Vivutio vya utalii Tanzania na faida za utalii wa ndani

Vivutio vya utalii Tanzania na faida za utalii wa ndani

Soma Media, Nenda Google search Kigwangala..

Kama wewe ni kilaza, mwombe hata Mke wako, au hata mchepuko akusomee
Umeanza vizuri. Ghafla umeondoka relini. Fuata njia usitawaliwe na hasira unaposema ukweli. Endelea kujenga hoja utaeleweka. Be patient wala usichukulie kill comment ni provocation. Huenda mjibu mada ana nia njema kuku challenge ueleweshe umma zaidi. Take it positively na uchukue kama nafasi ya kuelimisha.
 
Nimekaa nchi fulani ya bara la Asia mwaka mzima utalii wa ndani umekua kwa kasi yaani wewe unaetoka nje unaweza kwenda kutembelea sehemu ukakosa nafasi wamejaa wenyewe tuu! Nilichosikitika zaidi vivutio vyao vingi ni vya kutengeneza sio vya asili kama vyetu lakini wana uzalendo wa kupenda vyao.Ushauri wangu kwa serikali iandae watoto na vijana wa sasa kuwa wazalendo na kuipenda nchi yao ili wawe wajumbe wazuri hapo baadae halafu utalii ni kujitangaza lazima tuwe na mbinu za kujitangaza namaanisha tujitangaze mpaka kuwavutia walio nje na ndani.
 
View attachment 421962

View attachment 421964

View attachment 421965

Kwa miaka mingi sasa sekta ya utalii nchini imeshindwa kuchangia pato la taifa kama inavyostahili. Kuna changamoto nyingi sana ambazo zimesababisha jambo hilo lakini naomba nitaje chache kisha na wenzangu mnaweza kuchangia na kuishauri serikali hatua za kuchukua ili kuimarisha sekta hii muhimu kwa ustawi wa uchumi wetu.

1. Sekta hii haijatangazwa ipasavyo ndani na nje ya nchi na serikali

2. Sekta hii imekumbatiwa na watu wachache na kupitia umoja wao wameifanya sekta hii kuwa kama mali yao binafsi na ni wao wanaoishauri serikali kuweka masharti magumu ili kuendelea kunufaika wao peke yao.

3. Kuna masharti magumu yanayokwaza wafanyabiashara wadogo kuingia kwenye sekta hii na hivyo kunufaisha wadau wachache

4. Miundo mbinu katika hifadhi zetu ni kikwazo katika kukuza biashara hii ya utalii

5. Vyuo vyetu vya utalii ni vichache vinatoa mafunzo duni yasiyoendana na ukuaji wa sekta hii na wahitimu wengi wanaomaliza kusoma wanakuwa na uwezo wa kufanya kazi za chini na zile nafasi kubwa kushikwa na wageni

6. Kutokuwepo kwa vivutio na mahoteli makubwa katika miji mikuu yenye hadhi ambayo ipo jirani na mbuga zetu za wanyama

7. Kutokuwepo au kutoboreshwa kwa maeneo yenye historia ya miji mbalimbali hapa nchini

8. Maonyesho ya utalii kutopewa kipaumbele na kufanywa katika mikoa miwili tu Kilimanjaro na Arusha

9. Kutokuwepo kwa taarifa za mara kwa mara kuhusu takwimu za watalii wanaoingia nchini na nchi wanazotoka zaidi ya kupatikana kwenye hotuba za waziri bungeni.

10. Ushiriki mdogo wa maonyesho ya utalii nje ambapo serikali haisaidii kuwawezesha wafanyabishara wadogo wa utalii kushiriki maonyesho haya

Nini kifanyike:

1. Serikali ijikite kwa nguvu zote kutangaza utalii katika mataifa mbalimbali ili kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea nchi zetu. Juhudi hizi ziende sambamba na kutoa mialiko maalum kwa watu maarufu duniani kutembelea vivutio vyetu na serikali kuchangia baadhi ya gharama na ziara hizo ziwekwe mwenye vyombo vya habari vya hapa nchini na nje.

