Vivutio vya utalii Tanzania na faida za utalii wa ndani

Vivutio vya utalii Tanzania na faida za utalii wa ndani

Mkuu kwa kuanza naomba tuwasiliane tutengeneze fursa, haya yanayozungumzwa hapa bila kuthubutu kwa ku approach idara za serikali husika hakuna litakalofanyika.

Tuanze kuonyesha njia, kwamba jambo fulani linawezekana serikali itatukuta tumeashaandaa mazingira wao itakuwa ni jukumu lao kuandaa regulations.
upo ok. hivi tz tuna wataalamu washauri wa masoko/advertising/marketing/branding/
 
ningekuwa serikali miji ya Arusha na Moshi Ningeipimp balaa. mitaa yote lami, toa squaters zote, mitaa yote street lights, highways za uhakika kwenda mbuga zote, special police zone, usafi wa hali ya juu nk. kwa mwaka tunapata watalii 1m na wengi huishia mikoa hii. watalii wa siku hizi ni soft, wanataka usalama wa hali ya juu, usafiri bora, miji safi ili apige selfie,huduma za afya fresh, internet ya uhakika kuupload selfies hotel nyingi za bongo kwenye tripadvisor zinalalamikiwa kuhusu internet) nk. watalii wa mbugani wanapungua na wa anasa (Dubai, Paris na Macau) wanaongezeka. lazima tuchanganye ladha za kisasa kwenye miji yetu ya kitalii.
 
Nakubaliana na wew kwa mengi lakini si number 5.

Kabla ya kueleza niseme tu kwa kifupi tumekosa focus katika swala la elimu kwenye sekta ya utalii, hakuna course ambayo ina customise need ya Tanzania, we have different courses zinazokuwa named Tourism lakin zina cover vitu ambavyo saa nyingine vina kuwa hata nje ya Tourism yenyewe. Hatuwaambi wanafunzi ukweli wa wapi wakisoma nin wanakuwa au nin wanaweza kufanya. Na ndicho kinacho fanya kazi nyingi za juu kusimamiwa na wazungu au outsiders. Mimi na wish hawa wadau wote wa elimu wangekaa na wadau wa utalii wajue needs zao then watengeneze courses zinazo siuts needs za utalii. Accounts inafundishwa kwenye vyuo karibu vyote Tanzania na mtu akitoka kwenye hivyo vyuo anaweza kuwa accountant anywhere (of course principles za accounts are the same but tuna weza kufanya bachelor ya tourism ika incooperate vitu vyote na mtu akaweza kufanya kazi popote)

Naomba nikueleze japo kwa kifupi kuhusiana na vyuo hasa nikilenga zaidi vyuo vinavyo toa bachelor kwani kazi za ngazi ya juu kama ulivyo eleza number tano nadhani huwa inaanza either na Diploma ama Bachelor.
Hapa kwetu tuna vyuo vinavyo toa shahada inayohusiana na mambo ya Tourism visivyo pungua vitano kwa utafiti mdogo nilioufanya kipendi cha nyuma. I stand to be corrected with what i will describe hapo chini

1. College of African Wildlife Mweka
Hiki kinatoa Bachelor in Wildlife Tourism focus ukiwa ni kwenye wildlife ukiangalia wanaomaliza hapa wana possibility kubwa kufanya kazi kwenye maeneo ya hifadhi kama National Parks and the likes. Naukiangalia wengi waliajiriwa TANAPA ama Ngorongoro wanatoka Mweka. Hawa hawana knowledge ya travel neither ya marketing

2. University of Dar-es-salaam
Hiki kinatoa Bachelor of Commerce in Tourism and Hospitality Management focus ikiwa kwenye marketing hawa wanaposibility yakufanya kazi kwenye Tanzania Tourist Board as wenyewe wanahusika na marketing ya tourist attraction pia wanauwezo wakufanya kazi kwenye Travel agencies lakin si kwenye national parks. Hawana knowledge ya Wildlife taking into consideration utalii wetu unategemea wanyama kwa kiasi kikubwa hili ni gap, wata market wakati hawana knowledge

