Vivutio vya utalii Tanzania na faida za utalii wa ndani

Vivutio vya utalii Tanzania na faida za utalii wa ndani

Mtambuzi utalii ni muhimu lkn zile kesi za kina mkwizu nazo muhim sana ebu fanya kuzileta maana tumezimis sana
 
Big up mtambuzi.. Thread positive kama hizi ndo nazipendaa...Sio mtu anatukana kwa kisingizio cha kushaurii. Nani atasikiliza mawazo ya mtu anayetoa mapopu
 
View attachment 421962

View attachment 421964

View attachment 421965

Kwa miaka mingi sasa sekta ya utalii nchini imeshindwa kuchangia pato la taifa kama inavyostahili. Kuna changamoto nyingi sana ambazo zimesababisha jambo hilo lakini naomba nitaje chache kisha na wenzangu mnaweza kuchangia na kuishauri serikali hatua za kuchukua ili kuimarisha sekta hii muhimu kwa ustawi wa uchumi wetu.

1. Sekta hii haijatangazwa ipasavyo ndani na nje ya nchi na serikali

2. Sekta hii imekumbatiwa na watu wachache na kupitia umoja wao wameifanya sekta hii kuwa kama mali yao binafsi na ni wao wanaoishauri serikali kuweka masharti magumu ili kuendelea kunufaika wao peke yao.

3. Kuna masharti magumu yanayokwaza wafanyabiashara wadogo kuingia kwenye sekta hii na hivyo kunufaisha wadau wachache

4. Miundo mbinu katika hifadhi zetu ni kikwazo katika kukuza biashara hii ya utalii

5. Vyuo vyetu vya utalii ni vichache vinatoa mafunzo duni yasiyoendana na ukuaji wa sekta hii na wahitimu wengi wanaomaliza kusoma wanakuwa na uwezo wa kufanya kazi za chini na zile nafasi kubwa kushikwa na wageni

6. Kutokuwepo kwa vivutio na mahoteli makubwa katika miji mikuu yenye hadhi ambayo ipo jirani na mbuga zetu za wanyama

7. Kutokuwepo au kutoboreshwa kwa maeneo yenye historia ya miji mbalimbali hapa nchini

8. Maonyesho ya utalii kutopewa kipaumbele na kufanywa katika mikoa miwili tu Kilimanjaro na Arusha

9. Kutokuwepo kwa taarifa za mara kwa mara kuhusu takwimu za watalii wanaoingia nchini na nchi wanazotoka zaidi ya kupatikana kwenye hotuba za waziri bungeni.

10. Ushiriki mdogo wa maonyesho ya utalii nje ambapo serikali haisaidii kuwawezesha wafanyabishara wadogo wa utalii kushiriki maonyesho haya

Nini kifanyike:

1. Serikali ijikite kwa nguvu zote kutangaza utalii katika mataifa mbalimbali ili kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea nchi zetu. Juhudi hizi ziende sambamba na kutoa mialiko maalum kwa watu maarufu duniani kutembelea vivutio vyetu na serikali kuchangia baadhi ya gharama na ziara hizo ziwekwe mwenye vyombo vya habari vya hapa nchini na nje.

2. Kuna fukuto la mgawanyiko katika umoja wa wafanyabiashara ya utalii kati ya wale wafanyabiashara wakubwa na wale wadogo. Na mgawanyiko huu unatokana na wafanyabishara wakubwa kutetea maslahi yao zaidi na kuwaacha wafanya bishara wadogo wakikosa pumzi. Serikali inatakiwa kutengeneza mazingira yatakayowawezesha wafanyabishara wa utalii kuwa na mazingira mazuri ya kufanya bishara zao bila kujali uwezo wao wa kimtaji, lakini pia kuwe na utaratibu wa kuwatambua wafanyabishara wanaouza safari kupitia mitandao ya kijamii na utaratibu huo iwe ni pamoja na kuwapatia leseni na utaratibu wa kulipa kodi, hii itasaidia serikali kuongeza mapato kwa ukusanyaji kodi kwani kwa miaka mingi sekta hii imekuwa ni kichaka cha wafanyabiashara wasio waaminifu kukwepa kodi kwa mbinu mbalimbali, Tunaweza kufanya utafiti kwa nchi kama Afrika Kusini na visiwa vya Mauritius na Shelisheli au Botswana ili kujua wenzetu wamewezaje kuboresha sekta ya utalii katika nchi zao na serikali inanufaikaje na mapato ya utalii katika nchi zao