2. Kuna fukuto la mgawanyiko katika umoja wa wafanyabiashara ya utalii kati ya wale wafanyabiashara wakubwa na wale wadogo. Na mgawanyiko huu unatokana na wafanyabishara wakubwa kutetea maslahi yao zaidi na kuwaacha wafanya bishara wadogo wakikosa pumzi. Serikali inatakiwa kutengeneza mazingira yatakayowawezesha wafanyabishara wa utalii kuwa na mazingira mazuri ya kufanya bishara zao bila kujali uwezo wao wa kimtaji, lakini pia kuwe na utaratibu wa kuwatambua wafanyabishara wanaouza safari kupitia mitandao ya kijamii na utaratibu huo iwe ni pamoja na kuwapatia leseni na utaratibu wa kulipa kodi, hii itasaidia serikali kuongeza mapato kwa ukusanyaji kodi kwani kwa miaka mingi sekta hii imekuwa ni kichaka cha wafanyabiashara wasio waaminifu kukwepa kodi kwa mbinu mbalimbali, Tunaweza kufanya utafiti kwa nchi kama Afrika Kusini na visiwa vya Mauritius na Shelisheli au Botswana ili kujua wenzetu wamewezaje kuboresha sekta ya utalii katika nchi zao na serikali inanufaikaje na mapato ya utalii katika nchi zao

3. Serikali ilegeze masharti ya kupata leseni za kuanzisha kampuni za utalii kwani siku hizi kuna aina nyingi za kuuza safari ambapo huduma nyingine zinaweza kufanywa na mtu mwingine kama huduma za ndege, huduma za magari kuna makampuni mengi ya kukodisha magari nk. Iwapo serikali itabadilisha masharti ya usajili wa makampuni ya utalii itaongeza wafanyabishara wengi katika sekta hiyo na hivyo kujiongezea kipato cha uhakika.

4. Tuna miundo mbinu mibovu sana katika vivutio vyetu vya utalii na mfano halisi ni ilipo mbuga ya Selous. Hii ni mbuga ambayo ingetumiwa na wageni wanaokuja jijini Dar kutembelea na kuona wanyama mbalimbali ukiwemo mto Rufiji. Hii ni mbuga ambayo ingeweza kutuingizia kipato kama kungetengenezwa mazingira ya kuwepo kwa Treni itakayokuwa inafanya safari zake hadi Kisaki na kurudi kila siku na pale kukawa na Hoteli kubwa na wawekezaji wa utalii wakapewa maeneo ya kujenga ofisi zao na kuboreshwa kwa barabara inayoingia Selous ingerahisisha watalii kutumia treni hadi Kisaki na pale wanapokelewa na kupelekwa mbugani na magari kwa kupitia barabara zilizoboreshwa. Naamini wageni wengi wanaoishi jijini Dar wangetumia fursa hii kutembelea Selous kila mwishoni mwa wiki. Kwa sasa njia ya usafiri wa gari unachukua saa kumi kupitia Matombo na saa 7 kupitia Rufiji ili kuingia mbugani huku ndege ndogo zikitumia dakika 45 lakini ni ghali sana watu wenye kipato cha kawaida kumudu. Serikali inaweza kuwashirikisha wadau wa utalii ili kupata mawazo yao namna nzuri ya kuboresha miundo mbinu yetu katika hifadhi zetu

5. Serikali iongeze vyuo vya utalii ikiwa ni pamoja na kuboresha mitaala ili kuinua elimu inayotolewa na vyuo hivyo. Kwa sasa vyuo vyetu vya utalii ni vichache na elimu inayotolewa humo ni ya kuwaandaa vijana wetu kuja kuwa vibarua na siyo kuwa viongozi katika sekta hiyo. Kwa sasa sekta ya utalii ndiyo inayoajiri wageni wengi kuliko sekta nyingine hapa nchini huku wengine wakiingia na kufanya kazi kiujanja. Tunahitaji mkakati makini ambao utaboresha elimu ya utalii kwa vijana wetu ili kupunguza ukosefu wa ajira. Zipo baadhi ya nafasi katika mahoteli yetu na makampuni ya utalii ili kuzishika labda ukapate elimu hiyo nje ya nchi au upate mafunzo kazini. Hii ni aibu kwa nchi yetu yenye vivutio vingi vya utalii kutegemea nguvu kazi kutoka nje huku vijana wetu wakiendelea kuwa vibarua

6. Tunahitaji katika mikoa ambayo iko karibu na vivutio waalikwe wawekezaji wa kuwekeza katika mahoteli na pia katika mikoa hiyo yatengwe maeneo ya historia ya makabila ya mkoa huo na maeneo mbalimbali yatengwe kwa ajili ya utalii na yaboreshwe ili watalii wanapokuja kabla ya kutembelea vivutio vyetu huko mbugani wapate fursa ya kujifunza utamaduni wa eneo husika na kujua asili ya eneo hilo na watu wake.