3. University of Dodoma na University of Iringa
Hawa wanatoa Bachelor of Art in Tourism and Culture Heritage (UDOM) Bachelor in Cultural Anthropology and Tourism hawa wote focus ikiwa ni kwenye cultural management hawa wana possibility yakufanya kazi kwenye maeneo ya hifadhi yenye vivutio vya asili na wengine hufanya kazi kama maafisa tamaduni kwenye manispaa na wizara ya utamaduni ama wizara ya maliasili na utalii. Pia kuna courses nyingine za UDSM ambazo zinaingia kwenye category hii ambayo ni kama BA in Archaeology na BA in Heritage Management.

4. Open University of Tanzania
Hiki kinatoa Bachelor of Art in Tourism Management focus ikiwa ni kwenye planning although mwanafunzi anapata aspects pia za ujasiria mali. ukiiangali kwa undani hii course sio ya watu wa field kama kufanya kazi kwenye hifadhi kama ilivyo number one most likely nikufanya kazi kama ilivyo number 3.

5. Sebastian Kolowa Memorial University
Hiki kinatoa Bachelor of science in Eco-tourism and Nature Conservation focus ikiwa ni uhifadhi wa wamazingira inataka kufanana kidogo na number 1 but number 1 focuses zaidi kwenye wildlife, hii ina mpaka land use planning na mambo yanayo fanana na hayo. Hii pia inafanana na course ya UDSM inayoitwa BA Geography and Environment Studies haipo specific kwenye kitu kimoja ila ina touuch kila kitu kidogo kidogo kwa kifupi tunasema zipo too general. Hawa wana possibility yakufanya kazi kama wanamazingira na tourism wakiiacha

6. Sokoine University of Agriculture
Hiki kinatoa Bachelor of Tourism Management focus ikiwa ni Travel bachelor yao iko loaded sana na courses za lugha, possibility ya kazi sana sana kwenye travel agencies ambazo kwetu bado hazina nguvu kama zilivyo za wenzetu.

Utafiti huu niliufanya baada ya kuitwa kwenye interview mwaka 2012 na National College of Tourism nikakutana na mtu mmoja anaitwa Naiman Mbise (kama sijakosea jina) (Panelist) mim nikiwa na knowledge ya Tourism on Wildlife na yeye akiwa na knowledge ya Tourism on Travel and Tour guiding....akawa ananiuliza maswali ya travel tulishindwa kuelewana akanijibu kwa kashfa sana kwamba "mnamaliza chuo huku hamjui kitu" iliniuma sana mpaka leo, nikaenda kupitia mtaala wao na wa vyuo vyote hapo juu nikagundua hayo niliyo ya sema hapo. Na wish sana nikutane nae tena

Nawakilisha
 
upo ok. hivi tz tuna wataalamu washauri wa masoko/advertising/marketing/branding/
Wapo wengi kiasi cha kutosha sema tu strategies zao za kutafuta masoko kitaalamu haziko vizuri.
 
Mkuu katika industry niliyopo ya Hospitality wanakuja wanafunzi wengi kufanya mafunzo ya vitendo yaani field lakini ukiangalia uwezo wao wana tofautiana sana na wanafunzi wanaokuja kutoka vyuo vikuu vya nje kwa mfano hapo jirani Kenya au Malaysia na nchi nyinginezo.

Nadhani labda elimu wanayopewa haikidhi au wanafunzi hawapendi kusoma au wanasomea mitihani, Unamuona kabisa mwanafunzi haonyeshi interest ya kujifunza zaidi ya kuwa bize na mitandao ya kijamii na hata report zao wanapeana.