3. Serikali ilegeze masharti ya kupata leseni za kuanzisha kampuni za utalii kwani siku hizi kuna aina nyingi za kuuza safari ambapo huduma nyingine zinaweza kufanywa na mtu mwingine kama huduma za ndege, huduma za magari kuna makampuni mengi ya kukodisha magari nk. Iwapo serikali itabadilisha masharti ya usajili wa makampuni ya utalii itaongeza wafanyabishara wengi katika sekta hiyo na hivyo kujiongezea kipato cha uhakika.

4. Tuna miundo mbinu mibovu sana katika vivutio vyetu vya utalii na mfano halisi ni ilipo mbuga ya Selous. Hii ni mbuga ambayo ingetumiwa na wageni wanaokuja jijini Dar kutembelea na kuona wanyama mbalimbali ukiwemo mto Rufiji. Hii ni mbuga ambayo ingeweza kutuingizia kipato kama kungetengenezwa mazingira ya kuwepo kwa Treni itakayokuwa inafanya safari zake hadi Kisaki na kurudi kila siku na pale kukawa na Hoteli kubwa na wawekezaji wa utalii wakapewa maeneo ya kujenga ofisi zao na kuboreshwa kwa barabara inayoingia Selous ingerahisisha watalii kutumia treni hadi Kisaki na pale wanapokelewa na kupelekwa mbugani na magari kwa kupitia barabara zilizoboreshwa. Naamini wageni wengi wanaoishi jijini Dar wangetumia fursa hii kutembelea Selous kila mwishoni mwa wiki. Kwa sasa njia ya usafiri wa gari unachukua saa kumi kupitia Matombo na saa 7 kupitia Rufiji ili kuingia mbugani huku ndege ndogo zikitumia dakika 45 lakini ni ghali sana watu wenye kipato cha kawaida kumudu. Serikali inaweza kuwashirikisha wadau wa utalii ili kupata mawazo yao namna nzuri ya kuboresha miundo mbinu yetu katika hifadhi zetu

5. Serikali iongeze vyuo vya utalii ikiwa ni pamoja na kuboresha mitaala ili kuinua elimu inayotolewa na vyuo hivyo. Kwa sasa vyuo vyetu vya utalii ni vichache na elimu inayotolewa humo ni ya kuwaandaa vijana wetu kuja kuwa vibarua na siyo kuwa viongozi katika sekta hiyo. Kwa sasa sekta ya utalii ndiyo inayoajiri wageni wengi kuliko sekta nyingine hapa nchini huku wengine wakiingia na kufanya kazi kiujanja. Tunahitaji mkakati makini ambao utaboresha elimu ya utalii kwa vijana wetu ili kupunguza ukosefu wa ajira. Zipo baadhi ya nafasi katika mahoteli yetu na makampuni ya utalii ili kuzishika labda ukapate elimu hiyo nje ya nchi au upate mafunzo kazini. Hii ni aibu kwa nchi yetu yenye vivutio vingi vya utalii kutegemea nguvu kazi kutoka nje huku vijana wetu wakiendelea kuwa vibarua

6. Tunahitaji katika mikoa ambayo iko karibu na vivutio waalikwe wawekezaji wa kuwekeza katika mahoteli na pia katika mikoa hiyo yatengwe maeneo ya historia ya makabila ya mkoa huo na maeneo mbalimbali yatengwe kwa ajili ya utalii na yaboreshwe ili watalii wanapokuja kabla ya kutembelea vivutio vyetu huko mbugani wapate fursa ya kujifunza utamaduni wa eneo husika na kujua asili ya eneo hilo na watu wake.

