii yanakabiliwa na changamoto ikiwemo baadhi ya wageni kutokuwa na uelewa wa njia hiyo ya malipo. Teknolojia hii inahitaji uwepo wa mtandao wa intaneti katika maeneo yote ambayo ulipaji unafanyika. Ili kukabili changamoto hizo, Wizara inaendelea kutoa elimu kwa wageni kuhusu huduma hiyo ambayo haihitaji matumizi ya fedha taslimu. Wizara inawekeza katika kuimarisha miundombinu za ulipaji wa mfumo wa mtandao kwa kununua
satellite dishes na communication boosters.
Vilevile, inawasiliana na watoa huduma za kibenki ili kuhakikisha kwamba huduma za mfumo wa ulipaji kwa mtandao zinapatikana katika maeneo ya hifadhi.

29.
Mheshimiwa Spika,

upo mwamko mdogo wa wananchi katika kutembelea vivutio vya utalii pamoja na kushiriki katika biashara za utalii pamoja na Serikali kuweka gharama ndogo za viingilio katika Hifadhi za Taifa kwa Watanzania na raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa sasa, kiingilio ni shilingi 10,000 kwa Hifadhi zilizopo Kaskazini; shilingi 5,000 hadi 15,000 kwa Hifadhi zilizopo Kusini; na watoto shilingi 2,000 kwa Hifadhi zote nchini. Magari madogo hutozwa shilingi 20,000 katika hifadhi zote. Katika kukabiliana na changamoto hii, Wizara itaendeleza kampeni mbalimbali za kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za utalii. Aidha, Wizara imebaini kuwa, Sekta ya Utalii haijawekwa katika vipaumbele kwenye mipango ya maendeleo ya Mikoa na Wilaya. Katika kukabiliana na hili, Wizara itatoa elimu ya uhamasishaji kwa wadau na watoa maamuzi mbalimbali ili sekta hii ipewe kipaumbele stahili katika mipango ya maendeleo ya Taifa, Mikoa na Wilaya.

30.
Mheshimiwa Spika,

kuna ugumu wa kupata mitaji ya uhakika kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati ili kuendesha biashara za utalii. Ugumu huo unatokana na riba kubwa zinazotozwa na Benki za Biashara. Ili kukabiliana na changamoto hii, Wizara itaendelea kushawishi taasisi za fedha kuona fursa ya kufanya biashara na wafanyabiashara wadogo na wa kati katika biashara za utalii. Aidha, ipo changamoto ya miundombinu ya kuwezesha malipo kwa kutumia
credit card ambayo watalii wengi huitumia kulipia huduma mbalimbali.

31.
Mheshimiwa Spika,

changamoto nyingine ni kutokuwa na ardhi iliyotengwa kwa ajili ya kuendeleza utalii nchini. Wizara itaendelea kuzishawishi Mamlaka za Ardhi na Mipango Miji katika Halmashauri zetu kutenga maeneo maalum kwa ajili ya uwekezaji wa shughuli za utalii na kuhamasisha wananchi wanaomiliki ardhi kuingia ubia na wawekezaji wa utalii ili kutumia ardhi yao katika maendeleo ya sekta ya utalii.

32.
Mheshimiwa Spika,

upo uhaba wa wafanyakazi wenye ujuzi na utaalamu katika sekta ya utalii na hoteli. Ili kukabiliana na changamoto hii, Wizara imeanzisha Wakala wa Chuo cha Utalii cha Taifa na kuhamasisha sekta binafsi kuanzisha vyuo vyake. Aidha, itawaendeleza watumishi kitaaluma kwa kuwapa mafunzo stahili ili kuboresha utendaji kazi na kuongeza tija. Vilevile, Wizara itaendelea kujenga ushirikiano wa karibu baina ya Sekta ya Utalii na sekta nyingine za uchumi na uzalishaji kama

33.
Mheshimiwa Spika,

ili kuongeza ajira na mapato ya utalii, sekta nyingine wanashauriwa kutoa huduma na bidhaa zenye viwango kwa uwingi na kwa wakati unaohitajika katika soko la utalii. Aidha, wawekezaji katika sekta ya utalii waendelee kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini katika uwekezaji na utoaji huduma kwa wageni. Wizara itaendelea kuunga mkono jitihada za kujenga mazingira ya ustawi wa viwanda kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwa wingi na ubora unaohitajika katika sekta ya utalii.
 