Mimi binafsi nimeshuhudia kuna wanafunzi wengi walipita kwenye eneo langu la kazi waliosomea taaluma ya utalii lakini baada ya hapo ukikutana nao wanafanya kazi tofauti kabisa. lakini tatizo lingine labda ni kuona kazi za utalii kama za kitumwa maana hii industry unyenyekevu ni nguzo kuu ili kujenga mahusiano mazuri na wateja na pia kujihakikishia soko. Naamini labda hili nalo litakuwa ni tatizo.
 
....
  1. kujenga hovyo hovyo mahoteli ndani ya hifadhi bila kutumia EIA
  2. vijiji kuziba ushoroba (Mapito ya wanyama) mfano Tarangire Manyara Selela Esimongori...Arusha National park -Sinya -Amboseli
  3. siasa kushamiri maeneo ya hifadhi
  4. Tour guides kulipwa chini ya viwango
  5. wapambanaji mstari wa mbele tour guides Tour leader kutoshirikishwa kama wadau MUHIMU katika sekta hii
  6. kutokuwepo kwa kituo maalum cha kuwapeleka watalii mfano Tanzania visitors Center
  7. kodi za viwanja vya ndege kuwa juu
  8. sekta zenye mahusiano na utalii kufanya kazi kwa kujitenga
  9. kutowapa mafunzo maalum waongoza Watalii ya kutangaza utalii na vivutio muhimu Tanzania
  10. kutokuwa na watu professinal waliobobea katika biashara ya utalii huku Ng'ambo balozini
  11. kutokuwa na mtandao wa pamoja wa wadau wote wa utalii utakao zungumzia changamoto na kuzitatua
ntakuja baadae wacha nikale mtada na togwaulaya

Namba 2 hapo juu ni tatizo kubwa sana hasa kwenye eneo la Burunge Wildlife Management Area. Kuna wawekezaji wameruhusiwa kujenga mahoteli kwa masharti ya kujenga majengo ya muda( temporary structures) ili wakitakiwa kuondoka wasidai fidia lakini wamejenga majengo ya kudumu na wamekiuka mikataba. Pia wanafanya kazi za tour operators kwa kufanya game drives katika maeneo ya WMA shughuli ambazo ni kinyume cha mikataba yao. Kwa hiyo wasiporekebisha mapungufu hayo wafutiwe mikataba na waondoke katika hayo mapito ya wanyamapori. Pia kuna kijiji ambacho kinataka kujitenga na Burunge WMA. Serikali ikifute kijiji hicho ili hao wanakiji wasiotaka kushirikiana na wenzao wahamishwe na mapito yabaki wazi.
 
Mkuu katika industry niliyopo ya Hospitality wanakuja wanafunzi wengi kufanya mafunzo ya vitendo yaani field lakini ukiangalia uwezo wao wana tofautiana sana na wanafunzi wanaokuja kutoka vyuo vikuu vya nje kwa mfano hapo jirani Kenya au Malaysia na nchi nyinginezo.

Nadhani labda elimu wanayopewa haikidhi au wanafunzi hawapendi kusoma au wanasomea mitihani, Unamuona kabisa mwanafunzi haonyeshi interest ya kujifunza zaidi ya kuwa bize na mitandao ya kijamii na hata report zao wanapeana.

Mimi binafsi nimeshuhudia kuna wanafunzi wengi walipita kwenye eneo langu la kazi waliosomea taaluma ya utalii lakini baada ya hapo ukikutana nao wanafanya kazi tofauti kabisa. lakini tatizo lingine labda ni kuona kazi za utalii kama za kitumwa maana hii industry unyenyekevu ni nguzo kuu ili kujenga mahusiano mazuri na wateja na pia kujihakikishia soko. Naamini labda hili nalo litakuwa ni tatizo.