7. Serikali kwa kushirikiana na wadau wa utalii iboreshe maeneo yenye historia ya miji mbalimbali hapa nchini na kuitangaza ikiwemo ujenzi wa masanamu ya watu walioacha historia katika miji hiyo kama kule Tabora kina Mtemi Milambo au kina Kishosha Ng’wanamalundi

8. Kuwe na mkakati wa kutoa kipaumbele kwenye maonyesho ya utalii na yawe yanafanywa katika mikoa yote yenye vivutio ili kuimarisha utalii wa ndani hii iwe ni tofauti na ile ya kimataifa inayofanyika Arusha na Moshi, lakini hata hiyo ya Arusha na Moshi inapaswa kuboreshwa kwa kuiga wanavyofanya katika nchi za wenzetu

9. Taarifa za mara kwa mara kuhusu takwimu za watalii wanaoingia nchini na nchi wanazotoka ni muhimu ili kuwarahisishia wafanyabishara wa utalii kujua soko liko wapi, uwepo wa kitengo kitakachokuwa kinakusanya taarifa hizo na kuziweka mtandaoni kutasaidia kujua ni wapi tumejitangaza na wapi hatujajitangaza ili kuelekeza nguvu zetu huko.

10. Kuwe na mkakati wa kuhakikisha wafanyabishara wa utalii wanashiriki kwa wingi kwenye maonyesho ya utalii katika nchi mbalimbali ili kupata fursa ya kutangaza vivutio vyetu.

Naomba nipishe michango mingine kutoka kwa wadau mbalimbali ili tuweze kuishauri serikali namna nzuri ya kuboresha sekta hii ya utalii.


TOVUTI MBALIMBALI ZINAZOHUSU UTALII NCHINI

Tovuti Kuu ya Serikali: Watoa huduma za Utalii

National College of Tourism (NCT) | Tanzania

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Tovuti Kuu ya Serikali: Utalii


Umejitahidi kuchambua lakini umesahau hoja moja ya msingi ambayo haisemwi lakini ni ya muhimu sana nayo ni USALAMA. Hata kama yakawepo hayo yote kama hakuna usalama ni kazi bure. Matukio ya kutekwa mauaji au kunyang´anywa mali za watu hususani inapotokea kwa wataliii wenyewe linapoteza watalii wengi sana. Matukio hayo ya utekaji na mauaji yanasambaa na kusababisha hofu kwa watalii. Hakuna ambaye atahatarisha maisha yake, USALAMA ni kitu mihimu sana.
 
Wewe ndo afisa mawasiliano wa tourism industry?
Kama ndiyo, basi Idaara ya maliasili ina budget ya kugharamia kupata taarifa na kero na maoni za wateja, itumie kulipia hii thread then JF mod wapin juu.
Na kama hawataki kugaramia mawazo? Lakini hawajakataza watu kujitolea mawazo.
 
Tozo/kodi nyingi sana.

Elimu yetu hasa watoa huduma bado sana, kitu inaitwa customer care kwa taifa letu hakijapewa kipaumbele kihivyo.
 
Changamoto kubwa inayoikabili sekta hii ambayo hata Mtoa mada imekukamata ni kuthani kuwa utalii Wanyapori na Mlima Kilimanjaro pekee. Hakuna torism product diversification. Katika ngazi ya Kitaifa, maeneo ya yanatumika kama Kumbukumbu za Taifa, Vituo vya Elimu na Mafunzo; na Vivutio vya Utalii. Aidha, katika ngazi ya Kimataifa maeneo ya kihistoria ya Tanzania yamekuwa na umuhimu wa kipekee kutokana na mchango wake katika sekta za kisayansi, kielimu, kiutamaduni na kiuchumi. Umuhimu huu ni pamoja na: kuonesha ushahidi wa Chimbuko na maendeleo ya binadamu (Zinj - Olduvai Gorge); Viumbe na wanyama wengine (Dinosaurs); Vita ya kwanza na Pili ya Dunia; Biashara ya Utumwa na vipusa na kupingwa kwake; Tawala za Kikoloni na kupingwa kwake; matumizi ya zana za mawe; na njia za awali za kuhifadhi Kumbukumbu za matukio kabla ya ugunduzi wa maandish (Nichoro ya Miambani - Kondoa).