I Concur and support the thread...

TATO is dead or sleeping deep sleep

TATO wanacharge Flat rate Membership fee, This is very wrong......

TATO ni wavivu, hawataki kujifunza South Africa Association of Tour Operators au KATO ya Kenya...hawa wana categories katika membership

TALA License Flat rate fee n Wrong

Makampuni Makubwa kama Ranger Safaris, Thompson Safaris, Kudu, A & K, Leopard Tours, Zara Travel....wana magari zaidi ya 200, wana wageni zaidi ya 10000 kwa mwaka...How comes walipe TALA License ya 2000 $ sawa na Tour Operator Ndogo

Tour Operator Ndogo wanatakiwa walipe TALA License 1000 $ ili waweze kumudu ushindani na ili wakue...

Tour OPerator Ndogo ni za Wazawa na zinaajiri wazawa....uchumi wa Tanzania unarudi Tanzania

Watanzania wengi wakiingia katika biashara ya utalii, nchi itaingiza FOREX nyingi na pato la utalii litaongezeka kwa serikali

Utitiri wa Kodi...Inatakiwa Serikali iweke kodi moja kwa Tour Operator..yaani kuwe na Kodi moja jumuishi.

Hii Kodi moja ni rahisi kuifuatilia na ukwepaji wa kodi hautakuwepo
...
.....TATO imejaa wazungu na wahindi usitegemee sana kuyabeba makampuni ya hapa nyumbani
 
Lipeni kodi stahiki. Kila siku hoteli zimejaa ila kodi hakuna. Watalii wengi mchango wenu pato la taifa kiduchu.
 
Mmoja wa member wa JF ambaye uwa nawakubali hata kama tukitofautiana mitazamo.

Ushauri wako mzuri nadhani wahusika wanapita humu ukumbini kusoma habari.

Kingine muda ukikuruhusu tuletee habari zetu zile za kesi tata duniani na hukumu za mahakama.
 
Mara kadhaa nimejaribu kutumia namba za simu zilizopo kwenye website ya TANAPA ili kuweza kuwasiliana na maafisa wa TANAPA waliopo katika baadhi ya hifadhi ili kupata maelekezo ya kuwezesha kufanya maamuzi fulani lakini unakuta hizi namba hazipatikani.

Sasa kwa taasisi ambayo ilitakiwa iweze kuwa na urahisi wa mawasiliano na wadau wake hili ni tatizo kubwa.

Pia kwa utaliii wa ndani bado hakujawa na hamasa ya kuamsha ari ya Watanzania kufika kwenye hizi hifadhi.

Wengi huchukulia utalii ni jambo la matajiri na wageni kutoka nje.
....
.....nilijifunza kitu Sustainable Tourism kule Namibia wenzetu wako mbali sana haswa utalii wa ndani

mfano tu Serengeti au Ngorongoro kwa mbongo ni vigumu sana kufika huko zaidi ya kulala kwenye mabweni.....

nahakika Tanapa or NCCA wakitengeneza mazingira mazuri mfano zijengwe Lodge za Watanzania ndani ya hifadhi kwa 30,000 mpaka 40000 tsh per day bia bei ya kitaa na chakula ....usafiri wa basi mayai special kwa wabongo ...ndani ya hifadhi kuwe na malori maalum ya kuvinjari....na hakika watu watamiminika kama mvua...

cha msingi kuweka mazingira yanayofanana na utamaduni wetu .....watu tutakwenda
 
Mmoja wa member wa JF ambaye uwa nawakubali hata kama tukitofautiana mitazamo.