Mkuu kama kungekuwa na kitufe cha likes 1000x..
Hospitality industry yetu iko pathetic..,unbalanced,imehodhiwa na kundi dogo la wtu aka Cartel..
Hivi mpaka leo waTz tumekariri utalii ni Northern zone circuit tuu??? Serengeti na Ngorongoro kuona Simba??/aargggh
Tuna linchi lenye size ya 945,000 square kilometres....
Kuanzia Masasi mpaka Rusumo kna a thousands of Tourist attractions..
Tumeng'ang'ana na Serengeti na Ngorongoro..ni uhuni tuu wa hiyo Cartel kuinfleunce namna yetu ya kufukiria sababau wao walishaweka mizizi huko..
Arusha kuna kampuni zimeanza in 1950s and 60s..zisitaji majina.."uchochezi"
Zinaoperate kihuni,zinakwepa kodi na zinainfluence mpaka kisiasa..rejea Minister Nyalandu's saga..
Tuwe honest,let us change our perception ya utalii...Mbona Thailand,Malaysia na Indinesia wana mamisitu na beaches wanapokea wataa x10 yetu kwa mwaka...
Nini shida teyu...
Kukariri kwamba utalii pekee ni kupanda mlima au kuon simba...pathetic..
Kuna tourists wa kila aina..Mountain trekkers,sight seers,sun lovers etc..
Tuwe na taasisi independent ya utalii yenye creative mindsets...
Habari ya upande wa Elimu..
Ntapazungumza siki nyingine...
 
View attachment 421962

View attachment 421964

View attachment 421965

Kwa miaka mingi sasa sekta ya utalii nchini imeshindwa kuchangia pato la taifa kama inavyostahili. Kuna changamoto nyingi sana ambazo zimesababisha jambo hilo lakini naomba nitaje chache kisha na wenzangu mnaweza kuchangia na kuishauri serikali hatua za kuchukua ili kuimarisha sekta hii muhimu kwa ustawi wa uchumi wetu.

1. Sekta hii haijatangazwa ipasavyo ndani na nje ya nchi na serikali

2. Sekta hii imekumbatiwa na watu wachache na kupitia umoja wao wameifanya sekta hii kuwa kama mali yao binafsi na ni wao wanaoishauri serikali kuweka masharti magumu ili kuendelea kunufaika wao peke yao.

3. Kuna masharti magumu yanayokwaza wafanyabiashara wadogo kuingia kwenye sekta hii na hivyo kunufaisha wadau wachache

4. Miundo mbinu katika hifadhi zetu ni kikwazo katika kukuza biashara hii ya utalii

5. Vyuo vyetu vya utalii ni vichache vinatoa mafunzo duni yasiyoendana na ukuaji wa sekta hii na wahitimu wengi wanaomaliza kusoma wanakuwa na uwezo wa kufanya kazi za chini na zile nafasi kubwa kushikwa na wageni

6. Kutokuwepo kwa vivutio na mahoteli makubwa katika miji mikuu yenye hadhi ambayo ipo jirani na mbuga zetu za wanyama

7. Kutokuwepo au kutoboreshwa kwa maeneo yenye historia ya miji mbalimbali hapa nchini

8. Maonyesho ya utalii kutopewa kipaumbele na kufanywa katika mikoa miwili tu Kilimanjaro na Arusha

9. Kutokuwepo kwa taarifa za mara kwa mara kuhusu takwimu za watalii wanaoingia nchini na nchi wanazotoka zaidi ya kupatikana kwenye hotuba za waziri bungeni.

10. Ushiriki mdogo wa maonyesho ya utalii nje ambapo serikali haisaidii kuwawezesha wafanyabishara wadogo wa utalii kushiriki maonyesho haya

Nini kifanyike:

1. Serikali ijikite kwa nguvu zote kutangaza utalii katika mataifa mbalimbali ili kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea nchi zetu. Juhudi hizi ziende sambamba na kutoa mialiko maalum kwa watu maarufu duniani kutembelea vivutio vyetu na serikali kuchangia baadhi ya gharama na ziara hizo ziwekwe mwenye vyombo vya habari vya hapa nchini na nje.