Tanzania inasifika Kimataifa kufuatia uvumbuzi wa fuvu la ZAMADAMU aliyeishi miaka milioni 1.75 iliyopita katika Bonde la Olduvai; Nyayo za zamadamu aliyeishi miaka millioni 3.6 iliyopita huko Laetoli; uwepo wa Michoro ya Miambani Kolo -Kondoa; na miji ya kihistoria kama vile Kilwa na Bagamoyo. Aidha, Tanzania imefahamika kupitia ugunduzi wa Mijusi wakubwa (Dinasoria) katika Mkoani ya Lindi (Teandaguru) na Songwe. JE, NI WATALII WANGAPI WANATEMBLEA HAYA MAENEO ? YANA HUDUMA ZA UTALII ? KUMBUKA KUWA SIO LAZIMA SERIKALI ISIMAMIE HAYO MAENEO, SERA NA SHERIA ZINARUHUSU WATU BINAFSI KUPIGA PESA KUPITIA MAENEO HAYO.
 
Asalaam aleikum uliyo yazungumza yote ni sawa kabisa. Nimeona tatizo lingine kubwa na linalo kera kwa watalii waingiapo Julius Kambarage Nyerere Airport. Watalii huwachukua muda wa 3 hours au zaidi ili kupata visa na kulipia yaani unapanga que muda wote 3 hours to 3 hours and a half bila kujali wazee watoto na less able people ambao wa nakuja kutalii na bado wanatozwa 50 dollars each. Na hali hii nimeishudia kwa miaka mingi. Watalii wanashangaa na kuuliza je hii ndio kawaida kutumia zaidi ya masaa matatu na zaidi. Nimeongea na moja wa watalii anasema ametumia 24 hours from Australia via Qatar na hakufurahiswa na ile hali pale. There is no air conditioning no sofas or chairs he said he will think twice kuja tena Tanzania ni jambo linalo udhi na kusikitisha na uonevu kwa wageni hawa. Serikali iliangalie hili kwa jicho la tatu.
 
Natamani hii comment kuihamisha nimplelekee mhusika uso kwa uso atwambie nini kinaendelea. Kuhusu suala la wahindi na wazungu kujazana kwenye sector ya utalii ni dhahiri kwamba sisi wabongo tumeshindwa au hautuwezi. tujitadhimini wapi tunashindwa ili na sisi tuingie kwenye hiki kinyang'anganyiro tuache kutumika kama maboya.
 
Serikali ione umuhimu wa kuanzisha tv channel pekee ya kuonesha vivutio vya utalii vya ndani kama ilivo channel ya Geo wild Animals katika ving'amuzi vya DSTV,AZAM,ZUKU n.k tofauti na kutegemea TBC tu jambo ambalo linaweza kuongeza kiasi cha watalii wanao ingia nchini.
 
Sio wazo baya ila inatakiwa na sisi tuifanye kama kazi kwa kwenda kurekodi wanyama wetu
Kama una hobby hiyo na una camera zako nzuri huwezi kujua unaweza kukutana na maajabu mengi ambapo ni nadra na bahati kuona kinatokea
Wazungu wameuza sana hizi documentary na kuwa na hela ndefu sana.

Let's do it

Sent from my SM using Tapatalk
 
Natamani hii comment kuihamisha nimplelekee mhusika uso kwa uso atwambie nini kinaendelea. Kuhusu suala la wahindi na wazungu kujazana kwenye sector ya utalii ni dhahiri kwamba sisi wabongo tumeshindwa au hautuwezi. tujitadhimini wapi tunashindwa ili na sisi tuingie kwenye hiki kinyang'anganyiro tuache kutumika kama maboya.
safi sana.
 