7. Serikali kwa kushirikiana na wadau wa utalii iboreshe maeneo yenye historia ya miji mbalimbali hapa nchini na kuitangaza ikiwemo ujenzi wa masanamu ya watu walioacha historia katika miji hiyo kama kule Tabora kina Mtemi Milambo au kina Kishosha Ng’wanamalundi

8. Kuwe na mkakati wa kutoa kipaumbele kwenye maonyesho ya utalii na yawe yanafanywa katika mikoa yote yenye vivutio ili kuimarisha utalii wa ndani hii iwe ni tofauti na ile ya kimataifa inayofanyika Arusha na Moshi, lakini hata hiyo ya Arusha na Moshi inapaswa kuboreshwa kwa kuiga wanavyofanya katika nchi za wenzetu

9. Taarifa za mara kwa mara kuhusu takwimu za watalii wanaoingia nchini na nchi wanazotoka ni muhimu ili kuwarahisishia wafanyabishara wa utalii kujua soko liko wapi, uwepo wa kitengo kitakachokuwa kinakusanya taarifa hizo na kuziweka mtandaoni kutasaidia kujua ni wapi tumejitangaza na wapi hatujajitangaza ili kuelekeza nguvu zetu huko.

10. Kuwe na mkakati wa kuhakikisha wafanyabishara wa utalii wanashiriki kwa wingi kwenye maonyesho ya utalii katika nchi mbalimbali ili kupata fursa ya kutangaza vivutio vyetu.

Naomba nipishe michango mingine kutoka kwa wadau mbalimbali ili tuweze kuishauri serikali namna nzuri ya kuboresha sekta hii ya utalii.

TOVUTI MBALIMBALI ZINAZOHUSU UTALII NCHINI

Tovuti Kuu ya Serikali: Watoa huduma za Utalii

National College of Tourism (NCT) | Tanzania

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Tovuti Kuu ya Serikali: Utalii

Nakubaliana na hoja zako isipokuwa namba 1 na 5.

Kuhusu hoja #1: Mpaka sasa sijaona assessment yoyote ikionesha impact ya uwekezaji ambao tumeshaufanya katika matangazo ya vivutio vya utalii nchini. Bila kuona hiyo assessment, siwezi ku-support uwekezaji zaidi kwenye matangazo. Huo ni uchochoro wa kuiba hela. Ni nini impact ya kuweka matangazo kwenye viwanja vya EPL? Je watalii wanaokuja nchini wanafanya hivyo kwa kushawishiwa na matangazo? Wanapata wapi habari kuhusu vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania? Unaweza kukuta matangazo tunayolipia mamilioni hayana impact yoyote. Tunafanya mambo kwa mazoea kwa kuwa lengo ni kuiba. Na nahisi kwenye eneo hili tumeibiwa sana. Safari za nje kuhudhuria maonesho ya utalii zimefanyika kiholela sana. Kusema tu serikali ijikite kwa nguvu zote kutangaza utalii ni kutengeneza mazingira ya fedha za umma kuibiwa. Ni lazima kuwa specific na kufanya mambo kwa tija.

Kuhusu hoja #5: Wingi wa vyuo hautatatua tatizo. Actually, utaongeza tatizo kwa kuzalisha utitiri wa watu wasio na sifa. Kinachokosekana ni apprenticeship programs pamoja na certification program. Ili kuwa guide, ni lazima uwe certified kama ambavyo NBAA ina certify wahasibu. Huo utaratibu haupo. Matokeo yake, watu wakifeli shule wanakimbilia kuwa tour guide. Huo ni mfano tu but the same applies to hoteliers, travel agents etc. Biashara ya utalii ni delicate sana. Mgeni akipata experience mbaya, athari ni kubwa. Mtu alipe maelfu ya dola halafu anapata guide mediocre, wanakuwa disappointed sana. Na magaidi wengi ni ujanja ujanja tu. Very few are qualified.
 