2. Kuna fukuto la mgawanyiko katika umoja wa wafanyabiashara ya utalii kati ya wale wafanyabiashara wakubwa na wale wadogo. Na mgawanyiko huu unatokana na wafanyabishara wakubwa kutetea maslahi yao zaidi na kuwaacha wafanya bishara wadogo wakikosa pumzi. Serikali inatakiwa kutengeneza mazingira yatakayowawezesha wafanyabishara wa utalii kuwa na mazingira mazuri ya kufanya bishara zao bila kujali uwezo wao wa kimtaji, lakini pia kuwe na utaratibu wa kuwatambua wafanyabishara wanaouza safari kupitia mitandao ya kijamii na utaratibu huo iwe ni pamoja na kuwapatia leseni na utaratibu wa kulipa kodi, hii itasaidia serikali kuongeza mapato kwa ukusanyaji kodi kwani kwa miaka mingi sekta hii imekuwa ni kichaka cha wafanyabiashara wasio waaminifu kukwepa kodi kwa mbinu mbalimbali, Tunaweza kufanya utafiti kwa nchi kama Afrika Kusini na visiwa vya Mauritius na Shelisheli au Botswana ili kujua wenzetu wamewezaje kuboresha sekta ya utalii katika nchi zao na serikali inanufaikaje na mapato ya utalii katika nchi zao

3. Serikali ilegeze masharti ya kupata leseni za kuanzisha kampuni za utalii kwani siku hizi kuna aina nyingi za kuuza safari ambapo huduma nyingine zinaweza kufanywa na mtu mwingine kama huduma za ndege, huduma za magari kuna makampuni mengi ya kukodisha magari nk. Iwapo serikali itabadilisha masharti ya usajili wa makampuni ya utalii itaongeza wafanyabishara wengi katika sekta hiyo na hivyo kujiongezea kipato cha uhakika.

4. Tuna miundo mbinu mibovu sana katika vivutio vyetu vya utalii na mfano halisi ni ilipo mbuga ya Selous. Hii ni mbuga ambayo ingetumiwa na wageni wanaokuja jijini Dar kutembelea na kuona wanyama mbalimbali ukiwemo mto Rufiji. Hii ni mbuga ambayo ingeweza kutuingizia kipato kama kungetengenezwa mazingira ya kuwepo kwa Treni itakayokuwa inafanya safari zake hadi Kisaki na kurudi kila siku na pale kukawa na Hoteli kubwa na wawekezaji wa utalii wakapewa maeneo ya kujenga ofisi zao na kuboreshwa kwa barabara inayoingia Selous ingerahisisha watalii kutumia treni hadi Kisaki na pale wanapokelewa na kupelekwa mbugani na magari kwa kupitia barabara zilizoboreshwa. Naamini wageni wengi wanaoishi jijini Dar wangetumia fursa hii kutembelea Selous kila mwishoni mwa wiki. Kwa sasa njia ya usafiri wa gari unachukua saa kumi kupitia Matombo na saa 7 kupitia Rufiji ili kuingia mbugani huku ndege ndogo zikitumia dakika 45 lakini ni ghali sana watu wenye kipato cha kawaida kumudu. Serikali inaweza kuwashirikisha wadau wa utalii ili kupata mawazo yao namna nzuri ya kuboresha miundo mbinu yetu katika hifadhi zetu

5. Serikali iongeze vyuo vya utalii ikiwa ni pamoja na kuboresha mitaala ili kuinua elimu inayotolewa na vyuo hivyo. Kwa sasa vyuo vyetu vya utalii ni vichache na elimu inayotolewa humo ni ya kuwaandaa vijana wetu kuja kuwa vibarua na siyo kuwa viongozi katika sekta hiyo. Kwa sasa sekta ya utalii ndiyo inayoajiri wageni wengi kuliko sekta nyingine hapa nchini huku wengine wakiingia na kufanya kazi kiujanja. Tunahitaji mkakati makini ambao utaboresha elimu ya utalii kwa vijana wetu ili kupunguza ukosefu wa ajira. Zipo baadhi ya nafasi katika mahoteli yetu na makampuni ya utalii ili kuzishika labda ukapate elimu hiyo nje ya nchi au upate mafunzo kazini. Hii ni aibu kwa nchi yetu yenye vivutio vingi vya utalii kutegemea nguvu kazi kutoka nje huku vijana wetu wakiendelea kuwa vibarua