Asalaam aleikum uliyo yazungumza yote ni sawa kabisa. Nimeona tatizo lingine kubwa na linalo kera kwa watalii waingiapo Julius Kambarage Nyerere Airport. Watalii huwachukua muda wa 3 hours au zaidi ili kupata visa na kulipia yaani unapanga que muda wote 3 hours to 3 hours and a half bila kujali wazee watoto na less able people ambao wa nakuja kutalii na bado wanatozwa 50 dollars each. Na hali hii nimeishudia kwa miaka mingi. Watalii wanashangaa na kuuliza je hii ndio kawaida kutumia zaidi ya masaa matatu na zaidi. Nimeongea na moja wa watalii anasema ametumia 24 hours from Australia via Qatar na hakufurahiswa na ile hali pale. There is no air conditioning no sofas or chairs he said he will think twice kuja tena Tanzania ni jambo linalo udhi na kusikitisha na uonevu kwa wageni hawa. Serikali iliangalie hili kwa jicho la tatu.

Nimemfiikishia mlengwa wa TTB na Imigration pale Airport waifanyie kazi. Kupanga foleni hsta mimi niliona, niliwahi kukaa siku nzima na raia wa Sierra Leon jasho lilinitoka.
 
Nimemfiikishia mlengwa wa TTB na Imigration pale Airport waifanyie kazi. Kupanga foleni hsta mimi niliona, niliwahi kukaa siku nzima na raia wa Sierra Leon jasho lilinitoka.
Na ajabu kubwa ni kwamba watu na viongozi wa naona kama vile wao hawahusiki. Hii hujuma ni kubwa. Nawakumbusha tu viongozi husika ya kwamba airports ndio kioo cha Tanzania. Mtalii (tourist) asipopata mapokezi mazuri hata Holiday yake itakua ruined na ndio ikawa mwisho wa Mtalii kuja kwetu na kutangaza kuwa Tanzania hajapapenda kwa rafiki zake au kwenye mitandao ya kijamii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Adui mkubwa wa hii sector ni ponint number mbili hapo juu. Halafu kibaya zaidi makampuni mengi yakitali hasa pale Arusha inasemekana ni ya majirani zetu.

Sasa nini kifanyike? Mimi nashauri serikali iweke mfumo mzuri na madhubuti wa ukusanyaji wa kodi kwenye hii sector maana dalili zinaonesha kutakuwa na ukwepaji mkubwa wa kodi miongni mwa wafanyabiashara ya utali.

Pili, Wizara ihakikishe ina utangaza utali wa ndani kwanza na kuweka miundombini rafiki ikiwemo kuwa na mabasi maalum kwenye vituo vikubwa
vya mabasi vitakavyokuwa vinasfirisha watu kwa bei nafuu siku za weekend kutembelea hifadhi zetu. Watanzani tunapenda kutembelea hifadhi zetu tatizo ni mlolongo mrefu na wengi hatujui wapi pakuanzi.

Wizara ihakikishe inautangaza vivutio vyetu nje, kwa kutumia michezo, balozi zetu, diaspora, nk.
 
Uko sawa kabisa mkuu. Pia utalii wa ndani muhimu hivyo uhamasishaji ufanyike na gharama zipungue za kuingia katika vivutio mbalimbali hasa vya wanyama na hifadhi za misitu ya asili nchini.
 
Na ajabu kubwa ni kwamba watu na viongozi wa naona kama vile wao hawahusiki. Hii hujuma ni kubwa. Nawakumbusha tu viongozi husika ya kwamba airports ndio kioo cha Tanzania. Mtalii (tourist) asipopata mapokezi mazuri hata Holiday yake itakua ruined na ndio ikawa mwisho wa Mtalii kuja kwetu na kutangaza kuwa Tanzania hajapapenda kwa rafiki zake au kwenye mitandao ya kijamii.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tuendelee kushare information kama hizi, ili wajue na kurekebisha. Mid September nina session na watu wa uhamiaji airport kujua procedures na process za kupata visa.. ili kurahishisha kazi yangu ninayotaka kuianza. Vinginevyo ni janga unaleta wagenni unaishia kuwa stranded. Kupunguza urasimu usiokuwa na tija.
 
Ni vema watanzania tuwe na utaratibu wa kuitangaza nchi yetu kwenye mataifa mbalimbali kwa vile nchi yetu ina vivutio vingi vya kitalii vitakavyo wapendeza watalii watakaotembelea nchini.

#NajivuniaKuwaMtanzania
IMG-20181112-WA0067.jpg
 
Back
Top Bottom