Kuna changamoto nyingine imeanza hivi karibuni ile ya wafugaji kuvamia na kuingiza mifugo yao katika hifadhi bila ya kufuata utaratibu. Suala hili lisiporatibiwa linaongeza ushindani wa malisho na uwezekano wa maambukizo ya magonjwa kwa wanyama pori. Inabidi serikali na wadau wakae na kutatua changamoto hii. Ikiwezekana watumie utaratibu unaotumika Ngorongoro (NCA).
 
hii ndo post ya maana kuliko zote ambazo nimewahi kuzikuta hapa jamii forums, sababu imejitosheleza vya kutosha.
Ngoja nichafue hali ya hewa.. Members wenye zaidi ya 5 years humu ni ngumu kukuta wameandika pumba. Lakini mtu kajiunga June 2016 ana posti 5000 inamaanza kwa mwezi anatuma post zaidi ya book na per day anatuma post zaidi ya 30 ujue huyo ni kimeo. Kuandika content inahitaji tafakuri na lazima uwe ni msomaji mzuri wa vitu vyenye content ili uwe muandishi mzuri...😀😀😀😀
 
Utalii wa Ndani nilishatembelea Ngorongoro, Pazuri sana Manyara kama tulibaniwa hatukuweza fika ziwani ila tulilala hostel na Tarangire tulitalii ila tulibaniwa pia hatukuweza fika chemchem ya maji ya moto hivyo kiufupi sikupapenda ilikuwa Mwaka elfu moja mia tisa na tisini na tano.

Ngorongoro tulitelemka na gari moja matata four wheel drive umbo lake kama la lile bus lililotumika kwenye movie ya War bus langi ya green. tulizungunga na tuliweza teremka tukaona viboko,Simba,Tembo,Nyati Swala na wanyama wengi Kifaru hatukumuona kudadeki bila kusahahu Masai..

Safarini niliweza kuona Mazao ya Sunflower maeneo ya Karatu niliweza kuwa level moja na Mawingu yana kiubaridi ila yapo kama Moshi(Ukungu) kihewa kizito kizito hivi

tulifika Snake park tukaona Nyoka wa aina mbali mbali Na Ngamia pia

Pale Momera Kwa Dr. Nagi Tanzanite kuna wanyama ila pamechoka.

Sina Deni kubwa kwa Serikali kuhusu Utalii wa Ndani Bado Mikumi japo nilishawahi pita kwa Treni na wanyama niliwaona... Kusini pia bado kwa kina Livingstone nakobado sijafika... Kilipoanguka Kimondo napo sijawahi fika japo Mbeya nilishawahi fika lol
 
Hongera mkuu na ninaamini ipo siku utatembelea vivutio vingine, tutumie jukwaa hili kuishauri serikali namna ya kuboresha sekta hii ili wazawa nao wapate fursa ya kutembelea na kufaidi mema ya nchi
 
Nakubaliana na hoja zako isipokuwa namba 1 na 5.

Kuhusu hoja #1: Mpaka sasa sijaona assessment yoyote ikionesha impact ya uwekezaji ambao tumeshaufanya katika matangazo ya vivutio vya utalii nchini. Bila kuona hiyo assessment, siwezi ku-support uwekezaji zaidi kwenye matangazo. Huo ni uchochoro wa kuiba hela. Ni nini impact ya kuweka matangazo kwenye viwanja vya EPL? Je watalii wanaokuja nchini wanafanya hivyo kwa kushawishiwa na matangazo? Wanapata wapi habari kuhusu vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania? Unaweza kukuta matangazo tunayolipia mamilioni hayana impact yoyote. Tunafanya mambo kwa mazoea kwa kuwa lengo ni kuiba. Na nahisi kwenye eneo hili tumeibiwa sana. Safari za nje kuhudhuria maonesho ya utalii zimefanyika kiholela sana. Kusema tu serikali ijikite kwa nguvu zote kutangaza utalii ni kutengeneza mazingira ya fedha za umma kuibiwa. Ni lazima kuwa specific na kufanya mambo kwa tija.

