Kwani wapi nimesema utajiri na umasikini ni kipimo sahihi cha ndoa kwa mwanamke?
Kuna watu matajiri wanatafuta wanawake masikini wa kuoa, hawataki kuoa matajiri wenzao. Kwa sababu zao zozote, na kwa hawa ni sawa wakioa mwanamke masikini wa mali na akili. Hicho ndicho wanachotafuta.
Juzi nimeona kuna mtu katoa tangazo hapa JF anatafuta mke, kasema vilema watapewa upendeleo. Huyo mtu ana sababu zake za kusema hivyo.
Nilikuwa namjibu huyu mwanamme asiyependa wanawake tegemezi, na wanaume kama yeye, kwake yeye mwanamke masikini wa mali na akili si mwanamke sahihi wa kuoa.
Kwa sababu mwanamke huyo ni tegemezi, na mwanamme huyu hataki mwanamke tegemezi, hivyo, ni wazi hawataendana.
Ni suala la kufanya match tu ya watu watakaoendana kuepuka mizozo ndani ya ndoa.
Hao masikini wa akili na mali kuna watu wanasema mapenzi ndiyo kitu muhimu, hayo mengine wataelewana ndani ya ndoa, ili mradi kuna mapenzi. Kwa watu kama hao ni sawa kuoa masikini wa akili na mali.
Kuna watu wanaoa kwa kuangalia tako tu. Na hiyo ni haki yao ya kikatiba na kiutu, ilindwe.