Ushauri wako mzuri nadhani wahusika wanapita humu ukumbini kusoma habari.

Kingine muda ukikuruhusu tuletee habari zetu zile za kesi tata duniani na hukumu za mahakama.
....
.....Mnama tembelea hata Saadani National Park na familia ni rahisi sana kwa wakazi wa Dar
 
Mmoja wa member wa JF ambaye uwa nawakubali hata kama tukitofautiana mitazamo.

Ushauri wako mzuri nadhani wahusika wanapita humu ukumbini kusoma habari.

Kingine muda ukikuruhusu tuletee habari zetu zile za kesi tata duniani na hukumu za mahakama.
Mkuu

Mkuu nashukuru kwa heshima uliyonipa kuhusu kesi kwa sasa niko kwenye mchakato wa kutoa kitabu, nitawajulisha kikitoka.
Kuhusu mada husika natarajia pia mchango wako hapa.
 
Hii sekta nina hasira nayo sana...

Kiufupi Ujinga wa kwanza ambayo ni mistake kubwa sana ... Hii sekta imeshikiliwa na wahindi .. Na wageni ndio wenye mahoteli ndio wengi wao wana makampuni ya kiutalii..
Unategemea nini?

Huku ukija serikalini viongozi wetu ni wachumia matumbo wala rushwa wakubwa.
 
....
.....nilijifunza kitu Sustainable Tourism kule Namibia wenzetu wako mbali sana haswa utalii wa ndani

mfano tu Serengeti au Ngorongoro kwa mbongo ni vigumu sana kufika huko zaidi ya kulala kwenye mabweni.....

nahakika Tanapa or NCCA wakitengeneza mazingira mazuri mfano zijengwe Lodge za Watanzania ndani ya hifadhi kwa 30,000 mpaka 40000 tsh per day bia bei ya kitaa na chakula ....usafiri wa basi mayai special kwa wabongo ...ndani ya hifadhi kuwe na malori maalum ya kuvinjari....na hakika watu watamiminika kama mvua...

cha msingi kuweka mazingira yanayofanana na utamaduni wetu .....watu tutakwenda
Unachosema ni kweli kabisa.
kwa hali ya sasa ukimwambia mtu wa kwamba anaweza enda talii ngorongoro au Serengeti anaona kama ni jambo la watu matajiri tu na si la watu wa kada ya kawaida.

Hakujawa na hali rafiki.

Pia kuna siku nilikuwa katika hifadhi mojawapo hapa nchini, likaja kundi la watu wakiwa wamekodi gari kufika pale ofisi ya TANAPA wakawa wanataka kufanya malipo ya kuzuru ile mbuga na kulipia gari lililowaleta.

Sasa shida ikawa wao wana pesa taslim mkononi lakini maafisa wa TANAPA wanawaambia wanatakiwa wawe na kadi ya CRDB kufanya malipo. Wale jamaa walijikuta safari yao imevurugika wa kukosa mtu mwenye account CRDB.

Yote hii ni kutokana na kutokutoa taarifa pale wanapofanya mabadiliko au maboresho kwa huduma zao (TANAPA/Wizara).
 
Hii sekta nina hasira nayo sana...
Kiufupi Ujinga wa kwanza ambayo ni mistake kubwa sana ... Hii sekta imeshikiliwa na wahindi .. Na wageni ndio wenye mahoteli ndio wengi wao wana makampuni ya kiutalii..
Unategemea nini?
Huku ukija serikalini viongozi wetu ni wachumia matumbo wala rushwa wakubwa.
.....
......mifuko ya jamii kama NSSF wangewekeza huko kwaajili ya wazawa haswa mahoteli ....ili wabongo angalau waonye matunda
 
Back
Top Bottom