Kuhusu hoja #5: Wingi wa vyuo hautatatua tatizo. Actually, utaongeza tatizo kwa kuzalisha utitiri wa watu wasio na sifa. Kinachokosekana ni apprenticeship programs pamoja na certification program. Ili kuwa guide, ni lazima uwe certified kama ambavyo NBAA ina certify wahasibu. Huo utaratibu haupo. Matokeo yake, watu wakifeli shule wanakimbilia kuwa tour guide. Huo ni mfano tu but the same applies to hoteliers, travel agents etc. Biashara ya utalii ni delicate sana. Mgeni akipata experience mbaya, athari ni kubwa. Mtu alipe maelfu ya dola halafu anapata guide mediocre, wanakuwa disappointed sana. Na magaidi wengi ni ujanja ujanja tu. Very few are qualified.

Mkuu nakubaliana na wewe kwa asilimia 100. naamini hayo uliyopendekeza yakifanyiwa kazi tutafika mbali sana kiuchumi
 
Wakati fulani nilikuwa naongea na mmiliki wa kampuni ya utalii kutoka nchini Kenya, akaniambia kwamba kule kwao baada ya kuandamwa na Alshabaab walianzisha kampeni maalum waliyoiita TEMBEA KENYA, Hii kampeni ilianzishwa na serikali yao ili kulinda ajira za wafanyakazi katika sekta ya utalii ambayo iliyumba kiasi cha kutishia ajira za wafanyakazi wengi nchini humo katika sekta hiyo.

Makampuni mengi ya utalii zikiwemo hoteli zilipunguza gharama za safari za utalii na mahoteli pamoja na camps zilipunguza pia gharama za malazi na chakula kwa wazawa na wananchi walihamasishwa kufanya utalii wa ndani ambapo kulikuwa na muitikio mkubwa na serikali katika kuunga mkono kampeni hiyo ilichangia wafanyakazi katika sekta mbalimbali kufanya utalii wa ndani na mikutano na makongamano yalihamishiwa huko ili ku generate revenue katika makampuni ya utalii na mahoteli.

Kampeni hiyo ilipelekea kuzaliwa kwa Kampuni ya Bonfire homepage ambayo ilianzishwa na wajasiriamali wadogo mtu na mkewe bila mtaji mkubwa ambao walianza kwa kuuza safari za utalii kupitia mtandao wa facebook.

Wajasiriamali hawa walianza kwa kupatana na Mahoteli yaliyoko kwenye mbuga za wanyama na camps na ku book vyumba vingi kwa mpigo kisha kuviuza kwa mtindo wa groups kwa gharama nafuu na kuhamasisha wazawa kulipa kidogo kidogo kabla ya safari na hapo mtu anajihakikishia safari yake ya kutalii kwa gharama nafuu zilizopunguzwa kutokana na kuuzwa kwa vyumba vingi kwa mpigo.

Hivi sasa kampuni hiyo ni kubwa na ni miongoni mwa walipa kodi wakubwa nchini humo na sasa imevuka mipaka ambapo sasa inauza safari za nje kama Dubai na nchi za ulaya na Marekani jambo ambalo imejijengea sifa na kutwaa tuzo mbalimbali ikiwemo ile ya Qatar Aiways kutokana na manunuzi ya tickets kwa shirika hilo.

Hii ni changamoto kwa nchi yetu kuruhusu wajasiriamali wadogo kujiingiza kwenye biashara hii kwa kuuza safari za utalii kwa njia ya mitandao ya kijamii ili kujiongezea kipato na kujiimarisha kiuchumi. Tunaweza kuiga wenzetu waliafanya nini kwa mfano tunaweza kujifunza kupitia Kenya na Afrika Kusini.

Iwapo kutawekwa utaratibu mzuri wa kupanua wigo wa wafanyabiashara wa utalii hakika serikali itakusanya fedha nyingi sana za kodi na hivyo uchumi wetu kukua kwa kiwango cha ajabu.

Ombi langu kwa wizara ya Utalii.