6. Tunahitaji katika mikoa ambayo iko karibu na vivutio waalikwe wawekezaji wa kuwekeza katika mahoteli na pia katika mikoa hiyo yatengwe maeneo ya historia ya makabila ya mkoa huo na maeneo mbalimbali yatengwe kwa ajili ya utalii na yaboreshwe ili watalii wanapokuja kabla ya kutembelea vivutio vyetu huko mbugani wapate fursa ya kujifunza utamaduni wa eneo husika na kujua asili ya eneo hilo na watu wake.

7. Serikali kwa kushirikiana na wadau wa utalii iboreshe maeneo yenye historia ya miji mbalimbali hapa nchini na kuitangaza ikiwemo ujenzi wa masanamu ya watu walioacha historia katika miji hiyo kama kule Tabora kina Mtemi Milambo au kina Kishosha Ng’wanamalundi

8. Kuwe na mkakati wa kutoa kipaumbele kwenye maonyesho ya utalii na yawe yanafanywa katika mikoa yote yenye vivutio ili kuimarisha utalii wa ndani hii iwe ni tofauti na ile ya kimataifa inayofanyika Arusha na Moshi, lakini hata hiyo ya Arusha na Moshi inapaswa kuboreshwa kwa kuiga wanavyofanya katika nchi za wenzetu

9. Taarifa za mara kwa mara kuhusu takwimu za watalii wanaoingia nchini na nchi wanazotoka ni muhimu ili kuwarahisishia wafanyabishara wa utalii kujua soko liko wapi, uwepo wa kitengo kitakachokuwa kinakusanya taarifa hizo na kuziweka mtandaoni kutasaidia kujua ni wapi tumejitangaza na wapi hatujajitangaza ili kuelekeza nguvu zetu huko.

10. Kuwe na mkakati wa kuhakikisha wafanyabishara wa utalii wanashiriki kwa wingi kwenye maonyesho ya utalii katika nchi mbalimbali ili kupata fursa ya kutangaza vivutio vyetu.

Naomba nipishe michango mingine kutoka kwa wadau mbalimbali ili tuweze kuishauri serikali namna nzuri ya kuboresha sekta hii ya utalii.

TOVUTI MBALIMBALI ZINAZOHUSU UTALII NCHINI

Tovuti Kuu ya Serikali: Watoa huduma za Utalii

National College of Tourism (NCT) | Tanzania

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Tovuti Kuu ya Serikali: Utalii

Mtambuzi, nimeipenda sana hii mada yako. Inatufanya tufikirie nje ya masanduku. Inatukumbusha kitu ambacho wengi tunakisahau...fursa zinazotuzunguka kila upande...na hatutumii wakati wala nguvu zetu kufuatilia
 
Ahsante mkuu kwa kupita na kutambua mchango wangu katika jambo hili.
 
Ahsante mkuu kwa kupita na kutambua mchango wangu katika jambo hili.