Naomba wapitie uzi huu na kuchukua mawazo mazuri ya wadau na kuyafanyia kazi ili nchi yetu isonge mbele. Hii ni nchi yetu sote na tuna wajibu kama wananchi kuishauri serikali ili kujenga uchumi imara utakaonufaisha serikali na wananchi wake na vizazi vijavyo.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.

Ushauri mzuri sana huu.
Naamini wahusika wakiusoma watachukua hatua stahiki na kuufanyia kazi
 
Ha
I Concur and support the thread...

TATO is dead or sleeping deep sleep

TATO wanacharge Flat rate Membership fee, This is very wrong......

TATO ni wavivu, hawataki kujifunza South Africa Association of Tour Operators au KATO ya Kenya...hawa wana categories katika membership

TALA License Flat rate fee n Wrong

Makampuni Makubwa kama Ranger Safaris, Thompson Safaris, Kudu, A & K, Leopard Tours, Zara Travel....wana magari zaidi ya 200, wana wageni zaidi ya 10000 kwa mwaka...How comes walipe TALA License ya 2000 $ sawa na Tour Operator Ndogo

Tour Operator Ndogo wanatakiwa walipe TALA License 1000 $ ili waweze kumudu ushindani na ili wakue...

Tour OPerator Ndogo ni za Wazawa na zinaajiri wazawa....uchumi wa Tanzania unarudi Tanzania

Watanzania wengi wakiingia katika biashara ya utalii, nchi itaingiza FOREX nyingi na pato la utalii litaongezeka kwa serikali

Utitiri wa Kodi...Inatakiwa Serikali iweke kodi moja kwa Tour Operator..yaani kuwe na Kodi moja jumuishi.

Hii Kodi moja ni rahisi kuifuatilia na ukwepaji wa kodi hautakuwepo

Hao wakubwa walipe usd 3000 na wadogo usd 1000.
 
Kukomesha usafirishaji wa wanyama hai kama twiga manake watalii hawaji tena bongo twiga wetu wanapatikana kila mahali duniani, USA, Dubai, Sweden, etc, naomba nikiri kuwa ninamlaani yule mbongo alienzisha utamaduni wa kusafirisha wanyama wetu hai nje ya nchi, huyu ni mtu mbaya sana kuwahi kutokea katika historia ya bongo! Ametuletea mdororo mkubwa wa utalii na umaskini! nashauri serikali kutumia jeshi la wananchi kukomesha ujangili hasa wa tembo na vifaru na kutangaza vita ya ujangili na kuwafunga majangili na kuwatangaza wote wanaoshiriki biashara hii haramu , naamini serikali ina mkono mrefu na mtandao wa majangili unajulikana, kwanini hawatangazwi na tembo wanaisha?

Hebu fikiria tembo alivyo mkubwa watu wanaingia porini na wanaua tembo kwa maelfu, kweli serikali haiwaoni? nilisoma mahali tembo 30 huuwawa kila siku na tembo wamebaki 60,000 toka 150,000 miaka michache tu iliyopita, if this is true jamani we need to be serious manake in few years tembo watabaki picha tu kuwafundishia watoto kama dinosaur! au tutatumia nyumbu tulionao kwa maelfu kuwaambia watoto kuwa hawa ni jamii moja na tembo waliotoweka!

Nashauri serikali kubadili watumishi wa juu wa sekta ya utalii manake waliopo ndio walioifikisha sekta hapa ilipo, wapewe kazi zingine iwekwe timu mpya na targets mpya with specific deadlines, timu hiyo iwekwe chini ya waziri mkuu huyu hana urafiki na wazembe!

Income ya utalii pekee tukiwa serious na hii sekta inatuondolea umaskini! manake tulivyonavyo wengine hawana! mfano Amboni caves haitangazwi kabisa na ni great place! Kukuza utalii wa ndani yani wananchi na wanafunzi wahamasishwe nao kutembelea vivutio vyao, mabalozi wa bongo nje ya nchi wapewe targets za mikutano mingapi ya utalii wahundhurie kwa mwaka huko nchi waliko na waripoti kwa evidence mfano watume presentations zao na minutes za international forums walizohudhuria huko waliko na wataje plan ya namna wanatangaza vivutio vya utalii vya bongo na watoe ripoti za namna wanakanusha taarifa za wale wanaotaja vivutio vya bongo kuwa viko nchini mwao mfano Kenya ni vinara mt kilimanjaro , olduvai gorge husema viko kenya nasi tunakaa kimya tu why?

Mabalozi wagawe vipeperushi vya utalii bongo kwenye nchi walipo mfano nikiwa ulaya niliona mahali kuna studio ya wapiga picha wa kijapani nikaona kuna vipeperushi vya utalii vya kenya!

Nashauri uanzishwe mradi maalum wa kuzalisha wanyama wanaopotea kama dik dik, simba, tembo , vifaru na baadae kuwarudisha mbuga walikotoweka, pale Mkomazi panafaa sana kwa mradi huu, wanyama wanaisha kwa nini tusiwazalishe kama Afrika Kusini ni mafundi katika hili!

Kuweka wanyama wapya sehemu mbalimbali kama viboko nk , kuongeza vyuo vinavyofundisha somo la utalii

Hunting safaris zipigwe marufuku. Tuwe na photographic safaris tu ambazo pia zina pesa nyingi na ujangiri utakwisha kabisa. Kwanza kuua wanyama bila utaratibu ni sadistic na kuna watu wanaiita sporting! Hii ndiyo imemaliza wanyama huko ulaya na marekani. Africa kusini sasa eti kuna ranchi za wanyamapori!!!!!! wanyampori wanatakiwa wawe huru katika makazi yao ya asili ambayo makubwa yamebaki Tanzania tu. TAWA waweke utaratibu wa kupunguza wanyama wanaozidi malisho na wananchi wapate kitoweo cha nyama ya wanyamapori kama enzi za TAWICO.
 
Ushauri mzuri mkuu.
Ahsante sana kwa kushiriki mjadala.
 
Tumtumie Daimond. Mi ndio ushauri wangu japo aseme I am from the country of Serengeti and Kilimanjaro ans Zanzibar
 
Wadau nina M. A ya utalii hapa nakomaa natafuta fursa sijui nitoke vipi ?
Nafikiria nitafute college hizi nikafundishe.
Ngoja nisugue kichwa I am sure nitapata solution.
Ila mtaani kugumu sana aisee dah!! Sijui kwa nini nilichagua kusoma hii course.
 
Tumtumie Daimond. Mi ndio ushauri wangu japo aseme I am from the country of Serengeti and Kilimanjaro ans Zanzibar
Ila mdau kuna fungu lipo la kutangaza utalii wetu.
Unakumbuka ile kula uliwe ya JK? Alikuwa anaongelea kuspend kwenye matangazo ya kiutalii.
 
Tumtumie Daimond. Mi ndio ushauri wangu japo aseme I am from the country of Serengeti and Kilimanjaro ans Zanzibar
Tunahitaji mkakati mahsusi utakaoweza kufanikisha jambo hilo lisije likafanyika kienyeji au kisiasa. Tushirikishe wataalamu katika kutengeneza mapping plan
 
Wadau nina M. A ya utalii hapa nakomaa natafuta fursa sijui nitoke vipi ?
Nafikiria nitafute college hizi nikafundishe.
Ngoja nisugue kichwa I am sure nitapata solution.
Ila mtaani kugumu sana aisee dah!! Sijui kwa nini nilichagua kusoma hii course.
Mkuu kwa kuanza naomba tuwasiliane tutengeneze fursa, haya yanayozungumzwa hapa bila kuthubutu kwa ku approach idara za serikali husika hakuna litakalofanyika.

Tuanze kuonyesha njia, kwamba jambo fulani linawezekana serikali itatukuta tumeashaandaa mazingira wao itakuwa ni jukumu lao kuandaa regulations.
 
Poa Nitakutafuta kiongozi.
Kwanza hii thread ngoja niipitie mwanzo mwisho.
Sikupata muda wa kutulia kuisoma.
Najua kuna mawazo mengi sana ya wadau hapa!
 
Back
Top Bottom