Kama wengi wetu tungekuwa tunaamka asubuhi kila siku na fikra kama hizi, Tanzania ingekuwa mbali sana. Tusitegemee muujiza kama hatuoni hizi fursa zinazotuzunguka
 
TATIZO lipo katika wizara yenyewe

Policy zao na ufanyaji kazi...Wafanyakazi Wizara ya Mali asili ni Miungu watu

Hawana ubunifu wowote, just sitting waiting for salary and travel allowance

Wakienda Travel Fair ni ngono na shopping tu

Ni Ajabu hata Uganda, Kenya na Ethiopia tulingane nao kwa idada ya watalii
 
Utalii umedorora

Ila wanapiga propaganda kuwa wageni wameongezeka.... time will tell

Numbers do not lie
 
Kufikiri mlima kilimanjaro, serengeti na ngorongoro ama mikoa ya kaskazini ndo sehemu pekee kwa ajiri ya utalii ndo tatizo la nchi yetu. Ni mawazo yanayochagizwa 1. Ubinafsi wa watu fulani, 2. Ukosefu wa elimu na 3. Kutokuielewa vizuri nchi yetu.

Hayo ndo matatizo katika kukuza sekta hii. Hivi nchi ya Brazili ina mlima kama Kilimanjaro? ama niulize ni kitu gani kinaifanya Brazil kuwa kati ya nchi zinazofanya vizuri katika utalii? inafahamika ni nchi yenye kuvutia watalii kwasababu kuu moja, beaches zake. Sasa sie watanzania tuna upungufu wa fukwe? kuanzia Bukoba, Musoma, Mwanza kwenda Mtwara, dar, pwani mpaka Tanga. Haya maoneo yote ni fukwe za kutosha na nzuri sana tukiamua kufuta mentality ya u kaskazini, nchi yetu ina tatizo la ubinafsi na kukosa ubunifu
 
Tanzania ina vivutio vingi ila Viongozi wetu ni wavivu kufikiri....Mbaya zaidi hawapokei ushauri...ni Miungu watu..

Ethiopian wana nini cha zaidi hadi watupite kwa watalii karibu million 3?

Kwa nini Kenya tuwapite kwa kura laki moja? inatakiwa Kenya tuwapite kwa kura million 2.

Kenya wana matatizo ya ulinzi.....

Kenya park zao zimechakaa
 
Kufikiri mlima kilimanjaro, serengeti na ngorongoro ama mikoa ya kaskazini ndo sehemu pekee kwa ajiri ya utalii ndo tatizo la nchi yetu. Ni mawazo yanayochagizwa 1. Ubinafsi wa watu fulani, 2. Ukosefu wa elimu na 3. Kutokuielewa vizuri nchi yetu.

Hayo ndo matatizo katika kukuza sekta hii. Hivi nchi ya Brazili ina mlima kama Kilimanjaro? ama niulize ni kitu gani kinaifanya Brazil kuwa kati ya nchi zinazofanya vizuri katika utalii? inafahamika ni nchi yenye kuvutia watalii kwasababu kuu moja, beaches zake. Sasa sie watanzania tuna upungufu wa fukwe? kuanzia Bukoba, Musoma, Mwanza kwenda Mtwara, dar, pwani mpaka Tanga. Haya maoneo yote ni fukwe za kutosha na nzuri sana tukiamua kufuta mentality ya u kaskazini, nchi yetu ina tatizo la ubinafsi na kukosa ubunifu
Mkuu nimekukubali. Ahsante kwa mchango wako
 
Utalii umedorora

Ila wanapiga propaganda kuwa wageni wameongezeka.... time will tell

Numbers do not lie
Ni kama hakuna mkazo uliowekwa kuitangaza sekta hii ni kama vile inajitangaza yenyewe na kama mdau mmoja alivyosema sehemu zilizowekewa kipaumbele ni kanda ya kaskazini yenye wale BIG FIVE na mlima/milima
 
Pia wizara haitoi mwanya kwa wajasriamali wadogo wanaitaka kuingia ktk biashara hiyo rasmi ndio maaana huishia kufanya kazi kinyemela bila hata kulipa kodi..
Mfabo masharti ya leseni ya utalii ni magumu saana ya kuwa na idada ya magari 4x4 na dola 2000 kama ada ya TALA kwa mwaka.

Walau kungekuwa na categories zaidi ili kutoa mwanya kwa wanaotaka kuanza biashara hiyo.
 
Back
Top Bottom